Thursday, February 17, 2011

SIJAWAHI KUTOKA NJE YA NDOA - JB...

Hapa nikiwa na JACOB STEVEN (JB)
Katika Interview niliyofanya na JB amesema ANAMPENDA SANA mke wake, hajawahi na wala HATOKI NJE YA NDOA na hana sababu inayomfanya afanye hivyo kwasasa kwani mke wake ni mmoja kati ya WANAWAKE WAZURI SANA HAPA DUNIANI kwake yeye na anampenda kuliko kawaida na kikubwa yeye ni mwokovu na anampenda YESU....

JB yuko kwenye ndoa na mke wake anaefahamika kwa jina la QUEEN IRENE na wanakaribia miaka saba katika ndoa yao, nilivyomuuliza kuhusiana na familia JB alisema hajabahatika kupata mtoto lakini yupo kwenye HAPPY MARRIAGE na haoni kama anapungukiwa ama amepungukiwa chochote kwenye hilo na ni mara chache sana ambazo hukaa na kukumbuka yeye na mkewe kwamba hawana mtoto kwani ndoa yao ni moja kati ya ndoa zenye furaha pamoja na kwamba hawana mtoto hata mmoja.

Katika vitu vilivyowahi kumuumiza JB ni pamoja na kifo cha rafiki yake wa karibu sana MOHAMMED MPAKANJIA ambapo JB amekiri kuwa ana marafiki ndio lakini HAKUNA ALIEZIBA PENGO LA MPAKANJIA kwani alikuwa ni zaidi ya rafiki kwake yeye.

Huyo ndio JACOB STEVEN ama JB moja kati ya WAIGIZAJI WAKALI SANA ambao mimi personally nawakubali sana kiuigizaji na hayo ni baadhi ya mambo yanayohusiana na maisha yake.... BIG UP sana kwako brother, kaza buti kwani UNAWEZA SANA!!!

2 comments:

Anonymous said...

Jb na QEEN nawafahamu vzuri sana ndoa yao ina miaka tisa sasa na kitu wameoana tangu 2002 na mimi nilihudhuria harusi yao kuhusu kumpenda mkewe kwa nijuavyo mimi anampenda sana,na hakuna muigizaji bongo anaejaribu kumfikia JB yuko juu kiukweli

Anonymous said...

Mimi ni fan wa JB,kuanzia michezo kwa TV mpaka filamu,hasa version yetu ya 'Deliver us from Eve',bab kubwa role aliyocheza mule!
Ingependeza kama ungeweka picha ya yeye na mkewe Queen.
Ninachomuomba kaka yangu asiongee statements kama hizo kwani Shetani ana miguu mingi,kuna mijitu hawapendi amani iwe kwa wenzao,linaweza jitokeza lijanamke likamuharibia ndoa yake bure!