Tuesday, February 8, 2011

NIMEMKUMBUKA SANA BABA YANGU LEO...

Imefika miezi Tisa na siku kadhaa sasa tangu afariki dunia, na kila nikikaa mara nyingi huwa ananijia kichwani na huwa namkumbuka sana, lakini sielewi KWANINI LEO imetokea NIMEMKUMBUKA SANA BABA YANGU kuliko kawaida mpaka kufikia hatua ya kulia sana leo..

Pengo lako halitazibwa na mtu yeyote yule kamwe kwani kwangu haukuwa baba tu ila ulikuwa zaidi ya baba, kwangu ulikuwa rafiki, mtetezi, babu, mshauri na zaidi ya yote ulikuwa ni mtani wangu mkubwa sana.. nikiwa na mama huwa hatuishi kukuongelea ama kuingia tu kwenye maongezi yetu.

Nakukumbuka kwa mengi sana baba lakini kubwa hata kinitokee kitu chochote uwepo wako ulikuwa ni ngao tosha kwangu mimi..

Pamoja na kwamba umeondoka nakushukuru sana kwa mengi ambayo umenijengea na kunifanya zama mpaka leo niwe zama kutokana na malezi yako, Ulinijengea kupenda watu, kuheshimu kila mtu kwa umri wake, lakini kubwa nakushukuru sana kwa kunilea kwa mapenzi makubwa sana yaliyonijengea KUJIAMINI kwenye kila ninachokifanya na hii yote ilitokana na malezi yako wewe baba.

Natamani sana ungekuwepo lakini MUNGU ana mipango yake ambayo ina maana kwenye kila jambo na hawezi akalaumiwa kwa hilo..

Am glad siku ambayo ndio ulikuwa unaiacha hii dunia, masaa machache kabla hujakata roho nilipata nafasi ya kukwambia NAKUPENDA.

Ulikuwa ni MMOJA tu na hatatokea tena baba mwingine hapa duniani, Nakupenda sana baba, upumzike kwa amani na MUNGU akulaze mahali pema peponi
AMINA!!!

Hii ilikuwa ni safari ya mwisho ya baba yangu.. picha kwa hisani ya issa michuzi yeye ndio aliipiga hii picha

SITAISAHAU HII SIKU KATIKA MAISHA YANGU!

21 comments:

Ngoi said...

R.I.P my lovely grandfather Hussein Majuto wa Mketema. Nitakukumbuka daima. M

Anonymous said...

pole sana dadangu najua sio rahisi kumsahau ila la muhimu ni kuzidi muombea kwa mwenyezi Mungu ili aweze pata pumziko la milele nasi tuzidi muombea. Pole sana Dada

Anonymous said...

pole sana zama, kikubwa unapomkumbuka baba ni kumtilia ubani na kumuombea heri huko aliko pawe bustani yake nzuri, allah anakukumbusha kwa hilo sys.

Anonymous said...

Pole sana, mie pia nimefiwa na Baba yangu since 1993, lakini ni kama jana ninavyoona, kinachotakiwa ni wewe kunfanyia kisomo ikiwewzekana Alhamisi hii Mungu akipenda, wazazi wanahitaji kusomewa kila wakati.

Gwakisa said...

POLE DADANGU YOTE MIPANGO YA MUNGU YEYE AMETANGULIA NA SIE TUTAFUATA MUOMBEE DUA!KWA MWENYEZI MUNGU

Anonymous said...

duh pole zamaradi kila kitu ni mpango ya mungu, na kila nafsi itaonja umauti kikubwa na kinauma kutanguliana tu, jipe moyo muombee baba aili apumzike kwa amani,,

Anonymous said...

pole sana Zamaradi.

RUKIA MEZA said...

POLE ZAMARADI UWE UNAMSOMEA DUA, HATA ME NAFAHAMU JINSI MZEE MKETEMA ALIVYOKUA, ALIKUA MCHESHI SANA

MWINYI said...

pole sana zama bt thts hw lyf z i believ tht he z having a good tym wit angelz in heaven ryt nw kip praying for him..ADVOCATEE MWINYI

Anonymous said...

