Tuesday, April 27, 2010

MATUMIZI YA LUGHA YA KINGEREZA KWENYE FILAMU ZETU NI SAWA?

Ikumbukwe kabisa kwamba MLENGWA mkubwa wa filamu za kitanzania ni mwananchi wa kawaida sana ambae kingereza kwake si lugha anayoitumia kabisa na huenda hata haifahamu, Walengwa wakubwa wa hizi filamu ni wamama wa nyumbani, vijana wa kawaida tu na watoto, Hao wanaojua kingereza ni WACHACHE sana wanaoangalia, wengi wao hawazifuatilii kabisa hizi filamu za kwetu.

Lakini pamoja na yote kumekuwa na wimbi kubwa la kutumia lugha ya kingereza kwenye filamu zetu za kitanzania bila hata kuangalia kama kinachoongelewa ni fasaha ama la.

Si kitu kibaya kuongea lugha hiyo kama script inasema hivyo na wanaoongea lugha hiyo wana uwezo wa kuitendea haki, lakini kwa jinsi kingereza kinavyotumika inaonekaana kabisa kwamba kimechomekewa na hakukuwa na ulazima wa kutumika kwenye sehemu husika.

Nafkiri imekuwa kama FASHION na njia ya waigizaji kuonesha kwamba WANAJUA zaidi sababu kuna fikra potofu ambayo imejengeka miongoni mwetu kwamba kuongea kingereza ndio kuonekana umesoma ama unajua zaidi.

Lakini badala yake matumizi ya kingereza yanaleta matokeo tofauti kwani HAYAMPANDISHI yule mzungumzaji bali YANAMSHUSHA zaidi kwa watazamaji.
Na hiyo ni kupitia vitu kama PRONOUNCIATION(matamshi) ambayo mara nyingi inakuwa mbovu kuliko kawaida mfano kuchanganya R na L na vitu vingine, kitu ambacho kinatia aibu unapoangalia.

Kuna filamu nyingi sana zimeigizwa katika lugha tofauti kabisa na bado zinaeleweka na kupendwa hata kwa wasiojua lugha hiyo kupitia kitu kinachoitwa SUB-TITLE, ambazo hizi humfanya mtu asieelewa lugha inayotumika kuelewa filamu ile kwakuwa imetafsiriwa kwa chini.

Nafkiri SUB-TITLES ndio kitu kikubwa cha kuangalia zaidi na kukitilia mkazo kwenye filamu zetu.

Je kuna UMUHIMU wowote wa kuongea lugha ya kingereza kwenye filamu zetu ilhali TUNAIKOSEA????

7 comments:

Anonymous said...

Dada me naona ni bora waongee kiswahili kuliko kiingereza maana wanaharibu movie kuingiza lugha mbili yaani kiswahili na kiingereza na imekuwa shida sana na wamekuwa limbukeni ki halisi kutumia lugha ya kiingereza si kuwa msomi sana, hapa South Korea hawajui kiingereza ila wameweka (english subtitles) wakati wa editing na movie zao ni babkubwa na pia nimesikia hata huko wanaonyesha . wako huru sana ku act .Tanzania unakuta mtu ana force kuongea kingereza na hajui na sio grammar english ni bora waandike subtitles za kiingereza kama wanavyofanya mataifa mbalimbali, ona Japan hawatumii kiingereza na taifa kubwa wanapenda lugha yao je nyie mnao force kiingereza na hakiwapendi si muacheee??? usomi si kiingereza ni maarifa yako uliyopata hata kama ni kwa kiswahili shuleni na kama vipi ngumu kujichanganya na wasanii wenyekujua lugha basi rudi darasa la lugha ujifunze muongee vizuri na si kuingiza maneno na rafudhi chafu za kingereza mara Dat or that ndio hicho tuu be awake from ulimbukeni .

Kiswahili ni zaidi kwenye movie za hawa wasanii wetu kuliko kiingereza wanacho ongea kibaya

Mdau wa Z.

Benny
South Korea

Anonymous said...

yani umenigusa sana zamaradi mi nilikuwa nawaza ni wapi ningetolea dukuduku langu finaly umenisaidia.nakereka sana na kiingereza cha kwenye movie manake ni aibu tupu yani ukiwa na mtu anayejua unajisikia vibaya,pia hizo sub title bado pana kazi coz kuna moja niliangalia kwa kweli hapana watafute watu wanaojua.

Unknown said...

Watumie lugha ya taifa tu. mbona wenzetu wanatumia lugha zao za ndani? na movies tunaangalia? wameanza siku hizi kutupa maelezo kwa kingereza, zamani ilikuwa ni vitendo tu na kuhisi hapa anasema hivi. kiswahili tunakidumisha vipi? na kama kingereza basi iwe kingereza kilichonyoka ili tupate kuuza zaidi kimataifa.

mrembo said...

Na ukitaka kuwa adui yao waambie kuwa hawajui kiingereza lol

vei said...

bora 2 waongee kiswahili maana ni aibu 2pu hasa subtitle ndo usiseme nnachoweza kusema ni kwamba sisi ni watanzania na kiswhili ni lugha yetu ya taifa na tuikubali 2 swala lingine linalo udhi kwnye hiz movie ze2 ni ni kwamba kila m2 kwenye movie ana gorofa na nguo za bei ghal hata kama ana act part ya kawaida hapo uhalisia una potea coz hayo co maisha ya kawaida kwa watanzania weng

Anonymous said...

habari,kuongea kingereza ni sawa lakini tatizo letu tanzania nihuyo anayeitwa director of the movie nae hajui lugha.sasa ni broken kwenda mbele.kingereza kinakuza soko lakini not broken.shule muhimu ndugu zangu...sio wanunue magari tu kasomeni hata english course mtauza zaidi

Hans Megrah said...

Mi sioni umuhimu wa kulazimisha kutumia kiingereza.Ni hivi bidada.."English is a professional language and it needs professional people to speak professionally"...
Nimeangalia filamu mbili tatu wa hapa nyumbani ni matatizo matupu when it comes to English..Hebu tueleze Zamaradi unafikiri nini kifanyike ili tuweze kuwasaidia hawa jamaa zetu ambao lengo lao ni zuri ila maandalizi duni..