Thursday, May 12, 2011

MHESHIMIWA RAIS ANANIPA TABU SANA - SIMALENGA

Kama una kumbukumbu nzuri huenda umeshaiona hii sura zamani kidogo enzi hizo kwenye tamthilia ya kaole ambapo alikuwa akitambulika kama Mr. DIMERA, lakini jina halisi ni SIMON SIMALENGA ambapo kwa sasa ameachana na mambo ya maigizo na yuko hapa CLOUDS FM RADIO kama PRODUCER wa vipindi vya NJIAPANDA pamoja na JAHAZI ingawa pia hufanya na vipindi vingine lakini pia ni Mwanafunzi wa MWL NYERERE MEMORIAL ACADEMY ambapo anachukua Bachelor in POLITICS.
Alizaliwa miaka 35 iliyopita huko Njombe mkoa wa IRINGA, na elimu yake ya msingi aliipatia Tengero priamry School huko Morogoro Vijijini wilaya ya Mgeta na hiyo ilikuwa 1987 - 1993.
Baada ya hapo alipumzika kidogo mpaka mwaka 2004 alivyokuja kujiendeleza kwa kufanya Special Programs kama Private Candidate ambapo alisoma miaka miwili kwa minne.. Na baada ya hapo alichukua ADVANCE CERTIFICATE in Journalism na kisha akachukua DIPLOMA in JOURNALISM na kisha akajikuta ameingia kwenye sanaa mpaka alipokuja kuacha na kujunga na Tasnia ya Habari...

QN: TOFAUTI YA KAZI YAKE YA ZAMANI(MAIGIZO) NA YA SASA NI NINI??
ANS: Wakati nafanya maigizo nilikuwa na malengo ya kuwafikia baadhi ya watu (kiserikali na kijamii) na kwa kipindi hiko ilikuwa ni vigumu ingawa hao watu niliotaka kuwafikia huenda wao walikuwa wakiniona kutokana na kazi yangu(maigizo) ila mimi ilikuwa ni vigumu kwa upande wangu kuwafikia, LAKINI kwasasa imekuwa rahisi kuwafikia kutokana na kazi ninayofanya ingawa vyote hivi navifanya kwa malengo fulani, kwani bado kabisa sijafika ninapotaka kufika na ili niweze kufika ninapopataka hatua nyingine niliyofanya ni kurudi shule ambapo kwasasa nasoma MWL JK NYERERE MEMORIAL kama nilivyosema awali.

QN: MALENGO YAKO NI NINI HASA!!??
ANS: Malengo yangu hasa ni kuwa MWANASIASA, na ninaposema mwanasiasa si uanasiasa tu, ila mwanasasa mwenye nia ya dhati ya kutekeleza kile ninachokiona kina upungufu kwenye jamii.
QN: WEWE NI MTU WA AINA GANI!??
ANS: Kwakweli mi ni mtu ambae kwenye Starehe SIPO KABISA, na hata ukisikia kuna wimbo umetoka mpya halafu mi naujua basi ujue huo wimbo ni Mzuri kwelikweli maana mi si mfatiliaji kabisa wa hayo mambo.. Na pia napenda kufatilia nmustakabali wa taifa letu na nini kinaendelea kitaifa hata kama ni kidogo hakiwezi kunipita, ingawa kitu kingine ambacho napenda kidogo labda MOVIES, tena aina ya movies ninazopenda ni zile za KIPELELEZI.

QN: NI NINI UNACHUKIA!!??
ANS: Nachukia sana mtu kutokua serious, sipendi mtu ambae ana mzaha mzaha mwingi, mtu ambae hayuko makini, anaamka hata hajui nini kilitokea jana kiufupi huwezi kunikuta karibu na mtu wa aina hiyo, mtu ambae hayuko Current.

QN: NI KITU GANI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO!??
ANS: Nchi yangu na watu wake.

QN: KITU GANI CHA AJABU ALICHOWAHI KUFANYA NA HUENDA ANAKIJUTIA!!??
ANS: Kupata Mtoto Nje ya Ndoa, hiko ndio kitu ninachojutia ingawa haina maana kwamba simpendi mtoto wangu, nampenda sana ila tu SIKUPLAN.

