Wednesday, August 4, 2010

MAMA LEVO ANANIFANYA NAJUTA KUJIITA BABA LEVO


mambo vp MZAZI

swala hili lipo hivi. ujue mwanzo nilikuwa naona ni faraja kwa mtoto wangu LEVO kama ntatumia jina la BABA LEVO coz mwanangu akikua ataona ni jinsi gani ninavyo mpenda mwanangu.
lakini kwa sasa baada ya kuachana na mama yake. {MAMA LEVO}imekuwa tofauti kidogo coz juzi nilikuwa na show kadhaa home kwetu kigoma so wakati nipo huko ndo nikawa napata story kibao za mama levo coz amekuwa maarufu huko kwetu utazani na yeye anaimba.

na bora hata angekuwa anafanya mambo mazuri ingekuwa sio mbaya lakini daaaa!!! yaaani amefungulia geti coz hata washikaji ambao walikuwa wanamuogopa zamani coz alikuwa na mimi leo hii wamekuwa wanamnywesha mapombe wanalalanae yaani ameharibu CV yangu yoote coz kila anapopita watu wanaonyeshana huyu ndo mama levo aliyezaa na BABA LEVO ni muhuni yaaani kawa kama mtu aliyetupiwa jini la ngono sijui.

nimejiskia vibaya sana coz wakimsema yeye wananisema na mimi kwa vile hili jina ninalo litumia BABA LEVO na yeye ndo MAMA LEVO.
wanawake bana.

KAZI NJEMA MZAZI WANGU

Nimeiwasilisha kama ilivyo kutoka kwa baba levo
.

1 comment:

emu-three said...

Usikonde mshikaji, jina halitafsiri matendo ya mtu, wapo watu wana majina mazuri lakini matendo yao hayaeleweki, yeye hiyo ya mama nanihii, haifuiki kwasababu ni mama yake nanihii eeeh, uchafu wake ni wake! Usikonde na wala usipungue uzito