Monday, February 22, 2010

MDADA ALIEFUNIKA 2009 KATIKA BONGO MOVIES


Aunt Ezekiel Kulia akiwa na Maimatha wa jesse


Katika MOVIE LEO kupitia kipindi cha Leo tena hapa clouds FM tulishindanisha wanadada wanaofanya filamu hapa bongo ili tuweze kumpata msichana aliefanya vizuri kwa mwaka 2009/2010. Kura ziliweza kukusanywa kupitia njia tofautitofauti kama maoni ya watu wa nje, SMS, pamoja na kuongea na Madirectors, maproducers na watu walioko kwenye tasnia hii ya Filamu. lakini njia kubwa kabisa ilikuwa ni MAONI ya watazamaji wa hizo Filamu na hatimae AUNT EZEKIEL GREYSON akaibuka kuwa Mshindi kwa kuwapiku wasichana wenzie wote wa tasnia yake.

Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta Challenge na kuangalia nani kafanya nini kwa mwaka 2009 ambao ndio tumetoka kuumaliza, hatujui mwaka 2010 nani 'atashine' .

Filamu ya kwanza kabisa iliyomtambulisha katika Tasnia hii ilikuwa ni MISS BONGO ambayo ilikuwa directed na William Mtitu..

Baada ya hapo akaja kuonekana na kushine kwenye filamu nyingine nyingi tofauti, Baadhi ya Filamu ambazo ameshawahi kuzifanya ni pamoja na TASTE OF LOVE ambayo ilielezea maisha yake halisi, WICKED LOVE, HOSTEL na nyinginezo nyingi.

Kama Mdau wa Filamu namtakia kila la Kheri mwanadada katika kazi yake ya Filamu.

2 comments:

Anonymous said...

Baaab'kubwa hii mambo zamaradi yani itakuwa si mchezo..

Frank Dar!

Anonymous said...

Hivyo vigezo ulivyovitumia, havitumiki hata siku moja kumtafuta muigizaji bora. Au unatafuta muigizaji maarufu?