QN: Tofauti ya kazi yake ya zamani(maigizo) na sasa ni nini!??
ANS: Wakati nafanya maigizo nilikuwa na malengo ya kuwafikia baadhi ya watu (kiserikali na kijamii) na kwa kipindi hiko ilikuwa ni vigumu ingawa hao watu niliotaka kuwafikia huenda wao walikuwa wakiniona kutokana na kazi yangu(maigizo) ila mimi ilikuwa ni vigumu kwa upande wangu kuwafikia, LAKINI kwasasa imekuwa rahisi kuwafikia kutokana na kazi ninayofanya ingawa vyote hivi navifanya kwa malengo fulani, kwani bado kabisa sijafika ninapotaka kufika na ili niweze kufika ninapopataka hatua nyingine niliyofanya ni kurudi shule ambapo kwasasa nasoma MWL JK NYERERE MEMORIAL kama nilivyosema awali.

QN: MALENGO YAKO NI NINI HASA!!??
ANS: Malengo yangu hasa ni kuwa MWANASIASA, na ninaposema mwanasiasa si uanasiasa tu, ila mwanasasa mwenye nia ya dhati ya kutekeleza kile ninachokiona kina upungufu kwenye jamii.

QN: WEWE NI MTU WA AINA GANI!??
ANS: Kwakweli mi ni mtu ambae kwenye Starehe SIPO KABISA, na hata ukisikia kuna wimbo umetoka mpya halafu mi naujua basi ujue huo wimbo ni Mzuri kwelikweli maana mi si mfatiliaji kabisa wa hayo mambo.. Na pia napenda kufatilia nmustakabali wa taifa letu na nini kinaendelea kitaifa hata kama ni kidogo hakiwezi kunipita, ingawa kitu kingine ambacho napenda kidogo labda MOVIES, tena aina ya movies ninazopenda ni zile za KIPELELEZI.

QN: NI NINI UNACHUKIA!!??
ANS: Nachukia sana mtu kutokua serious, sipendi mtu ambae ana mzaha mzaha mwingi, mtu ambae hayuko makini, anaamka hata hajui nini kilitokea jana kiufupi huwezi kunikuta karibu na mtu wa aina hiyo, mtu ambae hayuko Current.

QN: NI KITU GANI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YAKO!??
ANS: Nchi yangu na watu wake.

QN: KITU GANI CHA AJABU ALICHOWAHI KUFANYA NA HUENDA ANAKIJUTIA!!??
ANS: Kupata Mtoto Nje ya Ndoa, hiko ndio kitu ninachojutia ingawa haina maana kwamba simpendi mtoto wangu, nampenda sana ila tu SIKUPANGA kupata mtoto.

QN: NI NINI UNATAMANI KUULIZWA NA HUJAWAHI KUULIZWA POPOTE!!??
ANS: Ni kuhusu SIKU YANGU YA KUZALIWA, Sijawahi kuulizwa na mtu ninajisikiaje ikifika siku yangu ya kuzaliwa... Kiukweli kabisa SIJAWAHI KUJISIKIA VIZURI kwenye siku yangu ya kuzaliwa, sababu inaweza ikawa ya kipuuzi lakini kwangu ni ya msingi, Kwanza kabisa naona muda unakwenda hivyo najihisi nina deni na changamoto kubwa sana kwa jamii ya kitanzania kwani mimi kama kijana najihisi sijatoa mchango kwa kiasi cha kutosha hata kwa jamii inayonizunguka, hiyo ndio sababu kubwa.

QN: KITU GANI HATUJUI KUTOKA KWAKO??
ANS: Sijawahi kufanya Birthday katika maisha yangu na wala sitegemei.

QN: KINGINE TUSICHOKIJUA??
ANS: Kuna mtu ananipa Tabu sana kwenye maisha yangu, na huyu si mwingine ila ni Muheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JAKAYA MRISHO KIKWETE, na kikubwa kinachonipa tabu kutoka kwa huyu mtu ni kwamba huwa natamani sana kujua kama ningekuwa na uwezo ningeweza kuingia kwenye kichwa chake ili nione tu muda wote NI NINI AMBACHO HUWA ANAFIKIRIA AMA KUWAZA, natamani sana kujua muheshimiwa rais huwa anawaza nini na pia nijue ni Mtu wa aina gani sababu huwa anabadilikabadilika sana, mara nyingine huwa charming na mara nyingine huwa tofauti kabisa, na nashkuru kwa mwaka huu nimepata bahati ya kuonana nae zaidi ya mara tatu lakini bado kuna kitu huwa kinanipa tabu sana juu yake sababu sijawahi kuongea ambacho ninacho kwenye kichwa changu (ninachotaka/tamani kumwambia).

