Friday, May 20, 2011

STEPS YATOA MSAADA KWA BONGO MOVIE CLUB..

Mkurugenzi wa STEPS ENTERTAINMENT Mr. Dilesh akizungumza kwenye ukumbi wa habari maelezo siku ya jana ambapo kampuni ya usambazaji ya steps entertainment imetoa misaada mingi tofautitofauti kwa timu ya watu wa filamu ambao wanaenda kucheza mpira wa miguu Mwanza jumapili hii pale CCM kirumba ambapo watacheza na waandishi wa habari wa MWANZA lengo likiwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kununulia madawati kwa shule za msingi za wlaya ya ISAMILO mkoani MWANZA.
Dilesh akimkabidhi Hartman Mbilinyi ambae ni Mwenyekiti wa Club ya watu wa Movie JEZI na vifaa vingine vya michezo.


MECHI HII ITAFANYIKA pale CCM kirumba siku ya Jumapili hii ya keshokutwa hivyo wakazi wa Mwanza mnaombwa mfike kwa wingi sana siku ya JUMAPILI pale CCM kirumba ili kuweza kujionea mechi hiyo kati ya MASTAR WA MOVIES pamoja na waandishi habari wa MWANZA!!!!


1 comment:

Anonymous said...

Huo siyo msaada bali wamebebeshwa mabango ya kibiashara, tatizo watz wanachelelewa sana kuelewa,..
hv hamuoni aibu kutembea huku na kule ukiwa umevaa jacket lenye jina la kampuni fulani? Amkeni jamani...