Wednesday, March 16, 2011

LEO TULIPATA UGENI KUTOKA DAYSTAR COLLEGE....

hawa ni vijana kutoka chuo cha uandishi wa habari cha DAYSTAR ambapo siku ya leo walifanya ziara ya kuja kutembelea hapa mjengoni na kuona jinsi vitu tofautitofauti vinavyoendelea hasahasa kupitia CLOUDS FM RADIO pamoja na CLOUDS TV.
Hapo nikiwa nao kwenye moja kati ya vyumba vya editing vya clouds TV ambapo ndio nilikuwa mwenyeji wao kwa siku ya leo..

Ziara ikiendelea katika sehemu tofautitofauti za CLOUDS TV.. hapo nilikuwa nikijibu baadhi ya vile nilivyoulizwa kuhusiana na Clouds TV na CLOUDS FM radio.
Kulikuwa na maswali tofautitofauti ambayo walikuwa wakiuliza ili kuweza kujifunza zaidi ukizingatia kwa kitu wanachosomea kinahusika zaidi na sehemu waliyotembelea leo..
Tukiwa katika moja ya vyumba vya Clouds TV ambapo huwa na watu tofautitofauti na ndio hapo walipokutana nao na mijadala ikawa inaendelea.
Joram Nyaumba ambae ni EDITOR wa Siz kitaa pamoja na 20 za town (aliekaa) akishangaa shangaa wageni..
zamaradi (mimi) akiendelea na maelekezo...
Hiyo ilikuwa ni leo majira ya saa sita mpaka saba katika ofisi za CLOUDS media group mikocheni ambapo wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari kutoka DAYSTAR COLLEGE walitutembelea kwa ajili ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na tasnia ya habari...

4 comments:

Anonymous said...

Kula vizuri angalau unenepe kidogo maana yake unatisha.......
Huna hata nyama mtoto wa kike

Anonymous said...

Its like kama wamekuja tu kushangaa shangaaa hawako kimasomo kwa jinsi wanavyoonekana ,lets be honest Zama ziara ya kimasomo kama wametembele studio at walitakiwa kucheki how matangazo yanavyokwenda hewani, time mnaporusha hewan nyimbo hivi how kuedit labda matangazo etc etc etc but sio swaga za kupigiana story kama mpo na ticha wa history kwa class bana bt si mbaya tumekuonana mdada ulivyotupia kiwalo umetoka woooo safiiiiiiiiiii hakunaga majotrooooooooooooooo

Jeff M said...

Ni mara yangu ya kwanza kufungua na kusoma 'blog' hii na, licha ya kuwa sijapata muda wa kutosha kusoma vizuri maelezo uliyoweka humu, napenda kukupongeza kwa kazi nzuri ya kuzitangaza filamu za wasanii wa Tanzania. Jambo moja linalonikera hapa ni tabia ya kupenda kuchanganya lugha ya kiingereza na kiswahili, tabia inayozaa lugha ambayo mitaani tunaita ki-swanglish. Naamini dada Zamaradi umefika kiwango kizuri tu kielimu hivyo sina shaka unaweza kutumia lugha ya kiswahili fasaha. Jitahidi kuacha hicho ki-swanglish na utumie kiswahili fasaha katika 'blog' hii, nadhani itapendeza sana. Huo ni ushauri wangu tu.

Anonymous said...

unatisha wa kike,keep it up