Monday, August 16, 2010

UNAUFAHAMU UPUPU!!???

Huu ndio upupu kama umeshawahi kuuskia ambao mara nyingi watu wanatumia kumpulizia mtu ili kumkomoa ambapo kuwashwa kwake hakuelezeki.
Kiukweli kabisa sikuwahi kuuona kwa macho ndio mara ya kwanza kwahiyo kama wewe pia hukuwahi kuuona ndio huo hapo kama unavyoonekana.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

UPUPU...
Si dawa ya waalimu wakorofi (ambao walikuwa wakimwagiwa na wanafunzi watukutu enzi za shule zetu), lakini pia nimeuona upupu kama mboga.
Nilipobahatika kuishi mkoani Lindi, nilishangaa kisha kuuonja na hata kula upupu kama mboga. Ni kama maharagwe japo wanasema una sumu sana.
Nilielezwa kuwa wachemshwa kwa masaa mengi na maji humwagwa kama mara saba (tayari hapo wameshafanya de-nature na hakuna virutubisho vinavyosalia), na baada ya hapo ulikuwa ukiuzwa na kinamama mida ya jioni maeneo ya sokoni / gengeni.
Ilionekana kuwa biashara imuendesheayo mtu maisha (kama ilivyo uuzaji pombe)
Kwa hiyo UPUPU ni zaidi ya "kiwashio", bali pia kwa baadhi ya watu ni "mboga".
Blessings