Pole mummy umeniliza maskini huwezi kusahau ila muombee inshalaah

Anonymous said...

Wadau, Kila unapomkumbuka mtu wako aliyetangulia mbele ya haki, inatakiwa umuombe Mwenyezi Mungu amsamehe mja huyo na umuombe Mola amuweke mahali pema peponi marehemu huyo.

Anonymous said...

Pole sn Zamaradi bt kumbuka Mungu anamakusudi kwa kila jambo ktk maisha yetu.Stay blessed!!!!!!!

Beauty Touch in Dar said...

japo wewe ni muislam, namimi ni mkristo, lakini lengo letu wote ni kuiona mbingu, biblia inasema hivi, mshukuruni bwana kwa kila jambo, zamaradi, pole sana, najua unaumia mno, najua hutasahau hata kidodo, endelea kumuomba mungu akupe nguvu za kipekee, akupe ujasiri akupe uvumilivu, najua kusahau ni ngumu sana, lakini mungu atakutetea,
pole dear
MAMA TRACY

Anonymous said...

kama wewe ni muislamu basi umrehemu baba kwa kisomo na sadaka, umemkumbuka kwa kuwa anahitaji dua zako

Anonymous said...

POLE ZAMA KAZI YA MUNGU . ILA MMNAWAZO UWEKE TOP TEN YA WASANII WANAOCHUKIWA NA WASHABIKI NADHANI HEMEDI ATAKUWA NAMBA MOJA TEHEEE. USIWAANDIKE MAJINA TUAMBIE TU MASHABIKI TUTOE MAONI ALAFU UTANIAMBIA

Hawa said...

Mmmhhh!! INALILAH WAINALILAH RAJUUN! Zama kikubwa ni kumuombea tu dua na c kingine mdogo wangu. Kumbuka cc wote safari yetu ni hyo2 moja, na kazi ya MUNGU haina makosa. So pia yatupasa kumshukuru MUNGU kwa makusudio yake yote anayofanya. Mi2 pia nilifiwa na wazazi wote wawili nikiwa mdogo sana. Ukikaa s'times lazima its pain sana lkn ndo hakuna jinc. M'mungu azilaze ROHO za marehemu wote mahala pema peponi AMENI!!! Pole sanaaa!

Zamaradi said...

ASANTENI SANA WOTE KWA MAPENZI YENU KWANGU NA MOYO WA UPENDO MLIOUONESHA,NIMEFARIJIKA SANA..
NAWASHKURU SANA WOTE na MUNGU AWABARIKI SANA..
TUKO PAMOJA!!!

Anonymous said...

Zamaradi Pole sana yaani huwezi kusahau na huwezi kuacha kulia kila unapokumbuka ila kama ulivyoshauriwa na wapendwa kuwa cha msingi na muhimu zaidi ni DUA TUU!! Leo hata mimi nilimkumbuka sana mdogo wangu MAGRETH I. MAPALALA alifariki 25/12/2009lakini naona kama ni jana nimelia sana toka jana lakini mwisho nimeamua kumuombea na kumshukuru Mwenyezi Mungu.M.M

Anonymous said...

Mmh dada yangu, umenikumbusha mbali kweli. kifo bwana usikie kwa mwenzio tu. Pole sana, swala kubwa nikumuembea mwenzetu aliye mbele za haki. Mwenyezimungu ampe pepo na amuepushie adhabu za kaburi. aamin.

Anonymous said...

Pole sana Zama, Endelea kumwombea uko alipo, kamwe hutamsahau na kila ukimkumbuka lazima ulie, hata mimi huwa hunitokea sana nikimkumbuka Baba yangu aliyefariki miezi 5 sasa,Jipe moyo mkuu dear.

latifa said...

Ananiuma saana mzee Mketema sitamsahau milele hasa pale alipokuwa anafunga safari kutoka kwake mpaka ofisini kwangu kuniletea machungwa na sometimes kunitumia ujumbe niende nyumbani kwake kuabadilishana mawazo as I was Mnyamala Ward Extv Officer, really miss u babu....Inshallah m. mungu akuepushe na adhaba za kabur...RIP MZEE MKETEMA.