Thursday, February 17, 2011

KAZI NI KAZI... UNAMKUMBUKA JOYCE WOWOWO!!!!????

Nilipita mtaa mmoja mwananyamala nikamkuta mkaka anajitafutia riziki kupitia njia hiyo hapo, nakumbuka zamani tulikuwa tukiwaita joyce wowowo na mara nyingi walikuwa wakichezeshwa bolingo... sijui sasa hv kama jina ni hilohilo ama mambo yamebadilika... mwanamke nyonga!!!
hapa alikuwa akicheza ARAMBA ya mzee yusuph, anakatika mauno huyo balaa.. sijui huwa wanawaungaunga vipi mpaka anakuwa anatoa show ya aina yake na anacheza style zote kama binaadamu.. huu ni ubunifu wa hali ya juu kiukweli!!!
kazi moja tu
Mara nyingi huwa hayuko peke yake ila huhusishwa na mwingine wa KIUME ambae yeye huwa anacheza MABLEKA (shakers na break dancers) ambae jina lake limenitoka kidogo.. unakumbuka huyu wa kiume anaitwa nani??

Nilivutiwa na hiki kitu kwani ni mmoja kati ya vijana ambae ameamua kuwa mbunifu na kujiajiri mwenyewe kihalali bila kuchukua cha mtu kama wengine wanaotaka maisha ya haraka na rahisi..

KAZI NI KAZI bora mkono kwa tumbo..

1 comment:

Mbele said...

Safi sana hii. Nimeipenda. Naafiki kauli yako ya kumwenzi huyu jamaa kwa jinsi anavyojitafutia riziki kihalali.