Mtoto Lu Hao mwenye umri wa miaka mitatu akiwa na uzito wa kilo 60.
MTOTO Lu Hao wa nchini China ana umri wa miaka mitatu lakini ana uzito wa kilo 60.
Ana karibu mara tano ya uzito wa kawaida wa mtoto wa umri wake na anakula mabakuli matatu ya wali wakati wa chakula cha usiku.
Alipozaliwa alikuwa na uzito wa kilo 2.6, lakini baada ya miezi mitatu alianza kupata uzito wa ghafla.
Hao ni mzito sana kiasi kwamba mama yake mzazi, Chen Yuan, kwa sasa anashindwa kumbeba.
Analazimika kumpakiza katika pikipiki wakati wa kumpeleka shule ya awali badala ya kutembea kwa miguu.
Familia ya Hao imejaribu kumfanyisha mazoezi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumnunulia vifaa vya mchezo wa kikapu nyumbani na kumpeleka mtoni ili aogelee lakini imeshindikana.
Hata akifanya mazoezi ya aina gani anazidi kuongezeka uzito na wazazi wake wanadai kuwa mazoezi yanamfanya ajihisi njaa sana.
Lu Yuncheng, baba mzazi wa Lu ana wasiwasi na afya ya mwanae na anasema: "Akiendelea kukua kwa staili hii moyo wake utashindwa kufanya kazi vizuri."
PICHA NA HABARI kwa hisani ya Global publishers!!!
PICHA ZA DADA DINA CARE'S FOUNDATION WAKITEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA
VETERANI
-
Mwisho wa wiki hii kikundi cha Dina Care's tulitembelea kituo cha watoto
yatima cha Veterani kilichopo Temeke na kushinda pia kupata nao chakula cha
mchan...
10 years ago
5 comments:
yani huyo mtoto sio bure atakuwa ana tatizo,mie niko na miaka 24 na nina uzito huyo alionao yeye,yani umri wangu unaingia kwakwe mara 8 lakini tuna uzito sawa.
pole yake kwani no kubebwa kwa mtindo huo na pia maradhi ya moyo yapo mbioni kwani sio kawaida.
zama me cjawahikucomment ila leo imebidi, huyo dogo ni balaa, mie nna 21yrs cjawahi fika hata 55kgs, nacheza kwny 40s ila yeye du???? 60kgs, kiboko hiyo--- mie ESTER
noma
Ukistajabu ya Mussa utayaona ya firauni,mie sijawahi ckia mtoto wa miaka 3 kuwa kg 60!!honest its ma first time.
nampa pole huyo mtoto ila nawashauri wazazi wampeleke hospitali na kumpa vyakula visivyo na mafuta na visivyonenepesha.pia wamwombe Mungu amsidie mtomto wao naamini atapona kwani siyo hali ya kawaida.
Post a Comment