Wednesday, February 24, 2010

JICHO LA TATU - TUTAFIKA KWELI?

Katika Entertainment Industry hapa Tanzania kuna fani tofautitofauti, lakini zile ambazo zinaonekana ziko juu zaidi na zinachukua attention ya watu wengi ni MUZIKI, MITINDO na FILAMU.

Nikianza kuzungumzia Industry ya Filamu ni kitu ambacho kimekua juu ghafla tu miaka ya hivi karibuni, tofauti na Muziki ambayo ni Tasnia kongwe zaidi, Na Industry ya Filamu imeshatoa watu wengi sana ambao mpaka sasa ni MA-STAR WAKUBWA MNO hapa Tanzania na wanaendelea kufanya vizuri.

Kuna Usemi Usemao HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA ambapo maranyingi huwa tunatumia msemo huu kujifariji na kujipa moyo pale ambapo tunaona mambo yanaenda ‘Slow’ ama tofauti na matarajio yetu. Lakini tukumbuke vilevile kwamba NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI na DALILI YA MVUA NI MAWINGU, kwa upande wa wasanii wa Filamu wanaonesha hakuna kabisa dalili ya mabadiliko kati yao, wanaridhika haraka na kusahau walipotoka. Ili kuweza kufanikiwa katika vitu tunavyovifanya siku zote ni Vizuri kuangalia ‘NEGATIVES’ zetu zaidi kuliko ‘POSITIVES’ sababu kwa kuangalia mabaya na udhaifu wetu itatusaidia kuendelea mbele zaidi kwa kurekebisha tunapokosea kuliko mazuri yanayotufanya tubweteke na kuamini kwamba kilakitu kiko sawa wakati huenda ikawa tofauti.

Ili fani zote hizo ziweze kuendelea mbele kuna kitu kimoja kikubwa kinachohitajika sikuzote ambacho ni MEDIA kwa maana ya Vyombo vya habari kama Television, Radio, Magazeti, Mitandao n.k. Kupitia Vyombo vya habari watu ndio wanatambua uwepo wa watu ama kazi Fulani.
Business without advertising ni kama kumkonyeza mtu gizani. Hata kitu chako kiwe kizuri namna gani lakini kama watu hawakifahamu hakitakuwa na faida yoyote, It’s useless. Hivyo kazi kubwa ya Media ni kuripoti habari na mambo mbalimbali yahusuyo tasnia tofautitofauti ikiwemo na wahusika wenyewe.

Ikumbukwe kwamba si kuripotiwa kwa MAZURI TU MNAYOYAFANYA bali hata pale MNAPOKOSEA media haitakuwa nyuma kwa hilo. Na hio ni kwasababu tu unapokuwa mtu maarufu wewe ni kioo cha jamii na kama kioo cha jamii watu watataka kujua mengi sana kuhusu wewe sababu kuna wanaotamani pia siku moja wawe kama wewe. Hivyo kama umeamua kuwa Star sahau kuhusu PRIVACY.

Lakini kwa upande wa baadhi ya wasanii wa filamu ambao wao ndio wangeweza kuwa muongozo kwa wenzao hali inasikitisha kidogo, Inaonekana kabisa kwamba wanasahau walipotoka, Wanasahau kwamba VYOMBO VYA HABARI ndio vimewafikisha hapo walipo, wanasahau pia kwamba wao ni vioo vya jamii hivyo kila wanalolifanya jamii inataka kujua nini kinaendelea katika maisha yao.

Ombi langu tu kwa yeyote anaehusika msiifanye hii fani ikaonekana kama ni ya watu waliokosa muelekeo wa maisha wakaona njia pekee ni kukimbilia huku hapana. Baadhi yenu Reaction zenu zinaonesha udogo wa IQ zenu na hiyo inatukanisha moja kwa moja tasnia yetu hii nzima ya Filamu tukichukua kauli ya Samaki mmoja akioza ni wote wakati kuna wengi ambao wanajua nini wanakifanya. Kwenye hiyo ni kama inawaharibia. Filamu ni Ulimbukeni na Ujuaji mtupu uliojaa huku.

Hebu jiulizeni kuna Mastar wangapi wakubwa hapa Tanzania wame-struggle mpaka kufikia walipofika si kijina tu bali hata Kiuwezo na bado wanaheshima na kuheshimika katika jamii, hawajisahau. Mfano mzuri ni lady Jaydee ambae ni mwanamuziki, This is a real Diva na mfano mzuri wa kuigwa na watu wa tasnia zote kwa sasa, mafanikio yake yanaonekana waziwazi na hiyo ni kutokana na msingi mzuri aliojiwekea , lakini mbona hana majigambo na hizo Showing off za kienyeji!!! I RESPECT THIS WOMAN. Sidhani kama angekuwa na hizo mbwembwe mlizonazo angefika hapo alipo.
Mnachotakiwa kujua ni NO ONE IS PERFECT, kila mtu hukosea si wewe wala mimi, hata wakubwa wa nchi hukosea pia maranyingine na ndiomana kukawekwa washauri, Ubinadamu ulizingatiwa.

