Wednesday, February 2, 2011

MSANII AJIUA BAADA YA MAJIBU YA FORM FOUR

Msanii mchanga ambae alikuwa kwenye kampuni ya 5 effects chini ya William j. Mtitu AMEJIUA KWA KUNYWA SUMU siku ya tarehe 29 january 2011 baada ya kufeli kwenye mtihani wake wa FORM FOUR..

Inasemekana kuwa baada ya majibu hayo kutoka alisemwa na mzazi wake na hiyo hali ikamkwaza na akaamua kuchukua uamuzi huo mkubwa uliopoteza maisha yake.

DIANA amezaliwa mwaka 1992 na amefariki siku ya 29 january 2011 ambapo kiukweli inasikitisha kuwa amepoteza maisha katika umri mdogo sana..

Mbali na kuwa kwenye kampuni ya 5 effects DIANA pia ameshashiriki kwenye filamu ya ONE BY ONE ya dr. CHENI ambapo alicheza nafasi ndogo sana hivyo ni ngumu kumtambua.. nitajitahidi nilete picha yake kwenu muda si mrefu.

Tunatoa pole kwa familia ya DIANA, KAMPUNI YA 5 Effects na wote wanaomfahamu..
MUNGU amlaze mahali pema peponi AMINA!!!!!

5 comments:

Anonymous said...

masikiini pole zake...ila wapi picha yake jama

Anonymous said...

duh pole kwa familia jamani ila angekuwa na subira matokeo mwaka huu si kilio cha mmoja, masikini kapoteza ndoto zake zoote,

Anonymous said...

R.I.P Diana, kushindwa mtihani si maisha, please picha yake ZAMARADI ni muhimu mno

Anonymous said...

Jamani pole kwa familia na marafiki wa Diana.Kwa kweli,mzazi ana kila haki kumfokea mtoto anapokosa umakini ktk swala la elimu ila si kupindukia maana matokeo yanakuwa kama haya,tragedy ambalo sasa dhamira itamsumbua mzazi daima.
Kufeli si mwisho wa maisha,mzazi angeweza muandaa mtoto kuresit exams au kumpeleka course,siku hizi mbona kuna namna kibao za 'kutoka' kimaisha?
Inaelekea Diana alikuwa anapenda sana kuigiza zaidi ya shule so kama wazazi wake wana watoto waliobaki,wajitahidi wawe wachunguzi as to what watoto wanapenda au wana kipaji so waelemee kuwasaidia hapo kama shule inaelekea kutokuwa ni kipaji chao tena...
Regards..

Anonymous said...

wazazi msichoke kukemea watoto wazembe. FULL SUPPORT!