Monday, January 3, 2011

MY BEST PHOTOS 2010 (nilizozipenda).....

Picha ni ukumbusho mzuri sana na kwangu mimi ni kitu muhimu sana kwasababu naamini binadamu tunaenda tunabadilika kadri siku zinavyokwenda na hata siku moja hauwezi kurudisha wakati nyuma na hapo ndipo UMUHIMU wa picha unapojitokeza kwangu mimi, sababu utakavyokuwa leo sivyo utakavyokuwa kesho, na ulivyokuwa jana sivyo ulivyo leo na kitu pekee kinachotusaidia kutunza kumbukumbu ya jana juzi na majuzi isipotee ni PICHA and that is the reason NAPENDA SANA PICHA..

Kwa mwaka uliopita(2010) kuna picha nyingi nimepiga, baadhi nikiwa na watu na nyingine nikiwa mwenyewe, lakini katika hizo zote kuna zile ambazo nazipenda zaidi ingawa haina maana kwamba picha hizi ndio nzuri kuliko zote kwangu mimi na huenda hata wewe zisikuvutie kabisa lakini mi nazipenda tu na nina sababu tofautitofauti za kuzipenda....

Hizi ni baadhi tu katika zile ninazozipenda na nitaendelea kukuletea nyingine kwa awamu...
I can call it photo of the year kwangu mimi, it was during my Birthday 4th October 2010, mimi na Ephraim Kibonde.. Always nikikaa na huyu mtu karibu huwa nafurahi, na hapo mbavu zangu zilikuwa kwenye hali mbaya sana.. he makes me happy kiukweli.. na hii ni moja kati ya picha zangu ninazozipenda sana...

Hii ni picha nyingine ninayoipenda, hapo nikiwa na Mohammed Dewji kwenye Birthday ya muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.. October 2010.
Ni kama anaambiwa ATEEEN-SHEN... anaitwa Baghdad anapatikana Clouds FM ukitaka kumsikia utampata kupitia CLUB 10 kila Jumamosi... Amekaa kama yuko kwenye gwaride kwenye hiyo picha.. mguu pande.. mguu sawa.. naipenda hii pia!!!
Hizo ni chache tu katika nyingi.. awamu ya kwanza ndio hiyo.. awamu ya pili inakuja SOON...

1 comment:

THE BIG MIC 120' SHOW. said...

I like the pozi ya KIBONDE anaweza commedy naye huyo