Sasa wewe unapokosolewa DON’T TAKE IT PERSONAL sababu hakuna mwenye Chuki na wewe, lengo ni kujenga na si kubomoa, WEWE NI NANI mpaka upambwe kila siku!? Mbona mnapenda SIFA tena zile za kijinga?? Badilikeni jamani ni aibu, nafikiri mngekuwa mnajua mastar wenzenu wa ulaya wanaishi vipi sidhani kama mngelalamika eti kwa KUKOSOLEWA FILAMU.

Lack of exposure ndio tatizo kubwa linalowakibili wengi wenu, Exposure ni kitu kizuri sana jamani, tusiishie NIGERIA tu, hebu tujaribu kuangalia mbali zaidi, siku zote siri ya mafanikio ni kuangalia wenzenu walioendelea kwenye kitu Fulani wanafanya nini juu ya jambo husika, Hakuna ubaya kuiga kitu kizuri. Tanzania ukishapita mitaa miwili mitatu watu wanakugeuzia shingo na kukuita jina basi unaona umeshamaliza kila kitu na unaridhika kabisa.

Kwa wenzetu mastar wakubwa kila wanachokifanya ni habari na wanaelewa kwamba ile ndio Price of being a superstar, sasa nyinyi kuongelewa filamu tena mara nyingine hata hujaskiliza wewe umefanya tu kuletewa tu habari “INDIRECT SPEECH” ambayo maranyingi kama sio zote haifiki kama ilivyokuwa ndio mnajipanikisha hivyo na mishipa inawasimama. Tutafika kweli?

Kiukweli mnasikitisha sana na mko kwenye hali mbaya mno bila nyinyi wenyewe kujijua. Acha wanaoendelea kuwasifia ujinga wawasifie na endeleeni kujazana ujinga ila mkikutana na WENZENU wa nchi nyingine ndio mtajiona MKO NYUMA kiasi gani, mara nyingi huwa tunapwaya.
Kibongobongo mtapeta lakini kama lengo ni kufika Hollywood kama mnavyokuwa mnajibu kwenye interview zenu kwa hali hiyo ya kutotaka mabadiliko MNAJIDANGANYA.

Mwenye masikio na asikie mwenye macho na aone, ni mawazo yangu tu si lazima ukubaliane nayo na hayahusiani na mtu yoyote.

Asante
Zamaradi Mketema.

15 comments:

Anonymous said...

Ni kweli inabidi watembee na wasome sana kujua mengi ya ulimwenguni katika kazi zao.

disminder

Anonymous said...

Me nishajua Zamaradi huu ujumbe unawagusa kina nani but anyways kazi nzuri,napenda ulichokisema bila uoga wala aibu kuwa fulani atasema au atanichukia.Ila me naomba niulize kuna kitu flani kuhusu movie za bongo nataka nikuandikie ukipost kama utaona kinafaa au ukizungumzie how can I do that?!
Yusuph

Anonymous said...

