Kwa sasa ndio najua kwamba si kila unaemuona anacheka usoni basi ana furaha moyoni, kiubinadamu saa nyingine inabidi tu ujisahaulishe mambo mengine ili maisha yaweze kuendelea na ndiomaana mtu huweza kujivika uso wa tabasamu lakini kuna mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.
For all this time nilikuwa nikienda kazini na kurudi maybe kutoka na marafiki sometimes tukicheka na kufurahi lakini haikuwa na maana kwamba nilikuwa HAPPY kama nilivyokuwa nikionekana, nilikuwa katika mawazo mazito ya kumfikiria baba yangu ambae alikuwa mgonjwa kwa kipindi hiko na mawazo mengi yalikuwa yakiingia na kutoka katika kipindi hiko cha kumuuguza.
Hatimae safari yake ya maisha ikafika mwisho na MUNGU akaamua kumchukua siku ya tarehe 4 april 2010..kazi ya MUNGU haina makosa.. ni siku ambayo SITAWEZA kuisahau katika maisha yangu kwani baba yangu hakuwa baba tu kwangu.. ila alikuwa zaidi ya BABA, My Dad was a big friend to me kiasi cha kuwa free kumueleza tatizo langu lolote.. so kuondoka kwake ni kitu ambacho naweza nikasema kimeni-affect kinamna moja ama nyingine na kimebadilisha mambo mengi katika maisha yangu.
Pamoja na kuondoka kwa mtu muhimu katika maisha yangu lakini bado kuna majukumu ambayo yananikabili na msema kweli mpenzi wa Mungu kichwa changu hakijawahi kuwa wazi kama kilivyo sasahivi, kila ninavyojitahidi kufikiria akili yangu inagota kabisa ni kama MIND yangu iko BLANK kabisa yani. sielewi nini cha kufanya akili yangu imelala kabisa na haitaki kufikiria mbali...
KWA WALE WADAU na wafatiliaji wa BLOG hii mnafkiri tufanye nini kama kuna mtu yoyote ana MAWAZO,MAONI ama MCHANGO wa nini kifanyike ama kizungumziwe ndani ya blog yetu... ungependa kuona nini humu ndani ama tuzungumzie kitu gani kuhusiana na tasnia yetu ama burudani kwa ujumla au chochote kile??? ...msaada tutani tafadhali.. mawazo yenu ni muhimu sana kwangu.
PICHA ZA DADA DINA CARE'S FOUNDATION WAKITEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA
VETERANI
-
Mwisho wa wiki hii kikundi cha Dina Care's tulitembelea kituo cha watoto
yatima cha Veterani kilichopo Temeke na kushinda pia kupata nao chakula cha
mchan...
10 years ago
11 comments:
Hi Zamaradi,
Kwanza pole kwa msiba.Hakuna neno mwafaka la kumwambia mfiwa ambalo litamliwaza kwa asilimia 100.Lakini nachoweza kusema,kwa imani ya sie Wakatoliki,ni kwamba Mungu alimpenda zaidi marehemu na ndio maana akamchukua.Sie wote ni viumbe wake ,na yeye ana mamlaka ya kutuchukua katika muda apendao.
Mie nilifiwa na mama yangu June 2008.Kwa bahati mbaya alipoteza fahamu kabla sijafika kutoka huku nilipo.Na aliendelea kuwa unconsciouss hadi anafariki,meaning sikubahatika kuongea nae japo neno moja.
Tell you what,hadi leo bado naugulia kuondoka kwa mama.However,nimemudu kuacha kulia kila napomkumbuka.Badala yake,kumbukumbu inaponijia nafanya sala kwa ajili yake.
Ni vugumu sana ku-overcome loss of someone who meant everything.Nonetheless,life has to go on.Na pengine hata marehemu asingependa sie tunaoomboleza tushindwe ku-fucntion kwa ajili yake (sio kwa nia mbaya bali kutokana na upendo).
Kwa kifupi,ndugu yangu,jaribu kuangalia yale ambayo marehemu alipenda kuona ukiyafanya then yakazanie.Sio tu yatampa faraja huko aliko bali pia yatakupa liwazo la namna flani.
Pole sana!
Pole sana Zam, maisha ni mitihani na mitihani tumeumbiwa sisi wala si miti. Mshukuru Mwenyezi Mungu wewe amekupa baba mpaka hapo ulipo, wengine hata hatukupata kufaidi raha za baba, tarehe 18/04/1987 sitaisahau kamwe, nilikuwa just std 2.
Innalillah wainnailaihi Rajuun
Muombe Allah akuongoze na akujalie sahau kwa kipindi hiki ili uendelee na kazi, naye ni mwema atakupa muongozo.
disminder.
pole zamaradi nakumbuka jinsi ulivvokua unampenda na kutupa story za marehemu dad wkt tupo shule kampala hilton,naelewa jinsi unavyo jisikia mamii pole sn
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu.
