Friday, May 27, 2011

PART ONE: SAFARI YETU ILIVYOKUWA TUNASHUKURU TUMEFIKA SALAMA TANGA..

Namshukuru sana MUNGU kwa kutufikisha salama TANGA kwani hakuna safari ndogo, waswahili wanasema safari ni safari.. na safari hii ni maalum kabisa kwa ajili ya SERENGETI FIESTA FILAMU ambapo siku ya kesho jumamosi pale LA CASA CHICA kutakuwa na Audition ya kutafuta waigizaji wapya kaisa kwenye filamu kuanzia saa NNE ASUBUHI!!!
Safari yetu ilianza saa kumi na mbili alfajiri na tulikuwa wengiwengi kidogo ambapo tulikuwa na Shafii Dauda ambae nae yuko Tanga kwa ajili ya Soka Bonanza itakayofanyika Jumapili, Wasiwasi Mwabulambo,Jimmy jam, Reginald Maro, Sophia Kessy, Mimi, Haroun, Katunda, Hellen Kazimoto na Peter a.k.a kabaisa...
Hii haikuwa tu safari but it was really FUN kuanzia kwenye gari ambapo watu wengi walicharuka kwelikweli kiufupi ilikuwa furaha tupu kama ambavyo unamuona Mr. Mwabulambo hapo akiwa na Hellen kazimoto, sikumbuki hata ni wimbo gani ulikuwa unachezwa hapo..

SASA SIKILIZIA KILICHOTOKEA BAADA YA HAPO.. HIYO NI PART ONE

3 comments:

mwana said...

jaman wasi wasi naye ana vitukojaman inavyoonekana tu mlienjoy sana kwenye hiyo safari

Anonymous said...

mmh kweli vituko,yaani gari linatembea huku watu wanacheza,nyie vijana punguzeni utundu basi.

SM said...

Hahaaaa, Shafiiiii, naona miwani na udenda vikitoka kwa utamu wa usingizi, waswahili wanasema raha ya kulala kwenye gari ni kumuengemea mwenzio, hao jamaa wamekosa wa kuwaegemea ndo maana full kupinda.Vipi zama hakuna aliyeota kama hivi "Mama naniliu geuka huku nikufinye kidogo" au hakuna aliyetoa hewa chafu hapo kweli?.