Friday, January 21, 2011

MLEMAVU WA MACHO ANAEFANYA VIZURI KWENYE MUZIKI WA KIZAZI KIPYA...

Anafahamika kwa jina la MR. Hi na Mlemavu wa macho anaefanya vizuri sana kwenye muziki wa kizazi kipya anaetamba na wimbo wake wa NATAMANI...

amesema kwamba laiti angepata hata DAKIKA MOJA TU ya kuona basi kitu anachotamani sana kukiona ni DUNIA.. anatamani akipewa nafasi ya kufumbua macho japo kwa dakika moja basi aone hali ya dunia ilivyo kwani amekuwa akiisikia tu na kuimagine vitu..

Mbali na kuiona dunia MR. HI anasema ikiwa anapewa nafasi ya kumuona mtu mmoja tu basi ataomba aoneshwe MPENZI WAKE yukoje...

kwa hayo na mengine mengi usiache kusikiliza CLUB 10 siku ya JUMAMOSI katika redio yako CLOUDS FM ambapo hapo utakutana na PG KWEKA maarufu kama BAGHDAD saa tatu mpaka sita asubuhi ambapo humo utapata kumsikia kiurefu na kujua mengi kuhusiana na MR. HI!!!!

1 comment:

Anonymous said...

kiukwel Jamaa mmi nilipata kumwona siku ya tamasha vijana juu ya uchaguzi pale Biafla! yuko poa sana mpeni saport watu wa media ili atoke na yye