Friday, January 21, 2011

FILAMU YA USHOGA YA TINO IKO TAYARI...

Hiyo ndio COVER ya filamu ya TINO inayoitwa SHOGA ambayo ameigiza kama SHOGA, kama unavyoiona hapo juu, ameonesha kama sura mbili ambapo upande mmoja ni taswira ya msichana na upande mwingine ni sura ya kiume ambayo ni yake mwenyewe TINO.. Na filamu hii itazinduliwa rasmi siku ya tarehe 4 mwezi FEBRUARI pale TRAVERTINE HOTEL na baada ya hapo wakazi wa MWANZA kaeni mkao wa kula....
Hissan Muya (TINO) akiwa katika sura yake ya kawaida..
Kwa wale wote waliokuwa na maswali juu ya filamu hiyo , majibu yote yatapatikana siku ya Uzinduzi wa FILAMU hiyo na kwa habari zaidi kuhusu TINO, nini anafanya na kuhusu Filamu yake hiyo.. USIKOSE kuangalia TAKE ONE siku ya JUMANNE saa TATU kamili USIKU palepale CLOUDS TV!!!

NIPE MAONI YAKO.. UNAIONAJE COVER YAKE (ya kwanza kabisa)!!!!?????

14 comments:

Anonymous said...

Kwanza napenda kuwaasa watz wasimwelwe vibata Tino couz ktk hii filam hayuko tofauti na jot anayeigiza kama Bi Kiboga so nisanaa tu juu ya kuelimisha jamii! ntajitahidi niipate couz mi ni mpenzi sana wa Filam za kitz! Big up tino cave lake liko poa sana!

Anonymous said...

Hili si jambo jema kwa Taifa.naomba wizara inayohusika kuipiga marufuku filamu hii kama Uganda anafungwa huyu.msituletee mambo ya wazungu.kama yeye ni shoga asiwafundishe watoto wetu.

Anonymous said...

natumaini maigizo ya humu hayatapelekea kuhamasisha ushoga.. maana wana jamii hasa vijana huwa wanaiga haraka sana maigizo ya celebrities..

Anonymous said...

Cover iko pouwa...nimependa walivyoitengeneza nadhani kuna msg wanatakata kufikisha thru this cover.I think ts about matendo ya kishoga,athari zake na namna ya kuyadestroy...na ts lyk ushoga anafanya ucku zaidi... na mchana ni mwanaume wa kawaida that is according to me na ndio msg nliyopata nlivyoona cover....

Anonymous said...

Cover iko pouwa...nimependa walivyoitengeneza nadhani kuna msg wanatakata kufikisha thru this cover.I think ts about matendo ya kishoga,athari zake na namna ya kuyadestroy...na ts lyk ushoga anafanya ucku zaidi... na mchana ni mwanaume wa kawaida that is according to me na ndio msg nliyopata nlivyoona cover....

Thom said...

pumbavu sana. sitanunua tena movi ya huyo shoga. shenziiii type

Anonymous said...

Zama mimi binafsi nafkiri hii movie mngeandika under 18yrs ili watoto wanaokuwa wasije wakajaribu kwani watoto kitu kinachokatazwa wao ndio wanataka kujaribu mi nafkiri iwe kwa wakubwa tu waelewa wa mambo otherwise mtaharibu hali ya hela mitaani hasa watoto wetu wanaokuwa thanks.

Anonymous said...

No comment

Anonymous said...

Tusiendeleze tabia za ushoga kwa kisingizio cha uhuru wa wasanii na riwaya ya maisha. Nasikia kuna jamaa alikuwa 'curious' tu akasema atajaribu mara moja tu na shoga mmoja, lakini matokeo yake ni kuwa alinasa katika tabia hiyo kwa miaka mingi. Ila napenda vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 18 waelimishwe kuhusu madhara ya tabia hii kimwili, kijamii na kiroho.

Anonymous said...

Kama tukitaka kuwaiga wazungu tuwaige kwa mazuri wanayoyafanya na yaliyowaletea na yanayowaletea maendeleo ya kiuchumi, kisayansi, kilimo, viwanda, kitamaduni na mazuri mengine. Lakini si ujinga wa kuiga kuvaa surali na kuonyesha chupi au kutumia sumu (madawa ya kulevya).

Anonymous said...

Mimi ningeomba hii movie ifutwe kabisa na nadhani hapa Tanzania hakuna kitengo cha kupitia movie na nyimbo zetu na ndiyo sababu itatoka na wapo wanaoona ni kitu cha kawaida.
Nipo pamoja na waliosema tusiige uzungu kwani hatuwezi kuzuia hata kama tutasema iwe kwa ajili ya zaidi ya umri wa miaka 18.
Na nina hakika siku moja huyo Tino atajuta kwa kuigiza hivyo au la anapenda kuwa shoga.
Vitu vya kuigiza vipo vingi sana na hawataki kuvigusa kwa sababu ya ufinyu wa ubunifu.

Anonymous said...

Wasanii wa Kibongo acheni kuiga uzungu na Unaigeria.
Muwe wabunifu na msiwe wachoyo wa kugawana kazi.
Tino utatuharibia utamaduni wa kitanzania pamoja na kwamba ushoga upo lakini si vyema kuendekeza, mi nadhani kama ulitaka kutoa elimu hapo umechemsha.

Anonymous said...

mwanaume akishapenda kujiremba 2 kuna walakin iweje ajichubue? relaxer ya nn kwa kichwa? mh BIG NO

Anonymous said...

Sio kama joti. Joti anaigiza kama mwanamke kamili sio ushopa