Saturday, January 8, 2011

UKWELI KUHUSU MIMI NA LULU.....

Hii ilikuwa ni siku ya mkesha wa mwaka mpya...

Kuna mtu kupitia FACEBOOK anajiita LULU MICHAEL akijifanya yeye ni ELIZABETH MICHAEL (LULU).. na anachofanya ni kama kuvamia mambo asiyoyajua na kujifanya yeye ni LULU wakati si kweli na kuandika maneno ya ajabu anayoyajua yeye mwenyewe ili kuonesha kama kuna BEEF kati yangu mimi na Lulu which is NOT true.. ninachotaka kuweka wazi ni kwamba huyo SI LULU wa ukweli ila huyo ni mtu anaejifanya LULU ambae ndie aliweka hata zile picha za LULU za UTUPU zilizotengenezwa ambapo alijifanya kama yeye ni LULU wa ukweli na hatimae LULU alitumia kipindi changu kuweka wazi hilo swala kwamba hakuwa yeye... sasa naona this time amekuja na style nyingine.


Kwa habari tu ni kwamba jana tu LULU ametoka kunipigia akionesha kukwazika na kitendo hiko cha huyo mtu kujifanya ni yeye na kuonesha kama kuna BEEF kati yetu wakati hakuna kitu kama hiko na hilo limenifanya niamue kuliongelea ili kuliweka wazi kwa watu ambao hawaelewi kinachoendelea..


Ukweli ni kwamba MIMI na LULU hatuna beef yoyote na wala HATUJAWAHI kuwa na BEEF yoyote, tunaheshimiana sana na ni mdogo wangu ambae tunashirikiana vizuri tu kwenye kazi na mambo mengi ya karibu, hivyo huyo ni MPUMBAVU mmoja tu ambae hana kazi ya kufanya na ana sababu zake binafsi ambazo sizielewi mpaka sasa.


Kiukweli sikutaka kabisa kuliongelea hili lakini kutokana na watu wengi Kuni-INBOX kupitia facebook, kunipigia simu na wengine kuniambia kwa kudhani ni kweli ndio hiko kimenisukuma niliweke hili swala wazi otherwise halikuwahi kunisumbua ni maneno tu ambayo mtu yoyote anaweza kuongea akijiskia kuongea ambayo ni ya kawaida sana kwangu mimi na hayanisumbui akili.... na ndiomana nimekaa kimya muda wote huo lakini kutokana na wengi kutokuelewa ukweli imebidi niliweke wazi..


NINACHOTAKA KUWEKA WAZI LEO kwa watu wengi ambao hawajaelewa ukweli uko wapi ni kwamba MIMI na LULU hatuko kwenye hiyo situation na wala huyo alieandika hivyo SI YEYE ila ni LULU FEKI na LULU mwenyewe kwenye facebook hatumii jina la LULU MICHAEL kama huyo chizi anavyojiita ila anatumia jina la ELIZABETH MICHAEL...


So kwa fans wote na wale wote ambao hawakuelewa kinachoendelea huo ndio Ukweli... YULE alieandika pale kwenye facebook SI LULU.

13 comments:

Don Dollar said...

Nishamsoma huyo jamaa, ila sio issue sema nn hako katoto nako mmh! take care acje akakuchafua na ww, mtoto nuksi huyo ha ha ha

Anonymous said...

kashauri kaka some maana kameanza kuzeeka sasa na umaarufu unapotea

mariam said...

zama mi siko ktk issue ya huyo mtoto sababu ana mambo makubwa machafu hata shetani hayatambui ivo dunia ndio itamfunza bado hajatambua.
issue yangu ni kwamba kuna movie moja hiyo embu itafute hiyo movie ni ya kibongo lkn wanaongea kingereza, kitu nilichonote at first nilikuwa napita naona watoto wanaicheck nikasikia sauti tu nikajua wanacheck movie za kinigeria, then nikarudi kuwaulizia je hiyo ni movie gani ghafla namuona monalisa, babu mmoja hvi anandevu zina mvi na hemed,kiukweli nilistuka sana nikasema je hii movie siyo ya kinigeria mbona nawaona watu ambao ni wabongo? kiukweli niliboreka sana hata kama wanaongea kingereza kwanini waliongea kama manigeria? yaani sauti utadhani ni kina geineviv ama ramsey ama mnigria yoyote ina prononciation siyo ya kibongo kabisa,plz nenda kaicheck sikumbuki jina ksbb niliwaambia waitoe kabisa pale, kama sijakosea "who is smarter" nahisi ndo jina lake plz labda mie ndo nimeielewa vibaya lkn sijaona maana yake ktk kuongea kama wanaigeria

Anonymous said...

