Thursday, February 24, 2011

MICHAEL JACKSON ALIVYOFARIKI NILILIA SANA - MC KENYATTA

Anaitwa MC kenyatta ambae ni muigizaji wa filamu wa hapa Tanzania lakini at the same time ni Dancer mashuhuri wa enzi hizo ambae alikuwa akipenda sana kucheza nyimbo za King of pop Michael Jackson....
Kenyatta anasema wakati MICHAEL JACKSON anaumwa alikuwa na unyonge wa hali ya juu na aliposikia habari za kifo chake ALILIA KULIKO KAWAIDA...
Na sababu kubwa iliyomfanya alie sana ni mapenzi yake ya dhati kwa MJ (Michael Jackson).
Baadhi ya CHEJO zake za Ki-MJ... hapo alikuwa ananitolea show ya ukweli ya Michael Jackson
Ukimuuliza SABABU KUBWA iliyomfanya ampende MICHAEL JACKSON, Mc Kenyatta anasema sababu kubwa ni kwakuwa MICHAEL JACKSON ALIKUWA AKIPENDA SANA WATOTO na kwa matatizo aliyoyapata yeye utotoni anatamani sana MICHAEL JACKSON ANGEMUONA AKAMCHUKUA ili aondokane na shida hizo, hivyo alikuwa akimuangalia MICHAEL kama mkombozi fulani.. na kingine alikuwa akipenda anavyocheza...

UNAWEZA UKASHANGAA SHIDA GANI ALIZOPITIA LAKINI KUNA SIRI KUBWA SANA NYUMA YA MAISHA YA MC KENYATTA AMBAPO NTAKULETETEA HALI HALISI YA MAISHA YAKE MUDA SI MREFU ila kwa DONDOO tu ni kwamba hivi unafahamu alivyokuwa mdogo ALIIBWA KUTOKA KWA MAMA YAKE MZAZI NA AMEKUWA AKILELEWA NA MAMA AMBAE SIO WAKE KWA MUDA WOTE HUO ( ALIEMUIBA) na hivi sasa ANAMTAFUTA MAMA YAKE MZAZI!!!.. kwa yote haya endelea kuwa na mimi ndani ya blog hii na nitakuletea kisa cha maisha yake kama kilivyo....

Lakini pamoja na yote hayo MC KENYATTA pia ni MC mashuhuri sana wa sherehe mbalimbali kama MAHARUSI, SEND-OFF, VIPAIMARA na shughuli yoyote ile na huwa anaimudu sana kazi yake kama MC kwani ni mtu ambae hufurahisha sana anapofanya shughuli hizo na mara nyingine hutoa hadi hizo SHOW za Michael Jackson katika kuchombeza.. hivyo kama una harusi yako, send-off, Ubatizo, Birthday, Kipaimara ama SHEREHE YOYOTE ILE unaweza ukamcheki kupitia namba zake za simu ambazo ni 0715-226005 au 0754-226005 ama 0689-226005. na anaweza akafanya sherehe yako iende sawa kabisa..

2 comments:

Anonymous said...

hhahahhahhaha zamarad we mtundu sana umenchekesha ulivyotumia neno chejo ktk picha za huyu bwana kaka..
I adore you

Anonymous said...

kaza buti kaka. sahau yaliyopita. utampata mama yako. ila..... ila.... kumbuka hili neno nakwambia. Mungu alikuwa na sababu ya kukutenganisha na mama yako. you never know labda usingekuwepo kabisa au ingekuwa ni afadhali na kutokuzaliwa kwahiyo usisikitike sana ni mipango yake huyu Mungu asiyekosea kamwe! kumbuka hili daima na uta-move on.