Wednesday, February 2, 2011

ALIEIGIZA KAMA SHOGA AVIMBISHWA TUMBO...

Mtu alieigiza kama shoga kwenye comedy ya mtoto wa mama jana yalimkuta yakumkuta baada ya tumbo lake kuvimba na kifua kuwa kinapanda na kushuka, hali hiyo imemkuta baada ya KUIBA saa yenye thamani ya shilingi MILIONI MOJA ambayo ni ya mtu ndani ya familia yao

Inasemekana hiyo saa ilivyoibiwa ulitolewa muda wa mtu alieiba kusema na kukiri ili kisifanywe chochote watu wakaona kama utani lakini kilichotokea SIKU YA JANA akaitwa MGANGA ndani ya nyumba ambapo wana familia wote wakapewa dawa ya kunywa na kila mtu akanywa ile dawa ambapo mtu alieiba ndio hiyo dawa itamfanya vya kumfanya.

Ghafla tu baada ya kunywa DANNY ambae ndio huyo unaemuona hapo juu hali ikawa mbaya akaanza kuhaha mara TUMBO likaanza kunguruma na kuvimba ambapo lilikuwa LINAPANDA na KUSHUKA... mbali na tumbo pia kifua kikawa kinapanda na kushuka na hali hiyo ikimtokea anakuwa kama anahaha ANASHINDWA KABISA KUONGEA analegea anakuwa hoi macho yanamtoka, lakini baada ya muda hali hiyo inamuachia.. baada ya muda tena inarudia tena na hali ikawa inaendelea hiyo..

Baada ya kutokea hivyo baadae ALIKIRI kwamba ni yeye ndie alieiba hiyo saa lakini ameshampa rafiki yake ambae alikuwa anatafuta nauli ya kwenda South Africa hivyo hiyo saa waliiuza ili nauli ipatikane na jamaa kashasafiri...

Wakati anaongea na mimi siku ya jana alikiri na kusema HATARUDIA TENA kwani tayari AMESHAADHIRIKA vya kutosha, Pamoja na kukiri kwake bado hali hiyo iliendelea ambapo ili imuachie lazima kutolewe LAKI MOJA kwa mganga ndipo mganga huyo atamuachia awe sawa..

Mpaka naondoka eneo la tukio hali yake haikuwa nzuri kihivyo na hata pesa ilikuwa bado haijakamilika pamoja na mchango uliokuwa umepitishwa kwa wana familia ili pesa ipatikane sasa sielewi kama kwasasa hali hiyo imemuachia.. ama la!!!

imetokea jana magomeni huko.. WADAU MPO??????

7 comments:

Anonymous said...

Tanzania tuna kazi kubwa sana kujenga /kutoa mawazo ya kishirikina tunahitaji elimu sana familia nzima mnakaa mnajadili kumuita mchawi/mganga??????? mnaamini giza katika karne hii ya 21?? maskini wazazi ndugu hamna kitu kabisa.

Anonymous said...

Zamaradi...hivi kweli kuna uganga? unajua mimi siamini ati?

Anonymous said...

pole Danny ibilisi gani alikupata maskini polee ila ujifunze kuiba si kitu kizuri.............. watu hao wanaojidai hawaamini ushirikina wanafiki wao ndo wakwanza wakichelewa kazini wakisemwa kidogo na boss wa kwanza kupiga ramli kuuliza nini tena mbona sipemdwi na boss hebu acheni unafiki bwana aaaahhhaaaa.

Anonymous said...

Hawa waganga wanatumia saikolojia. Kuna hali fulani ambayo inaitwa 'psychosomatism' ambapo ukiamini kuwa una ugonjwa fulani basi dalili hizo zinajitokeza. PIli, ukichanganya na uvugaji (hypnotism) ndipo unapata hali hiyo. Ukivugwa (yaani ukiwa hypnotises) unaweza kuambiwa (suggestion) kuwa mtu aliye mwizi atatokwa damu ya pua au atavimba na kweli hayo yakatokea kwa kuwa 'suggestive mechanism' yako ndiyo inayofanya kazi. Huyo jamaa alikuwa na kitu cha kujua kuwa yeye ndiye kaiba ('guilt conscience') na kwa hivyo alipokuwa hypnotised alijipa self-suggestive command iliyofamya tumbo lake livimbee!!!! Si uchawi, ni saikolojia.

Anonymous said...

AIIIBUUUUUUUUU MSANII MZIMA UNAFANYA KAMBO YA KIJINGA, NA INAWEZEKANA KWELI SHOGA WEWE NA KWA JINSI ULIVOKAA KISHOGA SHOGA, TUKIRUDIA KUKUHOJI PEMBENI MGANGA MWENYEWE UTASEMA KWELI MIE SHOGA. NYAMBAFFFFF

Anonymous said...

Tuache mambo ya uigizaji. Naomba kuuliza: huyu jamaa kweli amesalimika?

Anonymous said...

anon wa February 3, 2011 5:49 PM maelezo mengi na ref za uhakika lkn ni hivi uchawi upo hata ktk vitabu vyote vitakatifu inathibitika. musa alipambana na wachawi wa faraoh. hali kadhalika kwenye koran ipo mifano pia.