Monday, October 3, 2011

I CANT WAIT FOR MY BIRTHDAY KESHO.. SHUKRANI KWA MAMA YANGU PAMOJA NA WOTE WALIO KWENYE MAISHA YANGU.

Katika tarehe ambazo nazipenda basi nafikiri tarehe 4 ya mwezi wa KUMI itakuwa inaongoza sababu ndio siku niliyozaliwa..
Nakumbuka kwa mwaka niliozaliwa ilikuwa ni Ijumaa lakini kwa mwaka huu tarehe yangu ya kuzaliwa imeangukia Jumanne ambayo ni KESHO....
Always naipenda sana hii siku na naithamini sana na hata kama mtu atanikera kwenye hii siku huwa sipendi kumpa nafasi ya kuharibu siku yangu
I have so many people to THANK lakini mkubwa kuliko wote ni MUNGU ambae bila yeye hakuna mimi na naamini mambo yote yanayonitokea ni matokeo yako WEWE ya-ALLAH, nakushukuru kwa yote na kubwa zaidi kwa kunipatia wazazi ambao umenipatia.

Nikizungumzia wazazi nazungumzia BABA na MAMA... Napenda sana kuchukua nafasi hii kutoa heshima kubwa sana kwa my lovely DAD ambae tayari ameshatangulia mbele ya haki, naamini asilimia kubwa ya Zamaradi anaeonekana leo ni matokeo ya malezi yako wewe, umenilea kwa mapenzi makubwa sana ambayo yalinijenga kwenye mambo mengi sana na kubwa kuliko yote ikiwa ni kujiamini sababu always ulikuwa ukiniambia AM THE BEST na nimekuwa nikiamini hivyo mpaka leo hii. Hivyo kujiamini ulikonijengea kunanisaidia kwenye mambo mengi sana katika maisha yangu mpaka leo hii. Upumzike kwa amani!!!

Nikirudi kwa upande wa MAMA nafikiri inajulikana kwamba hakuna kama MAMA duniani, mama ndio kila kitu na napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru kwa mapenzi ya DHATI na UKWELI alionionesha tangu utotoni na ambayo anaendelea kunionesha mpaka leo.. mapenzi yako hayalingani na mtu yoyote katika dunia hii, wewe ni mtu ambae hata wote wanitenge wewe utakuwa upande wangu, ni aina ya mtu ambae maumivu yangu ni maumivu yako, ni mtu ambae unafurahia kwa dhati kabisa mafanikio yangu na pia ni mtu ambae Unaumia kiukweli na kuanguka kwangu...


Hakuna zaidi yako mama


LOVE YOU MAMA, VERY PROUD OF YOU!!!!!
Mama kiufupi siwezi na wala hakuna neno ambalo litaweza kuexpress mapenzi yako lakini kubwa tu jua NAKUPENDA, NAKUJALI na NAKUTHAMINI kuliko chochote, na kila ninalolifanya kwenye maisha yangu ni kwa sasabu yako.. siwezi kulipa hata robo ya ulichonifanyia sababu mapenzi yako hayafananishwi na chochote, unachotakiwa kujua ni kwamba NAKUPENDA kuliko chochote kile.. wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu, wewe ndio mboni yangu na wewe ndie mzazi pekee uliebakia kwangu, HAKUNA KAMA WEWE MAMA!!

Kuna wengi sana wa kuwashukuru ambao ni ngumu kuwataja wote lakini siwezi kumuacha mdogo wangu wa Pekee ambae huyu ni kilakitu kwangu.. naweza kusema ni kama zawadi aliyoniletea mama baada ya kuishi kwa muda mrefu kidogo bila mdogo wangu .. UMMY nakupenda sana na unalijua hilo, umekuwa ukinisupport kwenye vitu vingi sana katika maisha yangu pamoja na kwamba you are young to me lakini umejitahidi kuwa mshauri mzuri pale ninapohitaji ushauri kutoka kwako.. lol!! Love u soo much ma!! I am your another MAMA.

