Friday, May 27, 2011

NINA FURAHA KULIKO KAWAIDA KUKUTANA NA MTU HUYU LEO....

Ukiniuliza Mchekeshaji ninaempenda hapa Tanzania kiukweli kabisa jina la huyu mzee ndio litakuwa la kwanza halafu wengine ndio watafuata, anaitwa KING MAJUTO mmoja kati ya wachekeshaji wa muda mrefu sana hapa Tanzania na Asiechuja machoni mwa watu wengi.. Kuna mengi sana ambayo napenda kutoka kwa huyu mzee kiasi kwamba leo nilivyomuona tu nilishindwa kujizuia kucheka....
Nakumbuka wakati nikiwa mdogo nilikuwa nikihudhuria sana maigizo yao ya jukwaani enzi hizo akiwa katika kundi la Muungano cultural troupe ambapo kila jumamosi pale Vijana social hall kinondoni ndio ilikuwa sehemu yao ya kufanyia maonesho, na baba alikuwa akipenda sana kunipeleka pale kushangaashangaa maigizo na MZEE MAJUTO ndio nilimuonea hapo kwa mara ya kwanza ambapo kwa enzi hizo alikuwa akiigiza serious na kingine alipenda sana kuigiza kama anaonewa hivi na mtu wa matatizo na sio comedy kama ambavyo anafanya sasa, lakini baadae nikaanza kumuona kwenye comedy enzi hizo kwenye television na mpaka sasa kupitia DVDs mbalimbali...
Naweza nikasema kwamba namuheshimu sana huyu mtu, na naweza kusema yeye kama yeye mbali na jina alilonalo amejijengea Heshima kubwa sana kupitia fani yake hiyo, mi naweza nikamuita LEGENDARY kwenye sanaa nzima ya Vichekesho...


Mbali na kuwa kipenzi changu Mzee Majuto alikuwa kipenzi sana cha baba yangu, enzi za uhai wa baba yangu hakuwa mtu wa kupenda kuangalia TV ama hata movies lakini ukiweka DVD ya mzee Majuto utakaa nae Mwanzo mpaka mwisho na atacheka mpaka utasikia raha, so kukutana na mzee Majuto kumenikumbusha mbali sana na nimefurahi sana kukutana nae leo...


I was not in a good mood kabisa before na nilikuwa na mambo yangu mengi sana kichwani lakini kukutana nae tu imekuwa kama dawa kwangu naomba nikiri, He made my day aisee...


MUCH RESPECT TO YOU!!!!

5 comments:

Anonymous said...

huyo jamaa acha, yani anachekesha huyo balaa, sema kazaliwa nchi siyo ingekuwa nchi za wenzetu wanaojali vipaji vya watu huyo ni tajiri balaa, ndiyo hivyo bwana, mie nilikuwa naendaga muongano na kibisa alikuwa huyo na jamaaa anaitwa blanco yani take usitake utacheka, halafu majuta enzi hizo kila maigizo yake anaimba, basi mie na mshikaji wangu tukawa tunamwita mitchun wa bongo, namuusudu sana king majuto.

hivi Zamaradi umeolewa?

Zamaradi said...

Wewe kweli uko deep.. ni kweli kwa kipindi hiko alikuwa kila akimaliza kuigiza lazima aimbe... ha haa.. umenikumbusha mbali sana aisee!!
Kuhusu swali lako mimi sijaolewa ila nina mtu NINAEMPENDA SANA..
Asante kwa kutembelea blog
tuko Pamoja.

Anonymous said...

asante dada zamaradi kwakutuwekea habari ya king majuto hata kwa upande wagu namzimia sana huyu mzee kwa vichekesho vyake nina swali dada zamaradi je hiyo inayoonekana ni nyumba yake? naje hawo watoto hapo ni wakwake? ni hayo tu naomba jibu mpendwa ubarikiwe

Zamaradi said...

hapana.. hapo sio kwake ila ni sehemu tu waliyokuwa wakitumia kuigizia (location) na hata hao watoto sio wake kabisa.
Asante!!

SEBO said...

...nimeguswa sana na umenikumbusha mbali uliposema ulipomuona huyo mzee ulimkumbuka baba,pole sana....pia nimefrahishwa na picha pamoja na maelezo ya ndugu zetu ulokuwa nao safarini..hahaha.