QN: NANI ANAKU-INSPIRE??
ANS: Mh. Jakaya Mrisho Kikwete huwa anani-insipire sana, naweza nikasema hata kurudi kwangu shule kumechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na yeye, na ilikuwa nisomee sheria lakini nikaona nikisomea sheria itakuwa ngumu sana kumfikia hivyo nikaona nisomee habari na kwa kupitia hilo nashukuru nimeweza kuonana nae zaidi ya mara tatu kwa mwaka jana ingawa sijawahi kuongea ambacho ninacho kwenye kichwa changu.

QN: TOFAUTI YA ALICHOKUWA AKIKIFANYA ZAMANI NA SASA??
ANS: Zamani nilipokuwa kwenye maigizo ilikuwa tunatumia kipaji lakini ilikuwa ngumu sana kutumia akili yako kuweka ubunifu.. mambo mengi yalikuwa yanaendeshwa na kipaji zaidi na hiyo ilitokana na watu waliokuwa wakinizunguka, lakini kwasasa angalau kati ya ASILIMIA 100 angalau natumia hata 45% ya ubongo wangu katika kufanya mambo tofautitofauti, na hata sehemu ninayofanyia kazi inanipa uhuru wa mimi kufanya kazi yangu vizuri na haikulimit katika kufikiria. na kizuri zaidi kinachonifurahisha nina uhuru hata wa kujiendeleza kielimu tofauti na makampuni mengine ambayo ukisema unaenda kusoma basi ni kama umejifukuzisha kazi mwenyewe.

QN: KATIKA WATU WOTE ALIOWAHI KUWAHOJI, NI WATU GANI ALIFURAHI SANA KUHOJIANA NAO??
ANS: Mheshimiwa Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE, Profesa ANA TIBAIJUKA, pamoja na WAZIRI WA MAMBO YA NJE mh. BENARD MEMBE.

QN: MWISHO KABISA UNA CHOCHOTE CHA KUONGEA??
ANS: HUWA NAKERWA SANA na Baadhi ya MAWAZIRI, MANAIBU na MAKATIBU WAKUU WA WIZARA mbalimbali ambao hufanya baadhi ya taarifa za kiserikali kuwa SIRI.. wakati mara nyingi ninapotaka mahojiano nao huwa ni kwa nia njema na kwa maslahi ya taifa

12 comments:

Anonymous said...

we simalenga inaelekea kabisaa utakuwa mwanasiasa atakayetisha hapo baadae,ila bahati mbaya mie siipendi ccm so kutoka na hilo hata huyo raisi mwenyewe hapandi kabisaaaa

mtukutu said...

huyo kikwete naye mda mwingine namshangaa sana,kuna msiba mmoja alikwepo alafu anaonyesha smilling face,kwa kweli nilistuka sana.

Anonymous said...

nakutaskia kila la kheri kaka Mungu awe nawe kwa kila jambo inashallah utafikia malengo yako

Anonymous said...

Unachohitaji ni kujichanganya na watu. Naona Socolization kwako ni ngumu. Sio lazima ujirushe kwa kunywa bia au kwenda club unachohiyaji ni kuwa na watu mbalimbali.

Anonymous said...

DUUH KAMA NDIO HIVYO ANAONEKANA MTU BORING SANA UKIKAA NAYE YUKO SERIOUS, HAPENDI STAREHE, HATA MUZIKI, WALA HAPENDIMTU MWENYE UTANIUTANI NA MCHESHI, KILICHONIUA NI KUA HATA MOVIE ZAKE NI KIPELELLEZI TUU HATAKI HATA ZINGINE , MWE MKEO ATAKOMA

Mdanganyika said...

Hongera sana Simon,kwa kurudi shule na kupiga hatua moja mbele,coz kwa aina yako ya uigizaji ni taabu kidogo kuliteka soko la hapa Bongo,wapenda bongo movie hawapendi aina yako ya uigizaji,watu hawapendi vitu vya kuumiza kichwa,mambo yaDowans,Epa,Kagoda,sijui waziri gani si mtendaji uku uswazi kwenye mashabiki wa izo movie sio sehemu yako...mashabiki wa Bongo movie wanapenda trivial issues,komedi na mengineyo.

