Wednesday, October 26, 2011

THE LOST ADAM - moja kati ya filamu nilizozipenda kwa mwaka huu...Nimeangalia filamu nyingi sana kwa mwaka huu na hiyo ni kutokana na kazi yangu pia.. Kiukweli kuna improvements nyingi sana kwenye filamu zetu kwasasa lakini mara nyingi kitu ambacho huwa kinatuangusha ni STORY za filamu zetu.. nyingi ziko too shallow, na haya mambo ya part one na two ndio kabisa yanazidisha u-shallow kwenye filamu

Lakini pamoja na kwamba story nyingi ziko Shallow, bado kuna watu ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye filamu, ambapo hata kama story ni ya kawaida utakutaSCRIPT yake imesimama na hata DIRECTOR anakuwa ameitendea haki kiasi kwamba unaangalia filamu na unaona kabisa kwamba hii filamu imedirectiwa..

Moja kati ya filamu nilizoziona na zikanifurahisha kwa mwaka huu.. ni filamu ambayo imedirectiwa na Mtitu Game ambayo inaitwa THE LOST ADAM..

Kikubwa ni Uchezaji wa baadhi ya watu humo ndani.. ni kwamba wamefanya vizuri sana nikianzia na ROSE NDAUKA ambae amevaa uhusika vilivyo kabisa, JACOB STEVEN(JB) pia amefanya vizuri sana na naweza kusema huyu ni mtu ambae kwa movies zake nilizowahi kuangalia naweza kusema Hajawahi kuniangusha.. pia kuna Patcho Mwamba, Hemed Suleiman na wengine wengi ambao kila mtu amekamua kwa nafasi yake..

Kikubwa nampongeza sana Director wa hii filamu kwa kazi aliyoifanya kwani ukiangalia filamu yenyewe unaona kabisa kwamba imekuwa directed na mtu ambae yuko serious na anaijali kazi yake, ila zaidi angalia hiko kipande hapo juu ambacho ni MOJA kati ya SCENES nilizozipenda sana kwenye hii Filamu..

9 comments:

Anonymous said...

hii movie ni nzuri mno,rose ndauka ameubeba uhalisia vilivyo,na si yeye peke yake,wote walio act wamejitahidi mno.na mwisho wa mchezo ni kama surprise mkewe biggie kujitokeza.huwa napenda michezo ambayo mwisho wake hujui utaishia vipi.maana kuna movie nyengine,ikianza tu,unajua mwisho unaishia vipi.kama ulivy6osema zama,pongezi pia kwa director.

Muga said...

Du Zamaradi picha (movie) imesimama ingawa kuna parts ambazo hazipo connected na hiyo movie yenyewe Mfano pale Rose anapokimbia na kuanza kutapika, na pale anapoenda kutambulishwa kwa maadili ya kibongo hauwezi kwenda kutambulishwa kwa wazazi ukiwa umevaa vile, kwa hilo hakuwa katika uwalisia wa kitanzania, nashukuru kuona kwamba JB akuwangushi sio wewe tu hata mimi namkubali sana mtu huyo,

Anonymous said...

nimeikubali zam ngoja niende dukani nikanunue

Anonymous said...

dada kazi yako nzuri sana ila kama presenter kuna maneno inabidi uwe mwangalifu sana hautakiwi kutumia mfano neno KICHAA...huwa tunasema mgonjwa wa akili ni hayo tu.

Anonymous said...

izo nywele ungezibana zisingekusumbua kwnza km hujachana mi mamywele yenu yakubandika siyapendagi haya. uso umekuvimba sijui huna mood ya kutangaza

upendo msuya said...

Zama hata miminimeiangalia kwa kweli ni nzuri sana,I think now there is a need for u kuwa unatuambia hata sisi fan wako movie gan ya kibongo iliyoingia ambayo ni nzuri ili tununue, maana movie nyingine za kigongo sasa zinanikera sana, kama movie niliyonunua juzi ya aunt ezekiel inaita SAME GIRL upuuzi mtupu.

Anonymous said...

c mpenzi wa sinema za nyumbani kwtu ila hiki kipande kimechezwa vyemw akuna mapunguvu yyte yla kiukweli

Anonymous said...

Mi mwenyewe niliiangalia same girl nikachukia sana hasa part 2 wanajikumbusha weee yan hawa wasanii we2 cjui vp jamani nampenda sana aunt ila hyo filamu ya same girl ya hovyo sana!naomba kuwasilisha

Anonymous said...

nimecheka sana namkubali JB anajua kuact ,itabidi niagizie hii movie labda inaweza kuwa ina maadili ya kitanzania maana hizo movie za kibongo upuuzi mtupu movie ya kibongo niliyoipenda ni ile inayoitwa masaa 24 mpasuko moyoni lkn huu ujinga mwengine wote uniofuta sipotezi ime yangu kuuangalia