Monday, October 3, 2011

UNAMKUMBUKA HUYU!!!????Anaitwa MLOPELO, kwa wale ambao ni wafUatiliaji wa maigizo ya kaole kipindi hiko hatakuwa mgeni kwenu, alikuwa akiigiza kama mchawimchawi hivi akishirikiana na bi mwenda enzi hizo, ila kwasasa ni kama amesimamisha shughuli za sanaa kwa muda kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda wa miaka miwili..

Mlopelo kwasasa anakaa kwao maeneo ya TEMEKE akiwa kwa wazazi wake, hajaoa na wala hana mtoto..

Kwa kumuangalia kutokana na umbo lake unaweza ukahisi labda ni mdogo kiumri lakini huo ni udogo wa umbo tu ila kiumri amejaaliwa kula chumvi kidogo kwani kwasasa ana UMRI wa miaka Thelathini na tisa (39).


Mlopelo mbali na sanaa ya uigizaji pia ana kipaji kingine cha kuimba ambacho alifanikiwa kutuonesha ingawa analalamika kwamba redio hazipigi nyimbo yake.

Muda si mrefu nitakuletea kipande cha interview niliyofanya nae ili uweze kujua kwasasa yuko wapi, anafanya nini, pia kipaji chake cha uimbaji nakadhalika...

No comments: