Tuesday, March 15, 2011

HEBU TUJADILI HILI TAFADHALI...

Kwasasa hivi watu wengi sana wamekuwa wakifanya AUDITION (usaili) kwa ajili ya kutafuta waigizaji wapya wa filamu ambapo mara nyingi katika kutafuta waigizaji hao huwa kuna FOMU ambazo ni lazima yule anaetaka kuigiza ainunue kutoka kwa WASANII HAO WAKUBWA ambapo mara nyingi huwa zinauzwa kwa sh 5000 ama 10,000...

na ukiangalia asilimia kubwa ya watu wanaotaka kuwa waigizaji huwa hawana maisha hayo, uwezo wao huwa ni mdogo sana wa kifedha na hata nauli ya kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine huwa ni ngumu kwa upande wao (si wote ila wengi wao)...

Sasaunapomlipisha 5000 ama 10,000 ni sawa kweli!!!!???
Hivi hili swala la wasanii wachanga ambao hawajapata nafasi ya kufanya filamu kulipishwa PESA na wasanii wakubwa kwa kigezo cha kununua fomu pale ambapo wanataka kujiunga nao ni SAWA!!????

Hii imekuwa ni BIASHARA ama ndio njia ya kusaidiana!!!!?????

Naomba msaada tafadhali!!!

1 comment:

Anonymous said...

Dah yapa yap its true,ayaaa kweli kabisa then wanatoa forminauzwa buku 5 halafu wanataka mtu mmoja n mbaya zaid wanahitaji mtu mmoja then wametoa form mia ama 200 kwa haraka karaka anaramba laki tano ama mpaka mil. too be honest huo ni WIZI TENA MKUBWA tunawafahamu bhanaaaaaa tusifanyiane hivyo wabongo