Zamaradi; hongera kwa kujaribu kuweka wazi masuala yanayokwamisha maendeleo ya sanaa ya filamu nyumbani. Kuna masuala mengi ya kuongelea na yatakayoendelea kujadiliwa. Cha msingi wahusika wanapaswa kujua kwamba sanaa ya filamu Tanzania bado ipo nyuma sana, ten asana! Wanayoyaona kuwa ni mafanikio kama vile kuwa na simu kali, pamba za China, usafiri na say (kwa waliofanikiwa) kuwa na nyumba ya kuishi si mafanikio, ni vitu vya kawaida sana!! Kucheza filamu nyingi hakumaanishi kwamba kazi zako zinapendwa au umefanikiwa, mafanikio ni ubora wa kazi kila mara unapotoa kazi mpya na kudumu kwenye fani!! Mimi siyo shabiki wa movies za kibongo sana, lakini kwa chache nilizofuatilia naona tumeshindwa kuwa wabunifu, tunaiga kuliko kawaida na maudhui ya kazi zetu mara nyingi ni yale yale!! Wasanii wetu wanapaswa kukumbuka kwamba filamu ina malengo mengi..kuelimisha jamii, kufurahisha (kuburudisha), kukosoa, kuliwaza na pia ni chanzo cha kipato! Unapofanya kazi yako halafu haielewi au haifikishi hayo unakuwa hujafanya kitu!
Pamoja na suala la kutangaza kazi (advertisement) mimi nimegundua kazi zetu zinaibuka ghafla mno, hawafanyi utafiti wa kutosha kabla ya kutoa filamu, wanadhani mafanikio ni kutoa filamu nyingi, wanasahau ubora wa kazi yenyewe. Ndiyo maana filamu zetu nyingi zinakuwa kama mchezo wa kuigiza tu, naamini huwezi kutunga kazi na kurekodi ndani ya miezi mitatu au sita ikawa sokoni…msanii gain huyo anaweza kutoa filamu kila baada ya miezi sita? Hiyo ni filamu au ngonjera?? Mimi naawashauri wadogo zetu kwanza wenyewe wawe washabiki wakubwa wa filamu, waone wenzao wanafanyaje kazi zao! Pili siku hizi vyuo vinavyotoa elimu ya masuala ya habari na filamu vipi vingi, wajiendeleze huko kupata elimu na ujuzi zaidi. Tatu, wasanii wetu badala ya kukaa vijiweni au kutanua mitaani wajitahidi kutumia muda wao wa ziada kupitia mitandao ya internet nk kujua nini wenzao wa nje wanafanya ili wajifunze pia, wajenge network na wasanii wa nje ili wapate somo huko pia. Jambo jingine ni vema mtu ukajikita katika aina mojawapo ya filamu…kama ni vichekesho, filamu za mapenzi etc…hii itakusaidia kuwa consistent zaidi kwenye kazi zako, ukishabobea huko then ndiyo unaweza kuongeza ujuzi katika eneo jingine la filamu!
Kuhusu suala la wenzetu kujisikia “wamefika” au wameshakuwa “mastaa” mimi naona hilo ni tatizo sugu sana bongo! Si kwa wasanii wa filamu tu, hata wanmuziki (kizazi kipya), wanahabari (hasa Redio na TV), walimbwende pamoja na wanasoka. Hili ni tatzio sugu na linaturudisha sana nyuma! Unamkuta msanii ameshajiona yeye ndiyo Denzil Washngton etc, tunaishi ki-magharibi kuliko hata magharibi yenyewe ilivyo!! Hiyo ni kazi yako, iheshimu sana na waheshimu sana wapenzi wanokupa sapoti siku zote, unapojiona wewe bab’kubwa kisa ni mcheza senema wa bongo au mwanamuziki wa kizazi kipya…au sijui kwa kuwa unaonekana kwenye luninga unakuwa unajirudisha sana nyuma jamani, kwa sisi wengine kwa ujumla tunawadharau sana!!
Mimi nawapongeza sana wasanii wanoheshimu kazi zao na ambao kwakweli wamepiga hatua. Jaydee anafanya mambo makubwa na yupo kwenye fani muda mrefu sasa, anastahili pongezi!! Ukiangalia umati wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanofurika kuona machozi band kila week unajiuliza hivi ingekuwaje kama kati yao wangefanya vitu kama vya Jide??
Sanaa ni kazi kama kazi nyingine, ni maendeleo yao!! Hakuna jingine zaidi ya kuheshimu kazi, kujiheshimu wenyewe na kuwasikiliza mashabiki wako! Ukizingatia hayo mafanikio yatakuwepo! Mafanikio yatakuja lakini kwa sasa tusijione kuwa tumefika.

Semesozi, Puli-e-Khumri City

TITO said...

daah sista kweli kabisa wasanii wa filamu wamezidi maringo ila mi naona tatizo xul ndogo unajua wasanii we2 hawajui kwamba kila ki2 ili ufanye vizuri lazima uwe na shule lilngine hao wasanii kweli wapo ambao wanajua nini wanachofanya ila wanapotoshwa na wauza sura halafu kingine eti dada hivi kuna lazima m2 akitoka kwenye let say TUSKER PROJECT FAME or BIG BROTHER awe msanii wa movie to be honest i dnt think so coz most of them HAWAWEZI kucheaza filamu so i advice them wawe serious na kazi watafanikiwa ni hayo tu its me TITO TITORICH58@YAHOO.COM

Anonymous said...

vizuri sana unajaribu kuwafunua macho kama unavyosema hakuna EXPOSURE,kama wanavyosema kwamba msanii ni kioo cha jamii,sasa inakuwaje hawa wasanii wetu story zao zinalenga sana mapenzi,magari ya kifahari,majumba ya kifahari na lazima kuwepo na duka la nguo baada ya hapo dinner,hii inafunza nini watanzania wengi ambao ni maskini hakuna story nyingine ambazo zinaigusa zaidi jamii yetu ili ipate kuelimika kutokana na hali halisi ya hapa,kuna mambo mengi tu yanayoendelea kwenye mitaa yetu na kizuri hata hao wasanii wametokea huko sijui nani kati ya hao katokea kwenye silverspoon(maisha ya kifahari)si kosoi lakini nataka maendeleo kwenye film indurstry na fani zote na hata hapo walipofika wamejitahidi na nataka siku 1 mbongo achukue oscar.NGOGOMO

Anonymous said...