Pole mwenzangu haupo pekee yakao Zamaradi,mimi am November 22 baba yangu alinitoka. Zmaradi huwa nina 2 life ulaya na bongo, nakumbuka mwezi wa 8 nikiwa bongo nilipigiwa cm baba amedondoka chooni na uso ulienda upande, at the same time niliendesha gari mpk kijijini nia kumleta dar kwa matibabu, basi kufika pale akawa kidogo na nafuu ule uso ukawa sawa, ila alikuwa na sukari tokea 24 yrs before basi ikawa inapanda na shuka,nikamuona baba ananafuu nikamuuaga na kuja huku ulaya, bali alikuwa na wadogo zangu na mama kwangu huku nikiwa nawtumia pesa za matumizi n.k mwezi wa kumi akasema anataka kwenda kwake kjjn basi dereva akampeleka kumbe nia yake kwenda kuaga mji wake, the ugonjwa ukaja tena nikapiga simu wakamchukue haraka aje kwa dotor wake, siku hiyo sikulala roho yanituma nikate tiketi nije dar, nikaenda airport, nikapata flat sijamwambia yyte kuwa nakuja dar, maana mama hutoa moyo anaendelea vizuri tu, vile na shuka tu mpka home, nikaongea na bb, mwanao nipo hapa nakupenda baba, basi usiku hali ikabadilika hospitali kcu, baba alfajiri kimya forever, kumbe ni mungu ndio alinileta nimuone mara ya mwisho, hadi leo hii nikikumbuka nalia nalia nalia nilimpenda alinipenda, baba alituunganisha na ndugu zetu sintasau forever. mm ningependa utuletee nyota zenu za magazeti ya nipashe na mwananchi, kwa kishwahili,
pole sana!
Pole mpenzi kwa kuondokewa na mpendwa dad wako. lakini kumbuka kila nafsi itaonja mauti. kwa sasa ni mapemma kurudi ktk hali yako ya kawaida lakini after time utarudi kama kawa. mungu ni mwema amutuumbia kusahau isingekuwa hivyo watu wangekuwa machizi humu duniani.
nakutakia kila la kheri
Zamaradi.
Pole mdogo wangu kwa msiba wa baba yako. Mimi niliondokewa na baba yangu march 2005 sikutegemea ntaacha kulia kwa jinsi nilivyokuwa nalia kila siku. Time heals my dear kwahiyo usijizuie kulia pale unapojisikia kulia, lia. Taratibu machungu yataisha na utakuwa hulii tena.
Kumbuka ibada na yaenzi yote mzee aliyokuwa anayataka.
Pole sana.
ASANTENI SANA jamani kwa moyo wenu wa upendo kwangu na nawashukuru sana kwa maneno yenu ya BUSARA...
Hamjui mmenisaidia kiasi gani ila naweza nikasema kwamba NIMEFARIJIKA SANA....
MUNGU AWABARIKI WOTE.
Pole sana dada najua ni hali ngumu sana kibinadamu , inaumiza unapotokewa na jambo kama hili la kufiwa na mzazi ila mungu atakupa amani kabisa kwa sasa utajisikia kama mwenye mawazo na kufikiria mengi sana but siku zinavyokwenda utajisikia tofauti na mwanzo kabisa memory mbaya zote zitatoka dada yangu na polepole uta recover kabisa na itabaki story kuwa baba alifarikia ila hata ukisema baba alifariki hutakuwa na huzuni tena utaona ni kawaida kabisa maanake maumivu ya moyo mungu anayaponya siku hadi siku , utakaa ukikumbuka maisha mwako kuwa baba alikufa, ila hutalia tena kama ulivyolia siku aliyokufa inakuwa tofauti mungu wetu ni wa ajabu sana kuwa na amani tuu moyoni mwako na muombe mungu kila siku asubuhi uamkapo na usiku ulalapo akupe amani kabisa na kweli utapata amani kabisa , but dont be lonely kupita kiasi it can affect kuwa karibu na watu .
Mungu akusaidie sana na pia akupe moyo wa amani ndani yako surely kila kitu kitakuwa safi .
Ubarikiwe sana.
Ben Alpha
S/KOREA
Pole sana mpenzi naomba Mungu aendelee kuwafariji.
Sarah
Zamaradi, pole sana.
Ni mara ya kwanza kuingia kwenye blog yako na nimesoma habari hii ya kuondokewa na baba yako.
Jipe moyo dada, ni vigumu ila inabidi iwe hivyo, mwenyewe nimempoteza mama yangu mzazi Desemba 2009 najua unavyojisikia. Muhimu kazana ufanye mambo ambayo baba yako alipenda ufanye, hiyo itakupa wewe faraja hata yeye pia. Japo kwa macho ya kawaida humwoni naamini ndani ya moyo wako unajua anayaona utendayo.
Tunaaamini kuwa ipo siku tutakutana na wapendwa wetu.
Post a Comment