Anaitwa DESMOND ELLIOT mmoja kati ya waigizaji wa kiume wanaofanya vizuri sana Nigeria, na mpaka sasa ameshafanya filamu zaidi ya MIA MBILI. Mbali na Uigizaji pia ni Director mkubwa Nigeria na ni MUHITIMU WA UCHUMI kutoka LAGOS STATE UNIVERSITY . DESMOND ana MKE na watoto wawili, Rafiki yake wa karibu ndio aliesababisha yeye kuwa muigizaji baada ya kumshawishi sana aingie kwenye fani hiyo kwa kumuona anaweza. Baadhi ya filamu ambazo ameshawahi kufanya ni pamoja na MEN WHO CHEAT, YAHOO MILLIONAIRE na nyingine nyingi.
Desmond Elliot anatarajiwa kuja Tanzania kwa ajili ya MWALIMU NYERERE FILM FESTIVAL ambalo ni tamasha jipya kabisa la filamu litakalofanyika hapa DSM kuanzia tarehe 14february mpaka tarehe 19february 2011.
Katika tamasha hilo kutafanyika mambo makuu matatu ambapo kwanza kutakuwa na UZINDUZI WA SHIRIKISHO LA FILAMU LA TANZANIA (TAFF), pia kutakuwa naFESTIVAL yenyewe ambapo filamu tofautitofauti zitaoneshwa za hapa ndani ya nchi na hata zile zilizofanywa na watanzania waishio nje ya nchi na kingine ni TAFF SPECIAL AWARDS ambazo hizi ni tuzo za heshima kwa wale waliofanikisha na kusaidia filamu za hapa kwetu Tanzania.
Mbali na vitu hivyo baadhi ya activities zitakazokuwa zinaendelea kwenye tamasha hilo ni pamoja na WORKSHOP mbalimbali ambazo zitakuwa zikifanyika kuanzia saa NNE asubuhi mpaka saa KUMI jioni na baada ya hapo WATOTO watapata nafasi yao pia ambapo kutakuwa na maonesho ya filamu za watoto na hii itakuwa kuanzia SAA 10 - 12JIONI na usiku ndio kutakuwa na activities tofautitofauti.
Haya yote yatafanyika pale LEADERS CLUB kuanzia tarehe 14 FEBRUARY mpaka tarehe 19February..
TUJITOKJEZE KWA WINGI KUENZI VITU VYETU NA KUSUPPORT KAZI ZETU ZA NYUMBANI
PICHA ZA DADA DINA CARE'S FOUNDATION WAKITEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA
VETERANI
-
Mwisho wa wiki hii kikundi cha Dina Care's tulitembelea kituo cha watoto
yatima cha Veterani kilichopo Temeke na kushinda pia kupata nao chakula cha
mchan...
10 years ago
1 comment:
Zama naomba nikurekebishe kdg. Kama cjakosea Desmond ana watoto wa4 tena boys na ni twins mizao miwili hyo. Wa kwanza wana 4yrs na wa pili bado wadogo cna hakika wana umri gani!! Ninavyofaham mimi through magazine. By ma2 wa2
Post a Comment