Friday, May 27, 2011

PART TWO: MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI.. BAADA YA FUJO NA MBWEMBWE ZA MUDA MREFU HATIMAE HALI IKAWA HIVI...lol!!

Mwanzo wa safari watu hao unaowaona wamelala hawajielewi ndio walikuwa waongeaji kupita kiasi, wacheza show wa nyimbo zote na ndio watu waliokuwa wakionekana wana Energy.. lakini baada ya muda tu kidogo ikawa kwisha habari yao.. na hali yao ikawa mbaya kama unavyowaona hapo.. basi loote likawa KIIMYAAAAA utafikiri sio lile lililokuwa na makelele!!!!!! lol...


NAOMBA NITOE WASIFU WA KILA MMOJA KWENYE SAFARI YETU HII YA LEO...


WASIWASI MWABULAMBO: Huyu ndio alikuwa kinara wa maongezi lakini hapo ujanja wote mfukoni kama unavyomuona, mpaka nampiga picha hapo alikuwa haelewi lolote linaloendelea duniani..
SHAFII DAUDA: ha haaaa.. kazi yake kubwa ilikuwa ni kurequest nyimbo na kusema "hakuna kulala" lakini matokeo yake ndio hayo hapo yanajieleza.. kweli hakuna kulala.. lol!!

KATUNDA: Afadhali hata ya huyu.. mbwembwe hazikuwa nyingi hivyo kulala ni kama haki yake..


PETER a.k.a KABAISA: Ha ha haaaaaaa huyu bwana ndio alikuwa MAIN SPEAKER tulikutana Chalinze akiwa ametokea Morogorokwenye shughuli nyingine lakini safari nzima akaibeba yeye (kimaongezi) utafikiri tumetoka wote DAR lakini maskini hakuchukua round.. sijui alitumia nguvu nyingi kwenye kuongea!!!!!! lol


REGINALD MARO a.k.a P. DIDDY: serengeeti serengeeti.. ey ey ey ey.. ndiomana kuna ule msemo unaosema "KUNYWA KISTAARABU KWANI KUNYWA POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKO" nafikiri nimeeleweka...


HAROUN: huyu hakuwa na mbwembwe sana ila wakati tuko Chalinze alipiga CHAPATI NA MAHARAGE.. sasa sijui ndio SHIBE hiyo ama kuchoka tu sielewi!!!


JIMMY JAM: Maskini Jimmy hajielewi, ye alikuwa anapiga watu picha tu na vituko vyao, naona nguvu ilikuwa ya soda tu kazi ikamshinda matokeo yake na yeye kawa Tukio.. ha haaa... pole brother!!ZAMARADI MKETEMA: Katika watu wagumu kulala wakiwa safarini basi mi mmojawapo... Ukinikuta nimelala basi ntakuwa nimechoka kwelikweli.. mi usingizi wangu huwa naulipizia nikifika nnapoenda.. Hivyo kwenye safari ya leo nafikiri tuliokuwa macho ni MIMI na DREVA tu basi.. WENGINE WOOTE kushnehi.. mpaka Sophia alilala pia Camera tu iliisha charge otherwise nae mngemuona hapa!!!!!


But all in all it was REALLY FUN... nime-enjoy sana safari ya leo, watu wote hao unaowaona hapo juu walinipa Furaha ya kutosha kila mtu akiwa na Burudani yake anayoijua yeye... NAWAPENDA WOOTE!!!
Hii ilikuwa ni kabla ya kuangusha Gari.. Utafikiri sio WAO.. Ha ha haaaaaaaa.... MBIO ZA SAKAFUNI!!!! Hiyo ndio Part TWO ya safari yetu ya leo!!!

3 comments:

Anonymous said...

Hahaaaa kweli zama ulienjoy sana

yna said...

wasi wasiiii ujanja wote mfukoni uko hoi bin taaban.

James said...

Duuh kwa hali dereva angekuwa kama chala boy aliewauwa 5star. sijui ingekuwaje kwani watu wangekufa bila kuiona ajali. msiwaamini sana madeva mjipe zamu za kulala msije mkamliza joseph kussaga