Wednesday, June 16, 2010

KIFO CHA MPAKANJIA KIMEBADILISHA MAISHA YANGU - JB


Anaitwa JACOB STEVEN ama JB, ameshafanya filamu nyingi sana nyuma kama SWAHIBA, MAHABUBA, WAKTI, MY FIANCE na yinginezo nyingi sana, ni mmoja kati ya watu wanaouvaa uhusika hasa wakiwa kwenye set, ukiniuliza binafsi filamu ninayoipenda sana zaidi kati ya zile zote alizoact nitakutajia Swahiba.

JB ni mtu mwenye Mke mmoja anaempenda sana, kwenye swala la mtoto bado hawajafanikiwa lakini mwenyewe anasema yeye ni mmoja kati ya watu wanaoishi katika ndoa zenye furaha kuliko kawaida (HAPPY MARRIAGE) na anaenjoy sana maisha yake ya ndoa.

Ukiangalia sehemu nyingi anazoigiza huwa kama mtu serious na mwenye misimamo sana lakini nje ya filamu JB ni nani??

Shuka chini ufahamu vizuri zaidi kuhusu yeye.


QN: JACOB STEVEN NI NANI NJE YA FILAMU?
ANS: Jacob Steven nje ya filamu kwanza ni MLOKOLE HUNDRED PERCENT, ni muumini wa kanisa la Mikocheni B assemblies of GOD tena muumini mzuri kwelikweli na ni mzee wa kanisa, Pili mke wangu ni Mlokole kama mimi, Tatu ni msanii NINAEPENDWA NA WASANII WENZANGU KULIKO MSANII YOYOTE am proud to say this na kama unataka kuamini fanya uchunguzi piga kura uliza wasanii ni msanii gani mnaempenda wengi watakwambia ni JB wasanii woote wakike nawachukulia upendo kama wa baba na mtoto mimi niko tofauti na wale wanaowatolea macho na kuwavua nguo, na wasanii wa kiume wote nawachukulia kama wadogo zangu na wote hao wananipenda sana sababu niko tofauti sana na wenzangu nafkiri ni Kristo Yesu aliyeko ndani yangu ndio sababu kubwa.


QN: NINI AMBACHO UNAPENDA SANA??
ANS: napenda sana kuangalia Movies siwezi kulala bila kuangalia Movies hasa movie za nje.. Napenda sana Movies.


QN: NI MSHABIKI WA TIMU GANI HAPA TANZANIA!?
ANS: Mimi ni mshabiki sana wa timu ya Ashanti united watoto wa Ilala, wakati nasoma zamani nilikuwa nacheza mpira sana nilikuwa nacheza na kina kama unamkumbuka Golikipa wa zamani Joseph fungo pamoja na Joseph Katuba nilicheza nao enzi hizo Mwananyamala kule Mtukula.. lakini Jeshini kule kwa wale waliopitiaJKT Mgambo kwa mujibu wa Sheria baada ya kumaliza Form six nilikuwa nacheze mpira sana nilichezea timu ya kikosi, na sasahivi ni kwasababu tu ya umbo lakini kama hivi tunavyokosa wafungaji wazuri natamani nipungue kidogo kidogo na nicheze kwasababu nina uwezo wa kukimbia na kupiga mashuti uwezo ambao mafoward wengi hawana.


QN: MTU GANI MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO??
ANS: Mama yangu mzazi anaitwa MARGARETH MBURA pamoja na Mke wangu QUEEN IRENE lakini hao wote hawamshindi Yesu kristo.


QN: MTU WAKO WA KARIBU NI NANI??
ANS: Zamani alikuwa ni MOHAMMED OTHMAN HERRY MPAKANJIA ambae ameshafariki lakini ukiacha huyo ambae nimemsema sasahivi watu watatu wametokea kuwa watu wangu wa karibu sana, wa kwanza ni mdogo wangu anaenifuatia anaitwa Emily steven Mbura, na wengine ni Madirector wangu wawili ambao ni Adam Kuambiana na Issa Mussa (Claude).


