Friday, February 4, 2011

MAPENZI YAMSABABISHIA AJALI TITO

Kama unavyomuona hapo pichani msanii wa filamu MRISHO ALLY ZIMBWE maarufu kama TITO amepata ajali mbaya ya pikipiki iliyosababishwa na mgogoro wa mapenzi baina yake na mkewe siku ya juzi usiku kuamkia jana.
Sakata hilo lilianza alipokorofishana na mkewe ambapo hali hiyo ikamfanya aamue kutoka usiku ili akajichanganye na washkaji akipoteza mawazo lakini badala yake huku akiwa na chombo cha moto (PIKIPIKI) na mawazo ya mkewe kichwani akajikuta amejipiga kwenye msingi na kupata ajali mbaya ya pikipiki iliyosababisha majeraha sehemu zake za mwilini na kupasuka kichwani..

Baadhi ya majeraha ya kichwani

Tangu apate ajali mke wake amefika maramoja tu Hospitali kumuona na kuna mengi sana ambayo TITO ameongea kuhusiana na mkewe na sababu za ugomvi wao wa mara kwa mara ambapo kupitia TAKE ONE utapata kujua mambo yote hayo

Majeraha ya mguuni

Hivyo ndivyo ambavyo alivyo kwasasa baada ya ajali.

Kwasasa ametoka kwake alipokuwa anaishi na mkewe na yuko kwa dada yake ambapo ameamua kukaa kujiuguzia huko.
Usikose TAKE ONE siku ya JUMANNE saa tatu kamili usiku.

9 comments:

Anonymous said...

ndoa hizi,uzisikie tu.halafu jamaa akitafuta nyumba ndogo utamlaumu?{ingawa sio jambo zuri)juu ya ugomvi wenu ndani,ukisikia mume wako kapata ajali,kama wewe ni binaadamu,ugomvi wenu unauweka pembeni,unamjali mumeo,na pengine ugonjwa wake unakufanya umhurumie mumeo,lakini bi dada hata hospitali hakukupita.jamani tuwe na huruma

Jamaa ktk filamu nyingi anapenda ku-ect mmbabe sana kwa wanawake hapo hajashusha kipondo kweli! ila mpe pole sana couz kati ya watu ninaowakubali ni Tito so Ugua pole utapona tu!

Anonymous said...

mnapenda sana kujaji upande mmoja kwanini msimsikilize na upande wa pili? hata huyo jamaa nae pia anamakosa ndio maana kwa aibu amekimbilia kwa dada yake, hawa wanaume waone tu hivi hivi wamevaa na kufunga mkanda lakini yanayoyfanyika huko ndani ni hatari jamani. inawezekana hata huyo mkewe amechoshwa na mambo yake.

Anonymous said...

zamaradi kipindi cha takeone jumapili kinarudiwa saa ngapi/ maana kwetu mgao wa umeme j4 sisi hatuna umeme

st said...

Habari yako Zamaradi huwa napenda sana kukusikiliza kenye kipindi cha leo tena sijawahi kubahatika kuona kipindi chako cha take one sababu ya mgao wa umeme siku ya jnne, huwa jpili hakirudiwi kweli tuna mic sana. Arusha

Anonymous said...

hana lolote, kama kweli yeye mwanaume mwenye busara kwann asisuluhishe matatizo yake badala yake akaamua kuondoka na kwenda kulewa. kisa cha yeye kuanguka ni ulevi wala si mkewe kama anavyosema. it shows hayuko serious kwasababu kwann amwache mkewe akimbie kwa dadake? kua kaka matatizo ya nyumban si ya kutangaza unataka tukuone mwema sana au unataka tukuone tena baada ya kukaaa kimya sana mmmmhhh....

Anonymous said...

pole kaka lkn hebu tuangalie hii ishu kwa jicho la uchunguzi... mwanamume akigombana na mkewe haondoki. akiondoka ina maana kakimbia ukweli (ukweli unauma). halafu kuamia kwa dadake pia ni dalili kwamba hapo wanapoishi (yeye na mkewe) si kwake ni kwa huyo mwnamke anayemwita mkewe (si jambo la kushangaza kwa wasanii) so mwanaume ukiishi kwa mwanamke utanyanyasika tu hasa hawa mademu wa siku hizi ndio simu ikiita anaenda kupokelea chumbani ama nje kabisaaa! take care.