Wednesday, March 30, 2011

ILIVYOKUWA KWENYE PARTY YA KUMPONGEZA TWENTY PERCENT (20%)

Hii ilikuwa jana pale maeneo ya TABATA ambapo mkurugenzi wa GIBS media pro ambao ndio watengenezaji wa filamu ya 20% furaha iko wapi Mr. GIDO LEWANGA aliamua kumfanyia PARTY ya kumpongeza twenty percent kwa kufanikiwa kwake kunyakua TUZO TANO za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Hapo juu twenty akiwa na mkewe pamoja na mtoto wao (aliepakatwa na mkewe) kwa taarifa tu ni kwamba hapo mkewe alikuwa akitoa burudani kwani nae ni muimbaji na aliwahi kushirikiana na mumewe kuimba wimbo wa NINGEKUSAMEHE.. na ndio huo aliokuwa akiuimba hapo
Man water Man maji producer wa twenty akitoa machache kwa twenty...
Hilda hapo kushoto, Zamaradi katikati pamoja na Mrs. Lewanga hapo kulia
nikiwa na makaka.. huyo wa kushoto sikufanikiwa kupata jina lake ila huyo wa kulia ndio Editor wa Take one anaitwa junior ambapo hapo ilikuwa jana hapohapo tabata kwenye eneo la tukio..


Burudani ikiendelea.... ambapo baadae twenty alimsaidia mkewe na burudani ikaendelea...
With a friend hapo pembeni..

6 comments:

Anonymous said...

Nampongeza sana 20% na tuzo alizopata asibweteke atoe vitu vingine vikali sana..........
Huyu 20% nasikia anabwia unga sasa hivi maana naona bangi kaona haifai sasa sijui anaelekea wapi?Ona alivyoisha anazidi kuwa mbaya jamani hawa wasanii wa bongo vipi? Igeni wenzenu Kenya, na Uganda wanajitunza sana.
Nasikia kuna kundi kubwa la wasanii wa bongo flavour wanabwia.......
Vinginevyo anafanya vizuri sana
Jirekebisheni

Anonymous said...

jamani namkubali sana 20% yuko fit kwa utunzi na kuimba! ila ananiboa kitu kimoja hajui kuvaa kwa kweli sasa hizo ndevu si akashevu au nazo ni swaga?mweleze bwana Zama mwambie fans wake tunasema awe smart na unga aache anaonekana kachakaa sana.afterall napenda sana nyimbo zake.hopefuly utamfikishia ujumbe wangu

Anonymous said...

mm nampongeza kwa kweli uyo kaka napenda miziki yake sana kwa kweli nampa big up

middy said...

Hongera bwana mdogo 20% usibweteke kazi buti mwaya,mie nilikuwa napenda nyombo zako ila nilikuwa sio mshabiki wako kiviiiile ila pale tu nilipotanzama ile move yako ndo nikafall kwako totally n completelly na kusema kweli nilikuvotea sana tu na ucku ule wa tunzo tulipokuwa tunackia jina lako full kushangilia,na ww bwana kuonyesha kama huna tamaa hata
kidogo haukutia maguu.
Ila naye ajitahidi kuvaa coz hizo pamba zako lol sisemi wife mfanya mumeo awe smart bwana nini maana ya kuwa na mke kila cku namuona yuko raugh tu.
All da best kaka

Anonymous said...

Hongera zako 20,mwaka 2011 utokeze tena na ikiwezekana upate tunzo kama mwaka jana.
All da best kaka

Anonymous said...

20 hizo pamba zako tu mie hoi,hata hazieleweki,jikoki bwana unoke chicha.
Ukijifanya uko simple sana saa nyingine inaboa bwana,mie napenda mziki wako ila sipendi jinsi unavyovaa.jitahidi.