QN: UNAKUMBUKA NINI KWA MPAKANJIA??
ANS: nakumbuka mwaka 2000 yeye ndio alikuwa wa kwanza kuniambia JB hebu jaribu kutengeneza Movie zako mwenyewe, nakumbuka movie yangu ya kwanza ilikuwa kanisa la leo nilitengeneza enzi hizo zamani kipindi hiko gharama za utengenezaji zilikuwa chini sana nikafanya share na mjomba fujo fiamu iligharimu karibu milioni tatu, na mimi MILIONI MOJA NA LAKI TANO nilikuwa sina lakini MOHAMMED MPAKANJIA ALINIPATIA MILIONI MOJA NA LAKI TANO CASH BURE KABISA hiyo siwezi kusahau na kutoka hapo tu ndio nikaanza kufanya production zangu mwenyewe.


QN: KUONDOKA KWA MPAKANJIA KUMEATHIRI VIPI MAISHA YAKO?
ANS: Alikuwa akiwa na kitu kimembana sana mtu wa kwanza kuniambia ni mimi halikadhalika na mimi pia nilikuwa nikipatwa na kitu aidha cha furaha ama cha huzuni mtu wa kwanza kumwambia ni yeye, yeye alikuwa ni Mshauri wangu na yeye alikuwa ni Msiri wangu, MIMI NILIKUWA NIKIJUA CHOCHOTE CHA KWAKE NA HATA YEYE ALIKUWA AKIJUA CHOCHOTE CHANGU.

Kinachonifanya nimkumbuke zaidi kila baada ya kazi ilikuwa lazima tutafutane kilasiku kuachana kwetu ni mpaka kila mtu anapoenda kwake hiyo naimiss kwasababu ikifika muda kama ule namkumbuka sana sana na inaniwia vigumu kwasababu naimagine sasahivi tungekuwa sehemu fulani tunafanya hivi na vitu vingine kama hivyo. nimejaribu kupata marafiki lakini HATUJAWEZA KUWA CLOSE KAMA NILIVYOWAHI KUWA NA MPAKANJIA na hata nyuma kabla yake sikuwahi kuwa karibu na mtu kama nilivyokuwa na Mpakanjia, namkumbuka sana sana.


QN: ROLE MODEL WAKO NI NANI?
ANS: Role Models wangu ni wawili wa kwanza ni AMITAH BACHAN nampenda sana sana na mwingine ni RICHARD GERE na nimempenda sana kupitia filamu yake ya Unfaithful na Pretty woman. huwa siwezi kulala bila kuangalia filamu za hawa watu.


QN: UNAPENDA CHAKULA GANI?
ANS: Mi napenda sana SAMAKI NA KUKU zikitengenezwa na Wali na maharage. napenda mno lakini zaidi kuku.


QN: MAFANIKIO GANI AMBAYO UNAYO?
ANS: Wakati naanza Kampuni ilikuwa na Capital ya Milioni TATU tu kwenye Account lakini nimeweza kupigana kutoka Milioni tatu mpaka MILIONI HAMSINI benki.. hivyo hiko ni moja kati ya mafanikio mengi niliyoyapata kupitia filamu.

4 comments:

Anonymous said...

Zamaradi....kwenye hili
......MLOKOLE HUNDRED PERCENT....yeye ndie alisema? hebu mpe hongera zangu

Anonymous said...

Duh,,huyu bwana nimependezwa saaaana kusikia anvyompenda Mungu,,na kweli anavyoigiza inaonekana ni mlokole.Mpende Yesu zaidi utafanikiwa kuzidi hata hiyo 50elfu,,lakini wewe ni tajili kabisa hongera kwasababu hata wazili wa kwanza Pinda alisema hana hela yahivo benki.Mungu yupamoja nawewe.Big up JB

Anonymous said...

ZAMA,,,, BIG UP!!!! THIS IS A GOOD START FOR JACOB STEVEN (JB)LOOKING FOWARD TO SEE OUR CELEB PERSONAL LIFES IN N OUTSIDE OF THEIR CARIER

Anonymous said...

JAMANI MIMI KWA KWELI JB NAMZIMIKA KWA UIGIZAJI WAKE NILIPENDA SANA ALIPOIGIZA KATIKA FILAMU YA BORN AGAIN HAKIKA ANAJUA KUUVAA UHALISIA HASA HASA, KAKA JB MUNGU AZIDI KUKUINUA ZAIDI NA ZAIDI NA UENDELEE KUMSHIKA KWA NGUVU ZAKO ZOTE USIMUACHE MAANA NDIYE CHANZO CHA MAFANIKIO YAKO ZAIDI NA ZAIDI
marthawilly@yahoo.com