Thursday, April 1, 2010

UNATAKA KUWA MUIGIZAJI???kama unapenda kuwa muigizaji huenda ndoto yako ikawa imetimia, baada ya ziara ndefu ya kutafuta waigizaji wa Tamthilia mpya katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, kampuni ya Tuesday Entertainment chini ya mkurugenzi wake Tuesday Kihangala sasa inatafuta vipaji vipya kabisa vya uigizaji katika mkoa wa DAR ES SALAAM.

Usaili utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 11th April 2009 pale NEW MSASANI CLUB jirani na zantel kuanzia saa mbili asubuhi.

Hii ni kwa ajili ya tamthilia mpya kabisa ambayo inategemewa kuwa tishio itakayoitwa MILLOSIS. hii ni kampuni ambayo imeshafanya tamthilia nyingi zilizoweza kushika watu vibaya mno mojawapo ikiwa ni JUMBA LA DHAHABU.

Chukua fomu yako mapema kuanzia sasa katika vituo vifuatavyo

1. SAMAKI SAMAKI - Mlimani City

2. VIJANA SOCIAL HALL - Kinondoni

3. BAHAMA MAMA - Kimara

4. MSASANI CLUB - Drive in.

5. BIGGY RESPECT - Kariakoo

6. ZAKHEM PUB - Mbagala

7. MASHUJAA PUB - Vingunguti

Na usaili utafanyika chini ya madirector wa siku nyingi ambao ni GEORGE TYSON, CHRISSANT MHENGA na TUESDAY KIHANGALA.

1 comment:

Anonymous said...

Hawa ni matapeli, hawana lolote, wanaiba pesa za watu tu. Kwa nini wawatoze wasanii pesa? Kwa nini wasifanye kama RJ COMPANY, au N'GWALUN'GWALU ENTERTAINMENT PROMOTION. Wasanii shitukeni mapema, mnaenda kuibiwa hela zenu.