Thursday, January 6, 2011

SIJAWAHI KUVUTA UNGA ila BANGI..........- TWENTY PERCENT (20%)

Katika mahojiano niliyofanya na TWENTY PERCENT AMEKIRI kwamba yeye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa BHANGI enzi hizo ingawa kwasasa AMEACHA na hatumii tena mmea huo haramu..
lakini kuna swala lingine ambalo watu wengi walikuwa wakilisema kwamba anatumia madawa ya kulevya (UNGA)..Alipoulizwa Twenty AMEKANA na kukataa katakata swala hilo la utumiaji wa madawa hayo na amesema hakuwahi hata KUJARIBU kitu kama hiko

Katika mahojiano hayo Twenty amekiri kwamba amewahi kuishi maisha ya Ghetto kabisa na ameweza kushuhudia watu wake karibu aliokuwa akiishi nao pamoja wakichomwa moto, kukamatwa kutokana na wizi, kuvuta unga na uchafu mwingine lakini yeye kama yeye hakutaka kujihusisha kwenye njia hiyo pamoja na kukaa nao pamoja ila alichoamua kufanya ni Kufocus kwenye Muziki kwa kuamini kuwa hiyo ndio njia pekee ambayo ingemtoa....


Kwasasa twenty anatamba na nyimbo zake kama TAMAA MBAYA, YA NINI MALUMBANO na nyinginezo nyingi ingawa amekiri katika nyimbo zote alizoimba WIMBO ambao unagusa maisha yake moja kwa moja ni Wimbo wa MAISHA YA BONGO ambapo vingi vinavyoonekana na kuimbwa kwenye huo wimbo ni aina ya maisha aliyopitia..


Mbali na Muziki pia kwasasa TWENTY anatamba na FILAMU yake inayofahamika kwa jina la 20% - FURAHA IKO WAPI ambapo kwa upande wangu ndani ya 2010 hiyo ndio THE BEST FILM though kuna kasoro fulani fulani kwenye upande wa quality lakini Kistory na Script IT IS THE BEST.. trust me!!!!


3 comments:

Anonymous said...

namkubali 20 nyimbo zake full ujumbe, pia movies; he can act! Nimeckia he is the most highly paid actor bongo.

BIG UP!!!!

Anonymous said...

Nampenda sana huyu kijana na hasa nyimbo zake ndizo zinazonifanya nimpende, Filamu yake ndio kabisa kwani wimbo wa mwisho wa Mama Neema aliutoa wakati ambapo Mimi mwenyewe nilifikwa na msiba wa mchumbwa wangu na kuniachia mtoto mdogo.

Kibao hicho huwa kinanifanya nifikirie mengi kana kwamba aliona kinachoendelea na kunifika ndipo akatunga wimbo.

Namtakia kila la kheri katika maisha yake ya muziki na filamu.

Tupo Pamoja.

Anonymous said...

jamani namkubali sana huyu kijana nyimbo zake ni nzuri mno! movie yake siishi kuiangalia mara kwa mara.keep it up man