Monday, June 6, 2011

KITCHEN PARTY - HUSNA..

Jana ilikuwa ni kitchen party ya mshkaji wangu wa siku nyingi sana, anaitwa Husna Shaibu(kushoto) ambae tuliwahi kusoma wote shule moja O' level... Hongera sana mammy ukawe mke mwema huko!!!
Alisimamiwa na Best friend wake anaitwa Neema, Hapo wakikata keki!!
Wanakamati kama ambavyo unatuona.. mpango mzima ulikuwa ni kitenge na kila mtu alishona anavyojisikia kama ambavyo unaona madada walivyopendeza...
Mi niliamua nishone kama ambavyo unaona hapo juu na hivyo ndio nilivyotokea...
Raha ya kitchen Party ndio hii, Mwanamke Nyonga babu mengine haihuuuu... Go ADA, Go ADA, Go Go Go ADA.. Chezea mama MALCOM WEWE.. umetishaaaaaa!!!


Huyu ndio dada wa Bi Harusi anaitwa Jamila!!!
Bi harusi.. hapa sijui ilikuwa nini.. nshasahau.. lol!!!
Mh jamani mpiga picha hata sijajipanga, kashafotoa.. hapo nilipata bahati ya kukutana na school mate wa Enzi hizo.. anaitwa Rukia Haruna Meza mwanafunzi wa UDOM kwasasa!!!
Kutoka kushoto anaitwa TINA (mcharuko), BONITA (ndio ambae ananing'arisha kwenye ma-lace wig), MIMI hapo kati, Na Warembo wengine kama unavyowaona...
Chezea JOHARI wewe.. nae alikuwepo kama DADA wa Bi harusi!!
Ada (mama Malcom), Zamaradi na Jacky Pentzel.. tulikutana huko pia!!!
Zamaradi Mketema na Jacky Pentzel..
Ada, Jacky Pentzel, Zamaradi na Blandina Chagula (johari)
Wadada katika Pozi!!!!
Shughuli ni watu na watu wenyewe ndio sie.. kote kote nipo... hapo na mi nikicheza taarab mwanamke ujue vyote sio uzungu mwanzo mwisho mkataa kwao mtumwa.. chezea.. lol!!!!
Husna alitukutanisha wengi jana.. was really happy to meet you mammy baada ya muda mrefu sana...
Haya sasa mpenda picha.. Swagga is on.. ha haaa..
Nikiwa na Bi harusi hapo.. ma-school mate tulikutana.. It was a good thing sana and and i had alot of fun kukutana tena na watu hawa katika style hii.. maana hii ni baada ya miaka mingi ya kupotezana na kukutana juu kwa juu!!!
baada ya long time kitambo
Hapo ni baada ya kucheza SANA, kiukweli jana nilifurahi sana na kucheza vya kutosha kwenye sherehe hii, bi harusi mwenyewe nae alikuwa Mcharuko, alicheza hatari lol!! hapo tulikuwa tumeshacheza sana tumechoka na kitchen party ndio ilikuwa imeishia hapo.. from left.. Jacky, Zamaradi, Johari na Husna mwenyewe!!!
Hongera mama na kila la kheri kwenye harusi yako.. Ukatulie na mumeo huko!!!

16 comments:

Anonymous said...

umejaribu mwaya

Anonymous said...

zamaradi haukupendeza na hiyo surualina sare ilikuwa rangi mbaya. ila kiuno chao nimekipenda kidogo chenyewe kisichobeba kitambi

Anonymous said...

hata kama ndo uzungu, lkn kuna mavazi mengine yanaendana na shughuli yenyewe jamani, sasa ndo nn kwenye kitchen party kutinga hilo suruali.......yaani umechemsha mbaya, hope next tym utajipanga fresh

Anonymous said...

u look so mwaah.. but that was too much for kitchen party pretty

Anonymous said...

Kwa kuwa nakupenda lazima nikuambie ukweli : Hiyo suruali haikukupendeza kwa kuwa 1. rangi na design haziendani 2. suruali na top haziendani 3. hizo baggy trousers au teitei zinaendana na aina fulani tu ya patterns za rangi. Nawasilisha.

Anonymous said...

kwani kitchen party watu wanaenda wamevaa kaniki? umependeza mpenzi, that is what we call fashion, doing it your way and still look fly

Anonymous said...

KWA KWELI ZAM UMETISHA ILE MBAYA

Anonymous said...

JOHARI NDIO UMEZEEKA HIVYO AU NI PICHA TU MIKOROGO BWANA

Anonymous said...

TATIZO SIRO SARE KWANI HATA INGEKUWA KANIKI NA UKAITENDEA HAKI INGEONEKANA POA TU KWA KWELI MDOGO WETU ZAMARED HAKUPENDEZA MI NAHISI ANGESHONA GAUNI LAKE POA ANGETOKA ILE MBAYA KWANI NAMKUPALI SANA KWENYE MAVAZI

Anonymous said...

KITCHEN PART ILIKUWA ZAMANI SIKU HIZI IMEINGILIA KWELI HAKUNA KINACHOELEWEKA KABISA NI MAMBO YA AJABU MAVAZI YASIOELEWEKA HAYA BWANA YA NGOSWE TUMEUACHIE NGOSWE

Anonymous said...

CYO KILA KIINGIACHO MJINI UNAVAA AU UNASUKA AU UNASHONEA KAMA HUYO JOHARI LANCE WIG HALIJAMTOA WALA AWAACHIE WENGINE KAWA BIBI C BIBI NA HAYO MACREAM CYO KHA.NAMPENDA NDO MANA NAMWAMBIA UKWELI JAMANI.hata kama unapendeza style moja komaa nayo tu yani cyo kubadilisha af unachekesha watu kisa et style imeingia mjini.mtazamo wangu.cu

Anonymous said...

Unajua ujanja ukizidi sana nao unaharibu, ila huna hata washauri kama wewe ulishindwa kujidesign kitu kizuri?? Ni kweli Zam hujapendeza kabisa na pia mpangilio mbovu huo mimi sijaelewa ulikuwa unamaanisha kuvaa nini!!!

Anonymous said...

Zamaradin alipendeza sana jamani acheni wivu wenu. kwa sie tuliokuwepo kwenye hiyo k-party tunajua jinsi alivyotoka bomba.

Anonymous said...

lol zamaradi hujapendeza my dear,kwa mavazi hayo,au ndo skin kitenge?? nakupenda mamy thats why nakwambia. johari umekuwa kinyunyu jamani, umechokaa kama mama mwenye watoto kumi tena asiyekuwa na matunzo.acha cream ridhika jinsi Mungu alivyokuumba,kila cku unachuja

Anonymous said...

Zamaradi mbona umejifotoa sana kupita wenye shughuli?Ki ukweli hujapendeza na wanao kuambia kuwa umependeza wansemea upenzi tu.Jamani kwenye ukweli tuseme ukweli.

Anonymous said...

kiukweli zama umeharibu huna tofauti na asha ngedere au mwajuma ndala ndefu