Thursday, February 17, 2011

WAANDISHI WAMETUTENGA WATU WA MIKOANI - JULLY TAX

Hapo nikiwa kwenye interview na mtengeneza filamu kutoka MWANZA,
Anaitwa JULLY TAX, ni mmoja wa watengeneza filamu wakubwa kutoka mkoa wa MWANZA na hata TANZANIA kwa ujumla kwani ameshatengeneza filamu nyingi ambazo zinafanya vizuri sokoni kama SALADIN ambayo ilijipatia umaarufu mkubwa sana, MTEMI, MAMA WA KAMBO, RADI COBRA na nyinginezo nyingi sana..
Anasema changamoto kubwa sana wanayoipata watu wa mikoani ni kuwa mbali na MEDIA tofauti na wasanii wanaofanyia kazi DSM.. aliendelea kwa kusema si kwamba wao hawafanyi kazi nzuri ila media haijui kazi yao kwani inajali watu wa DAR peke yake na haitambui wala kujua kuhusiana na kazi za mikoani.... hapo akiwa na mwanadada aliefanya filamu ya SALADIN kama saladin wa kwanza kushoto....
Kikubwa anachoshukuru ni kukubalika zaidi kwenye nchi za jirani hasahasa CONGO ambapo wanatambulika zaidi na zaidi kuliko nchi yao ya TANZANIA...

No comments: