Monday, October 3, 2011

NAOMBA RADHI KWA KUWA KIMYA KWA MUDA WOTE HUO

Nimekuwa kimya kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja sasa, kuna wengi wametuma comments negatives and positives kulalamikia hali ya ukimya wangu.. lakini kiukweli kabisa kwa wote waliotuma comments ziwe mbaya ama nzuri nathamini sana kwakuwa mnanithamini pia na ndiomana mnapoingia na kukuta hamna kitu,kidogo mnakuwa mnakwazika na kuongea vile ambavyo mnaongea..

Siwezi kutoa sababu ya ukimya wangu sababu ni nje kidogo ya uwezo lakini sababu haikuwa ni kukosa habari ama vitu vya ku-update sababu katika maisha ninayoishi kila siku nimezungukwa na habari kuanzia kwa wenzangu walionizunguka mpaka kwenye vipindi ninavyofanya on TV and radio hivyo sio mtu wa kukosa cha kuweka humu.. ila ninachoweza kusema ni mambo tu yaliingiliana na kauzembe kidogo kutokana na kutingwa na vitu vingine naomba nikiri hilo.. hivyo kutokana na sababu hiyo ambayo wengi wenu hamtanielewa sina budi kuchukua nafasi hii KUOMBA RADHI KWA WOTE ambao hawakupendezwa na hili..

Nawapenda WOTE mnaonipenda na kunichukia sababu naamini wote mna sababu za kufanya hivyo na hata kwa wale wanaonichukia bila sababu pia nawapenda sana sababu kuna sababu ambayo wao wenyewe wanaweza wasiijue ama wanaijua lakini wanashindwa kukubali kwamba ndio hiyo hivyo salute kwenu wote sababu mnazidi kunipa changamoto kwenye maisha yangu...

Naamini kila anaeingia humu iwe kwa nia mbaya ama nzuri ananikubali na ni mtu wangu na ndiomana tunaendelea kuwa pamoja!!!!

I AM WHO I AM.. what you see is what you get!!!

LOVE YOU ALL....

10 comments:

Anonymous said...

usijali mupenzi ni kawaida ila usikae kimya sana luv u by Gatuso

Anonymous said...

U DNT CHANGE AT ALL KM VP FUNGA BASI. USHATOA MAEEZO KIBAOOOOOOOOO NA KUJISHAUA KM HUWEZI KOSA HABARI KWASABABU YA KAZI YAKO OK FINE BAADA YA HIYO INSHA KM SI ESEY TUPE BASI TUKIO LOLOTE STILL KIMYA. MSONYOOOOOOO

Anonymous said...

appology eccepted...... endelea kutupa mambo Zamaradi.
Kikky

machota said...

Duh!!!!! Kweli bana! wadau tumedauka mpaka baaaaaaasi!!!! Tuko pamoko kama Zam.... na mket.....

Anonymous said...

Mummy hebu changamka basi, kwa miezi miwili ulifanya vizuri mara ukatoweka kwa takriban mwezi mzima. Lakini usituletee tena picha za Diamond na Wema wakichezeana wala picha za Ireni na Penny wakiyaonyesha mapaja yao manene yaliyojaa cellulites hadharani. Lol.

Anonymous said...

Jaribu kuwa na nidhamu ya matumizi ya wakati yaani time management. Maadamu umeomba radhi tumekusamehe... one last chance...Leticia.

Anonymous said...

kwa kweli kah kama unajua huwezi kutumikia miungu wawili ya nini sasa angaika na mungu mmoja tu hata maandiko ya dini yanakataza bana tumechoka kuombwa msamaha kila wakati halafu hamna effort yoyote wacha hizo kabisa

Anonymous said...

yap hilo muhimu unajua wa tz wengi kuna maneno matatu hivi tunayakimbia katika maisha yetu SAMAHANI, ASANTE, POLE... Nimekukubali kitambo unavyojua kupanga cha kuongea si mtu wa kukurupuka kabisa as tym goes on unazid kunifanya kukukubali zaid na zaid nakumbuka kama si mwanzon mwa mwaka huu niwie radhi,ukaongeza point moja zaid ya kukukubali unajua kuandika sana unajipanga 'thus why nataka kukutafuta tuandike kitabu''nilisoma makala uliyoandika kuhusu ten years ya kumbukumbu ya mshua wako kiukweli umetulia sana upande huo...anyway tuachane na hayo n naandika mengi coz nakukubali...mi nilivyo kitendo cha kuomba msamaha huwa nasahau yote then inakuwa kuanza upya then namuheshimu mtu anayeomba msamaha'kiukweli jaman watu tuwe na nidhamu na tunatakiwa kuappriciate ye kuomba msamaha u know why? si sheria ni ama lazima ku update ni matakwa ya mtu lakin kaona hakufanya hivyo kaomba radhi. so badiliken wajameni dah.....Zama kuna siku nilikataa kutuma maoni kwenye vile visanduku vya maoni vya mahali tofauti tena nikawaambia labda wanilipe kwanza unajua kwa nini?coz unawasaidia katika marketing bila ya wewe kufahamu so comments zote chukulia ni mzuka coz wanakusaidia kufanya yako yakuendeee hahahahaha.Ni hayo tu...No Name

Anonymous said...

Tumekusamehe zama wala usikonde
I love u
Wako
James

Anonymous said...

happy belated birthday Zama... nakumbuka bak in the dayz Muhimbili Primary ulikuwa unasoma na TWIN wako ambaye yeye ni9 kulwa n wewe doto...vp yuko wapi siku hizi?? i dont see u mentioning her hata kwa bahati mbaya.. wot happened to her..Anonymously Me