Hongera sana binti kwa maneno ya ukomavu na busara uliyoyaandika kuhusu wasanii wetu, hasa hawa wa Filamu. Ni imani yangu kuwa kama wanaustaarabu wa kupitia mitandao watasoma kile ulichokiandika.
Kuna kitu naomba kujua kutoka kwako,kuna bi dada mmoja alipoolewa alikuwa anataja majina matatu kujitambulisha kwa watu katika vipindi anavyoviendesha lakini kwa sasa amepunguza majina na kutumia yale aliyokuwa anatumia kabla ya kuolewa, je ameachika? maana hata pete havai siku sizi. Unataka kujua ni nani,anaitwa Joyce Kiria.

Anonymous said...

mmh article nzuri ila ndefu jamani mpaka unaluz concentration..

gud work zammy

margy jo

Anonymous said...

yani thank U Zama,mana am tired of this so "called" movie actors na actresses jaman ni aibu mimi mpaka naona aibu sometymz yani watu wanajifanya wanajua kuliko mpka wanaharibu.these people don't know how to act like real stars jaman kwa wenzetu uko mbele a celebrity ndio kioo cha jamii na maisha yake yanafuatiliwa na the media reports everything whether good or bad. aliripotiwaw Clinton na his cheating affairs plus tiger woods sasa hawa wenzetu hawataki kukosolewa who are they anyways???? u've fixed them in a right position Zamaradi and don't u be afraid coz ndio unawanyoosha..plus anaekasirika it means they av a certain weakness and they know it except they don't wanna change au ndo to my opinion they just don't have the talent to do so...well kip up the good work! and i love ur looks very beautiful and natural..take care

UR Fan

Anonymous said...

Naomba kuuliiza katika mashindano yenu ya so called best actor, best actress mbona sijaona mkiuliza best movie ya Tz for the year 2009/10.

I am not particularly interested in the movie production but more on the stories. Most stories are crap...ila lets give a big hand to a few smart ideas.

Anonymous

Anonymous said...

Zamaradi Big up mama
I really likes you so very much Kwa kweli sina la kuongeza mii ni mpenzi sana wa movie na nimesomea japan. Ninachokiona hapa ni maigizio na ulimbukeni wa waigizaji wetu kama ray , kanumba, magali, sheni and the like from Kaole sanaa.
Zamaradi hakuna movie hapa ni fujo, makelele na crapy things Iam writing a feature article will send to you mama

Anonymous said...

Kitu ambacho umenifurahisha zamaradi ni "uthubutu" yani umeongea bila kupindisha maneno that's gud zamaradi big up, back to the mada kama ulivosema lack of exposure hili tu hakuna lingine kwa sbb niliona yule the so called the great alivolia na media hasa blog alivokosolewa kwenye kiinglish. instead kutake as a challenge yeye akaanza kulialia na kutafuta sympath as if kaonewa.

Anonymous said...

Hongera Zamaradi kwa kuwaelimisha sana sana hao wanaojiita movie star.. Tanzania bado hatuna Movies na maanisha tasnia ya Filamu bongo bado haipo hao akina Ray,Kanumba bado ni waagizaji tuu kama walivyokuwa kule Kaole tofauti hapa ni kwamba wamejitenga kidogo na kuwa na vijikundi vya ubabaishiji...Bado wanaigiiza kama wanataka mafanikio Wakubali kukosolewa labda siku moja watajifunza na siku moja tukawa na movie stars. Kwanza waache kuigiza Nigerian Movies wanatuibia wananchi etii Kanumba jina la movie yake "This is It" tangu lini? Yeye ni Wacko Jacko? Aise waende shule kwanza...

Zeddie said...

hahahahah Zamaradi hongera my dear uko vizuri na penye ukweli uwongo hauna nafasi. natumai ujumbe umewafikia walengwa hata sisi tusio mastar ujumbe umetugusa

Big up Zamaradi

Anonymous said...

You are absolutely ok Zamaradi! Keep it up! Mwenye masikio na asikie maneno haya!