Friday, October 7, 2011

SIJUI NIELEZEE VIPI NIELEWEKE LAKINI JUA TU NAUPENDA HUU WIMBO KULIKO MAELEZO YENYEWE...Ukiniuliza sababu naweza nisiwe na ya maana sana ya kukupa lakini kwakweli NAUPENDA huu wimbo kuliko kawaida, na nikiwa nausikiliza huwa sipendi kabisa bugdha na ni moja kati ya nyimbo ambazo nikizisikia zinaniingia ile kabisa moyoni ( i feel this song for real yani),Kwa kifupi naweza nikasema ujio mpya wa Sumalee UMETISHA!!!!

Nikianzia na mistari jinsi ilivyopangwa kuna kama kaubunifu fulani hivi kametumika kwenye vina, mdundo wake kama wa ki-kwaitokwaito hivi, na hata idea ya wimbo kwa ujumla..Kiufupi huu wimbo Unanimaliza.. Big Up kwa hilo Suma!!

Tukirudi kwenye Video ndio kabisa yani.. nimependa jinsi wanavyocheza humo ndani, its really nice na kingine hata sumalee mwenyewe mwanzo kama haonekani hivi, anakuja kuonekana mwishoni mwishoni mwa wimbo!!! Sidhani kama masikioni mwangu utachuja leo ama kesho.. na mara nyingi huu wimbo ukipigwa nashindwa kuvumulia, ntainuka tu kama nna nafasi hiyo, na hata kama sina nafasi basi hata ntashtuka tu bila kutegemea!!!

NAMSHUKURU SANA SUMALEE kwa kuniongezea furaha kwenye siku yangu ya kuzaliwa kwa kunipa ka-suprise kadogo ambako kana maana kubwa sana kwangu, nafikiri alijua ama alinisikia nikisema kwamba huu wimbo naupenda sana, nilipigwa na butwaa siku ya birthday yangu baada ya Babu tale kunipigia simu na kuniambia kuna mtu ana zawadi yangu nimsikilize ghafla akampatia simu mtu na nikashikwa na butwaa nilivyosikia sauti ikiniimbia HAKUNAGA ambapo sauti hiyo ilikuwa ya sumalee mwenyewe.. I felt soooooo GOOD aisee and i really really appreciate kwa hilo suma...

KIUKWELI HATA KAMA KUNA MTU ANAUPENDA HUU WIMBO SIDHANI KAMA ATAKUWA KANIZIDI MIMI...

I LOVE the SONG!!!

7 comments:

Anonymous said...

Wimbo mtamu mbaya hapo hakunaga ubishi kabisa,hakunaga kugombana hakunaga kukataaa hakunaga kuchukia yaan hakunaga hakunaga.No Name

Anonymous said...

HAKUNAGA KM ZAMA HAKUMANAGA

Anonymous said...

USWAZI KWETU YAANI WATOTO HUWAELEZE KITU NA HAKUNAGA KILA KITU NI HAKUNAGA YAANI NI BONGE LA WIMBO HALICHOSHE NA LIKIPIGWA LAZIMA MZUKKA UPANDE HAKUNAGA KM SUMA LEE HAKUNAGA

Anonymous said...

hapybdy zama-lucy

Anonymous said...

hata mimi huu wimbo ndio kwanza nausikia lakini nimetokea kuupenda gafla kwa kweli sauti nzuri maneno mazuri sana hauchoshi kusikiliza kila saa lakini kitu kingine mimi naona kw upande wangu ni mpangilio ya video sio mzuri narudia tena wimbo mzuri sana sana kwakusikiliza lakini kwa kwakuangalia hiyo shoo sio nzuri kiimpangilio yaani huo wimbo najinsi alivyoekti sio kabisa haviendani

Anonymous said...

zama hii nyimbo ni nzuri kweli sijawai kuisikiliza, haswa hao wahusika wawili mtu na mpenzi wake, wameua kabisa, yani ni wanakipaji haswa, wameuvaa uhusika asilimia 100 hata mimi nasema BIG UP Suma

Anonymous said...

kweli wimbo ni mzuri lakini action za kwenye video na wimbo ni tofauti yaani vitendo havifanani na maneno ya kwenye wimbo kabisa kucheza ndio lakini action 0