Huyo jamaa kwenye facebook anaweza kujulikana. Nenda kwenye kampuni yoyote nzuri ya internet hapa TZ na baada ya kupata ushirikiano wa polisi wanaweza (1) Kujua nchi aliyoko huyo mtu (2)Kwa kushirikiana na service provider yoyote katika hiyo nchi wanaweza kujua 'terminal' yaani kompyuta (kutumia connection ya line ya simu) anayoitumia. Mara nyingi tatizo la mijitu kama hiyo yenye ugonjwa wa kuwaharibia watu majina yao ni kuwa wanapenda kutumia internet cafes wakizuru facebook. Wamejifunza kutokana na Bw ML (wa blogspot ya matusi iliyolaaniwa ya zeutamu) alivyokamatwa. Nakushauri uanze jitihada za kum-"trace" mtu huyo. Namalizia kwa kusema kuwa mtu huyo anayewachafulia jina huenda akawa Mtanzania kwa kuwa tuna WATZ wengi wenye ugonjwa huo. Na kwa kuwa wewe Zamaradi ni mzuri wa sura, tabia na umbo na unaifanya kazi yako vizuri kiasi cha kuwa kuna maelfu ya watu wanaokupenda sana (fans wako), lazima kutakuwa na watu wanaokuonea wivu. Lakini usijali: Mweke Mola mbele na muombe Akulinde. Kila la heri.

Anonymous said...

Nakubaliana na mchangiaji wa nne; TZ ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ugonjwa wa PHD (Pull him/her down syndrome). Yaani, kuna watu wengi ambao wana wivu wa kijinga kiasi cha kwamba wakiona kuwa mtu anafanya vizuri katika fani yake na anapendeza basi wanamwonea wivu na kumchukia bila sababu. Mara nyingi watu kama hao kazi yao ni kuwaharibia watu majina kwa kuwazulia uongo. Lakini kama alivyosema mchangiaji huyo wa nne, ukimweka Muumba wako mbele atakulinda. Chuki za binaadamu hazimpati anayelindwa na Muumba wa ardhi na mbingu na vitu vyote .

Anonymous said...

Kinachonishangaza ni kitu kimoja tu: Je hao watu wenye kwenda kwenye facebook na kutumia majina ambayo si yao hawana kazi ya kufanya? Je hao watu ambao wanatumia internet kutukana watu wengine hawana kitu cha maana cha kufanya? Tutumie mtandao (1) kupata elimu (2) kupashana habari, na (3)kwa burudani. TUSITUMIE MTANADAO KUTUKANANA, KUJENGA CHUKI WALA UBAGUZI WA AINA YOYOTE. Nina hakika watu wanaotumia internet kutukana, kugombanisha na kusambaza chuki wana matatizo ya akili. Mimi mshabiki wa Zama niko Arusha.

Anonymous said...

Zamaradi, rejea maoni ya mchangiaji wa nne. Njia rahisi nyingine ni kuwa-contact facebook na kuwaeleza kuwa kuna 'impostor' anayetumia majina ya watu wengine kugombanisha watu. Kuna watu wamefanya hivyo na facebook imechukua hatua.

Anonymous said...

mimi ni lulu michael feki, zamaradi you can see or meet me if u wish , yes i admit that currently i use someone's pic in my facebook account i.e photo.but soon i will change it. and dat is the only mistake i have done coz names always intersects so by that fact i argue to have use my legitimate name. sorry zamaradi nimekudis kidogo ila tutafix ni chalenges za kawaida. tena nasema ili niweze kuposti comment lazima nitoe valid email adress ninayotumia facebook, kwa hiyo am the fake lulu

Anonymous said...

Hapo hakuna kigezo cha kutumia kusema ametumia Jina la mtu maana ukiangalia Ni kwamba Hicho kijamaa kimetumia jina la LULU MICHAEL na Mwenye Jina anadai kuwa yeye jina lake halisi ni ELIZABETH MICHAEL na LULU ni jina la Uigizaji tu , tena si LULU MICHAEL ni LULU.
Kwahiyo hapo kisheria humfungi mtu.
Tena ngoja niende nikaMuADD huyo bwana ili niweze kufaudu mauhondo

Anonymous said...

Take it easy mana watu kama hao wapo kwa ajili ya kujenga jamii..anasema ili uwe down but u need to move on sister........

Anonymous said...

wengi hawajui matumizi ya mitandao ya kijamii mpaka wanakera watu wengine ila kama waliotangulia kuna mijutu haina la maana la kufanya kazi ni kutaka kuwaangusha watu tu achana nae asikupotezee muda ama kama vipi dili nae ili na wengine waache hizo tabia wanatuboa mbbaya ila pia unaweza kumchukulia kama hana akili poa mana ni habari ya uwongo all in all wadau wako tunakukubali na upo msatri wa mbele kutupa mwenyewe stori zako kama inayohusu wewe kupelekwa polis ulikuja kutuambia mwenyewe si tunasikiliza maneno yako na sio ya wapumbavu hao wasiokuwa nakazi ya kufanya...kamua mama No Name

REHEMA SELEMANI WA MWANZA said...

zama hata mimi imeshanitokea kwani kuna mtu alifungua account mpya ya facebook kwa kutumia jina langu na akaweka picha zangu yaani mpaka leo hata sijui huyo mtu ni nani na ana lengo gani jamani watu mmmh!!

Anonymous said...

Lulu kawa mswaki sahiv Tz maana matendo yake lol wengine hatumjui kwa mema bali.... @ Marium ni kweli Muv inaitwa who is smater kweli inakera.