Tuesday, March 15, 2011

UNAWAKUMBUKA HAWA..!!!!?????

Waliwahi kuwika sana kipindi fulani kupitia tamthilia kwenye kundi la kaole.. unawakumbuka hawa!!!???
nakumbuka enzi hizo niko shule mdogodogo naangalia michezo yao na ikifika tu jumamosi nilikuwa sikosi kwenye TV...

Enzi hizo tamthilia zetu zilikuwa na msisimko wa hali ya juu sijui kwakuwa vilikuwa ni vitu vigeni ama labda kwasasa hakuna wakali sielewi, lakini zamani tamthilia zilikuwa juu sana na ziliweza kuteka watu wengi sana tofauti na sasa...

alikuwa na character ya peke yake.. unamkmkumbuka!!!???

Katika watu waliokuwa wananifurahisha na kunichekesha kwa kipindi hiko, huyu pia alikuwa ni mmojawapo na kikubwa ni maneno yake ya papo kwa papo na majibu yake ya ajabu (mashushu) akiwa na mumewe ambae nae alikuwa na misemo iliyopitiliza.. Unamkumbuka huyu!!!???? Hao ni baadhi ya watu ambao ambao waliwahi kushika sana kupitia vipindi vya kwenye LUNINGA(tamthilia) na kwa enzi hizo walikuwa juu sana kupitia michezo yao.. mimi nawakumbuka.. vipi wewe unawakumbuka!!??? kama ndio Unaweza kunitajia majina yao kuanzia huyo wa kwanza mpaka wa mwisho na nini kilikuwa kinakufurahisha kwa kila mmoja...
UNAWAKUMBUKA HAO!!!???

8 comments:

Anonymous said...

Yes Zamaradi mimi ni miongoni wa waliopenda sana kuangalia tamthilia za kaole..kwa kipindi hicho kaole ndio ilikuwa inashika si mchezo..
Huyo wa kwanza ni
1) NINA
2)KEMMY
3)BUPE
4)ZAWADI
5)BI STAR
6)BAHATI
Natumai sijakosea mpz...kuwa na kazi njema dear.

Anonymous said...

Huyo Nina yuko vizuri sana ana bonge la jumba kanunuliwa la milioni kama hamsini hivi. Anakaa karibu na kwa shekhe yahaya......
Ila amejiachia sana au ndiyo mambo ya fwedha haya bwana.......
Mke wa muhogo mchungu naye kawa bonge jamaniiiiiiiiii

Anonymous said...

nawapenda sana wasanii wa zamani. nakumbuka enzi za shule ya msingi sikosi mbele ya luninga ifikapo muda wa tamthilia zao. Wanajua kuact sio km wa sasa labda nilikuwa mdogo nilikuwa sioni kasoro.But they are good actress compare to wasasa

Anonymous said...

Nawakumbuka kwa sana wa kwanza ni:
1) NINA 2)KEMMY 3)BUPE 4)ZAWADI
5)BI STAR 6)BAHATI
Daah nakumbuka enzi zile wote walikuwa wanabamba ila bi star na mhogo mchungu walikuwa real alafu walikuwa the best.

Anonymous said...

the only down side sijui kama walifaidika financially na kuuza sua kwenye runinga

Anonymous said...

asante kuwaweka dear, nimefurahi kumwona dadangu Kemmy. Nina nilikuwa namfagilia ni balaa ila hapa nilishindwa kumtambua jicho.

Kokusima

Anonymous said...

Nakumbuka enzi hizo nilikuwa UDSM pale Mlimani acha kabisa hao waigizaji. Kulikuwa na mtu anaitwa Swebe, Kibakuri, Nyamayao na kama. Walikuwa wanatisha sana kwa kuigiza katika mazingira ya Uswahili. Nakumbuka kipindi ilikuwa vipindi vyao vilikuwa maarufu na vilikuwa vikishindana na tamthilia ya Babarita na ile ya katili Max Stocktel na kaka yake ambaye nimemsahau jina. Muhogo Mchungu, Bi Star na mtoto wao Kibakuri ilikuwa balaaaa. Hivi Bi Zawadi ulikuwa darasa la ngapi?

Anonymous said...

Nimefurahi sana kuwaona waigizaji wa zamani.
Bi Muhogo Mchungu alikuwa muigizaji safi sana katika mazingira ya Uswahili kama mdau mwingine alivyosema hapo juu na mtoto wao mmoja wa kike,yaani kale katoto ka kike ndio kilikuwa kinanifurahisha mno!Kalikuwa kanaact bila ya kuangalia camera,yaani effortlessly!
Dada Nina mbona amejiachia namna hii??Ukilinganisha alivyokuwa kwenye 'Girlfriend' na alivyo sasa ni tofauti!Alikuwa ana ueusi fulani,halafu nyororo kulikoni sasa?Kawa mueupe,hata mimi nimeshindwa kumtambua mpaka niliposoma comments za wenzangu!
Nawatakia kila la heri ktk maisha yao sasa.