Unasema hupendi mtu ambae sio current,how?wewe mwenyewe umesema hupendi burudani,au kupenda,kufatilia mambo ya siasa ndo kuwa-current?Mkapa alitujengea national stadium japo alikuwa hapendi michezo,ndo maana aliteguka nyonga,akaenda kutibiwa UK kwa kodi zetu wadanyanyika.Enzi za mwalimu Nyerere alisema siasa ni wito,ile hali ya kupenda kutumikia watu kwa uadilifu,na si ile hali ya kutamani maisha ya wizi na ulafi wa wanasiasa wa leo.Kuhusu JK,ana-inspire watu wengi tu,ata mie nilikuwa mmoja wao enzi zile za tumaini lililorejea ya maisha bora kwa kila Mtanzania.Lkn mkuu wa kaya hayupo ivyo,ndo maana ata wewe umesema humuelewielewi.JK ana KARAMA,icho ni kitu adimu,mara nyingi uzaliwa nacho.JK anapendwa,ana kipaji cha kuongea na kushawishi,kupanga mikakati na kuonesha njia kinadhalia,ndo maana mpaka leo mna amini mkuu wa kaya anaangushwa na wasaidizi wake aliowachagua mwenyewe.Mie naamini JK kwa karama aliyonayo,alijaribu kushawishi watu kutimiza ndoto yake ya kuwa mkuu wa kaya,na si uwezo alionao kutuondolea dhiki hii sie wadanganyika,kwa kusema ivyo JK ataondoka madarakani bila kuwa na jambo la kujivunia zaidi ya kumbeba Anna Makinda kuwa spika wa kwanza mwanamke,Lowassa kuwa waziri mkuu mstaafu,Rostam mweka hazina wa chama,Karamagi mkataba mnono wa TICS,Chenge vijisenti na pasenti za Rada na ndege ya rais,kumchomeka kwenye chama na serikali Ridhiwani(young billionaire),kumkubalia Bi Salma kuanzisha WAMA ili ajilimbikizie mali yeye,familia yake na rafiki zake kina Zakia Meghi,Regina Lowassa,Mwanaidi Majaar,Sophia Simba,Blandina Nyoni,Hulda Kibacha etc.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Pam said...

kaka kazi na dawa being serious in life bila kupata japo wasaa wa kuburudika ni tatizo kisaikolojia ongea na yule mama wa kipindi na Dina akupe ushauri there must be something wrong with u..
shule muhimu kwa hilo nakupongeza kwa juhudi umenitia moyo hata mie haijalishi umri umesogea.kila la heri katika azma yako ya kuwa mwanasiasa unaejali.

Watu mnapenda sifa sana au unadhani atakupa ubunge kiti maalum hivyo ni maalum kwa wanawake naungana na mdau wa kwanza kwamba kikwete alichojaliwa ni kushawishi watu wampe urasi basi, hana kingine cha ziada, amalize hiyo miaka yake aondoke tumemchoka nchi ameichafua kwa kuendekeza marafiki na ndugu zake sasa hapa ikulu pamekuwa kama chooni kila mtu ana amri kuanzia mama hadi watoto, nyie mlioko nje hamjui tuulizeni sisi wa ndani ikulu haina heshima tena kama enzi ya nyerere na mkapa,

me sina la kuongeza watu wenye akili sana (big up!) wote hapo juu wamemaliza. labda cha nyongeza ni kwamba mshkaji akiendelea na hulka hii ya kuwa serious anaweza pata msongo mkubwa wa mawazo pale ishu zake zisipokwenda kama alivyotaraji na kupata mental breakdown. kama anabisha ajaribu kuulizia watu wenye maarifa na tabia za watu..mdau

Anonymous said...

Huyo jamaaa ni mshamba as far as I know anajipendekeza kwa wanasiasa na kuwalamba miguu( kumbuka mwaka jana kabla ya uchaguzi na mashati yake ya kijani. The thing brother huna mvuto wowote wa kuwa kiongozi sababu huna uwezo wa kujenga hoja na kuisimamia. My Take.. You are living in a dream that will never come true politics don't work that way kwa kuwaza kuwa ndani ya kichwa cha raisi hizo kauli waachie watoto wa shule za msingi.Na nimekuona mgonjwa zaidi pale unaposema unajutia kupata mtoto nje ya ndoa. SHIT!! Responsible fathers don't say that kinda crap. How would the child feel akisoma hizo kauli zako. Kwa kifupi una matatizo ya kisaikolojia you are a ''LONER"". You don't even like your birthdays Cmon.. Hupendi watu wenye mzaha wakati huyo Mkwere unaemfagilia ni zaidi ya mzaha.. Ulichelewa sana kuja mjini na standard seven yako ungewahi mapema.. Kingine umeshindwa kusoma sheria sababu you don't have the qualifications mkubwa usidanganye watu umeamua kusoma politics ili ufikie watu, sheria lazima uwe umefaulu lugha na history advanced level ambayo wewe hukusoma.. I hate HYPOCRITES....