Thursday, June 17, 2010

NIMEAMUA KUIGIZA SHOGA - TINO

Msanii wa filamu za Kitanzania Hissan Muya maarufu kama Tino ameamua kuja kitofauti kabisa na kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa na msanii yoyote wa filamu hapa Tanzania kwa kuamua KUIGIZA KAMA SHOGA...

Huu ni ujasiri wa hali ya juu aliouonesha kwasababu nimeweza kuongea na baadhi ya wasanii wa kiume kama JB, CLAUDE, CHENI na wengineo na katika hao wote wengi wao walisema hawawezi kuigiza kama mashoga though mwisho wa siku ni sanaa tu.

Tangu kitu hiki kisemwe kupitia kipindi cha Movie leo ya clouds FM kumekuwa na MZOZO na GUMZO kubwa ambalo limeibuka baina ya watu wengi wakidai kwamba si sawa na wengine wakisema sawa..

Kwako wewe unaonaje!!???? Ni sawa mwanaume kuigiza kama Shoga??

6 comments:

Anonymous said...

MAMA ISLAAH,MABIBO

Kusema kweli haipendezi kwa mwanaume rijali kuigiza kama shoga cos sio jambo zuri katika jamii, japo hatujafahamu mwisho wa siku filamu hiyo itakuwa inamzungumziaje huyo shoga ila mimi binafsi sioni kama ni jambo zuri, labda kama huyo ecta anataka kusema katika maudhui yake kama ndio hivyo au ni mimi hisia zangu; ktk kuact kwake labda akiwa mtoto alikuwa anafanyiwa kwa kutishiwa kupigwa au jambo lolote baya na mtu anaye mfanyia halafu ile hali ikaendelea hadi anakuwa mkubwa, kimtazamo nina maana hii kuwa mashoga wote sio huwa wanapenda wengine ndio hivyo huanzishwa wakiwa watoto unakuta hadi wanafikia utu uzima anaendelea na hali ile cos anakuwa amekwisha haribika ,kama maudhui yake ni hayo itakuwa poa na itakuwa inawaelimisha wengine wasiojua madhara ya ushoga au vipi mtu anakuwa shoga,japo wapo wengine hupenda kwa tamaa zao za kutaka mambo makubwa kuliko uwezo wao unakuta wanafanya mabo hayo ili waweze kufanikisha kile wakitakacho kwa wakati huo.
ila ni kumuomba M.Mungu atuepushie na watoto wetu maana dunia inakokwenda ni hatari kubwa kwa watoto wetu.

Anonymous said...

Kwa huyo tino na afanye tu.....hamna neno.

Anonymous said...

Nafasi ndiyo hasaaaa kwa huo mkorogo na vipodozi vya kaka zetu wa bongo

Anonymous said...

Kama ni msanii lazima awe tayari kufanya kazi mbalimbali, mwisho was siku kama mtu ni shoga, basi ni shoga sidhani kwamba kwa yeye kuigiza ndio kutamfanya awe shoga. Kiukweli ni kwamba ushoga upo na magazetini yanaongelewa hata ya humu nchini. Tatizo letu watanzania tunapenda kufumbia macho vitu ambavyo vinaonekana badala ya kukubali ukweli na matukio. Sioni ni jambo baya kwa yeye Tino kuigiza kama shoga. Filamu hiyo itategemeana na hadithi yenyewe. Mbona watu hupenda kuangalia hizi series za kina mamushka na zimejaa mashoga wa kila aina, na watu hufurahia na kila siku saa nne usiku lazima waangalie? Ni sababu story line inakua inaelezea mambo mengi ya maisha ya binadamu. Huu ni mtazamo wangu tu binafsi.

Jane, Magomeni

Anonymous said...

ili uwe msanii wa kukubalika ni lazima uwe tayari kuigiza nafasi yeyote utayopewa na uperform to the best of it, mbona tumeona kina Will Smith na kina Tom Hanks waigizaji wakubwa wakipewa movie kama hizo na kwa kweli utanshangaa utadhani ni kweli kama huwajui katika real life yao basi unaweza kudhani ni kweli mashog. unfortunatelly sishawishiki hata kidog kuangalia sinema za kibongo ni bado sana na hawako tayari kukosolewa once mtu akifanya hivyo anaonekana hater lol jamnai hatufiki hata kidogo, mtu badala ya kuact anauza sura kila tendo anataka aiface camera. scrip hakuna watu wanaropoka inaudhi kupitiliza.hakuna wardrobe yule dada wa big brother sijui Elizabeth kavaa nguo siku amekuwa nominated kutoka lol tena naiona the same outfit ameact nayo movie jamani wakakti mtu alionekana na africa nzima kweli tunacheza makida makida.

Anonymous said...

Tabia yao ya kujichubua Usoni ndio inayotufanya tuwaone mashoga kabla hata hawajaigiza. Sasa akiigiza Mwake si ndivyo aonekanavyo.

Unajua Zama wasanii wa Bongo wana matatizo sana kwanza hutumia majina Bandia zaidi kuliko yao Sina maana Tino ila nina maana (The Great, The Greatest ,Sugu ,Chokolaa!) hii nini maana yake.
Mwache aigize....Kizito