Tuesday, June 8, 2010

NILIYOYASHUHUDIA KWENYE MECHI YA BRAZIL na TAIFA STARS

Katika hali ya kawaida Mechi kati ya Brazil na Taifa stars ni kitu kikubwa sana, na hiyo yote inatokana na ukubwa wa timu yenyewe.
Kutokana na ukubwa wa timu Magoli matano tuliyofungwa inaweza ikawa sio habari pia kwasababu ni kitu ambacho kilikuwa kinategemewa kutokana na ukubwa na uzoefu wa timu yenyewe tuliokuwa tukicheza nayo.
Lakini kuna matukio mengi ambayo yalitokea jana na ndio hayo yanayoweza kuwa habari kwenye mechi ya jana

La kwanza ni yule kijana wa kitanzania alieruka Fence na kuvamia uwanjani kabisa wakati mpira ukiendelea na moja kwa moja kwenda kumkumbatia mchezaji wa Brazil KAKA ambae nae alimpa ushirikiano wa kutosha tu kwenye hilo(HUKU MPIRA UKIENDELEA) na baada ya hapo akatoka uwanjani akiwa na Furaha ya ajabu ila wazee wa kazi wakamtight lakini lengo lake likiwa limeshatimia. Ni kitu ambacho hakijawahi kutokea!!

Tukio lingine ni lile lililomhusisha mchezaji wa Taifa stars JERRY TEGETE pamoja na mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil (Defensive midfielder) GILBERTO SILVA.Mara nyingi wachezaji wanapomaliza mchezo huwa na kawaida ya kubadilishana jezi na hata kwenye mchezo wa jana pia ilikuwa hivyo ambapo baada ya mchezo SILVA na TEGETE walionekana kubadilishana jezi lakini kilichotokea ni kwamba baada ya TEGETE kupokea jezi ya mchezaji huyo wa Brazil na yeye akavua yake ili amkabidhi mchezaji huyo wa Brazil ila katika hali isiyotegemewa na wengi GILBERTO SILVA ALIIKATAA jezi ya Tegete na kuondoka huku akiwa amemuachia jezi yake, kitendo ambacho kila mtu alieshuhudia alikitafsiri katika hali yake.

Wakati wimbo wa taifa wa Brazil unaendelea kuna sauti nyingine zilikuwa zinasikika kupitia Spika zilezile za pale uwanjani na kusababisha muingiliano wa vitu hivyo.

Wimbo wa taifa wa TANZANIA mara ya kwanza ulikuwa ukikatika katika na kusababishwa urudiwe tena kwa mara ya pili ambapo ndio ulikubali kucheza vizuri.

WEWE UMEONA NINI KWENYE MECHI HIYO???

1 comment:

Anonymous said...

wakati timu zote 2 zinaingia kila timu iliingia na watoto wadogo nadhani wale ni chini ya miaka 10...sasa kuna kitoto kimoja kilikuwa kimeshikwa na wachezaji wa brazil wakati rais anapita kusalimiana nao ALIKUWA ANAMSUMBUA AU KUCHEZA NA SANA YAANI ALIFANAY UTUNDU WA AJAB KWA YULE MCHEZAJI WA BRAZIL...picha zaidi nenda kwa michuzi.


Uwanja haukujaaa hilo nalo pia neno.