Watu ni wengi mno waliofanikisha zama kuwa zama, bila kusahau rafiki zangu wote ambao tumeweza kusaidiana kwenye mambo mengi sana shida na raha nyingi tuko wote, na hapa nazungumzia watu wote ambao wamewahi kuwa watu wazuri kwangu kwa kipindi tofautitofauti.. SHAMSA FORD, IRENE, HILDA, nawapenda sana sana wote na nataka mjue kwamba nathamini hata kile kidogo ambacho mliwahi kufanya kwangu haijalishi kwamba mko karibu ama mbali na mimi kwasasa.
Katika vitu ambavyo nimebarikiwa na namshukuru MUNGU ni kuwa na marafiki wengi, I have so many friends kiasi ni ngumu kutaja wote lakini hata kama sijakutaja jua nakupenda na kukuthamini, Hifla, Salome, Edith, husna bila kumsahau Ada(mama malcom) ambae amekuwa akinilea kwenye vitu vingi sana kama mtoto wake (nizoee mama ndivyo nilivyo) lol..

Ukiachana na hao pia napenda kuwashukuru wafanyakazi wenzangu pia ambao tumeweza kuishi vizuri kwa kipindi chote hiki, wengi nikiwa nimewakuta na wakanipokea vizuri mpaka leo hii,tumekutana kwenye mazingira ya kazi lakini tumejikuta tunashirikiana kwenye mambo mengi sana na kuunda urafiki kwa baadhi yao, ni ngumu kutaja wote lakini jua tu nawapenda sana pia.. Mully B, Dina Marios, Da Geah habib (VIP) hahaaa unajua huwa tunasumbuana wapi, Kibonde, Kayanda, venture, dee, Junior, Raymond Charles, P.diddy, da asma, Da Regina,Simalenga, Nugaz, dozen, Mwabulambo, bonge,barbara hassan, Babu tale (jirani), Suka, Jimmy jam, Soudy Brown (naomba flash. lol) Gerald hando ambae amekuwa ni mshauri wangu kwenye mambo mengi ya kikazi, Reuben ndege, brother Sebastian na wafanyakazi wenzangu wooote.. Dah ni ngumu sana kutaja wote maana ni wengi mno lakini nawathamini woote!!!

Pamoja na MA-FANS wangu woote ninaowafahamu na nisiowafahamu wote wanaonissuport nawashukuru sana!!

Bila kumsahau Boss wangu Ruge Mutahaba ambae ameweza kunionesha mwanga kwenye mambo mengi sana pamoja na maboss zangu WOOTE!!
SHUKRANI ZA DHATI na MUNGU AWABARIKI WOTE!!!

12 comments:

Machota said...

Happy Birthday Zam!!!!!! Mungu akujalie maisha marefu na yenye mafanikio teeelee!!! Peace!

Anonymous said...

happy birthday dear, mungu akujaalie kila la kheri katika maisha yako. maneno yako yamenigusa sana nimesona mpaka machaozi yamenitoka! nakupenda sana Zama.

Anonymous said...

UYooo katoto kamekuwa kakubwa leo kanatupa habari jaman kazama Hp Bdya mamito umefanana na mama uwiii by Gatuso

kikky said...

Happy Birthday Zamaradi, wish you all the best in your future endeavors.
Kikky

Thec la said...

May you be gifted with life's biggest joys and never-ending bliss. After all, you yourself are a gift to earth, so you deserve the best. Happy Birthday.

Anonymous said...

happy birthday Zama, nakupendaga sana wewe dada ingawa sikujui ila natamani uwe rafiki yangu.

Hilda

RUKIA said...

jamani maneno mazuri, happy birthday, RIP mzee mketema, jamani mama zamaradi pande za kinondoni studio nikipita pale lazima niingie kumpa HI! Hongera sana

mama 2 said...

Happy Bday Zama! unafanana na mama wewe! mama ana mvutoooo! hongera mtunze ili uendelee kujivunia mamayo.

Anonymous said...

hongera ya kuzaliwa zama ila umeshukuru wengi japo kwa uchache kwani wote nafasi haitoshi lkn kuna nafasi moja ya pekee hatuja iona ya mwandani wako vp?

Anonymous said...

Zama nitakutafuta tuandike kitabu dah unajipanga sana na unajua nini huwa unaandika. H.bday mdada Mungu akujalie maisha marefu yenye kila la kheri.No Name.

Anonymous said...

Happy birthday zama ingawa mimi na Da hu ujatuandika lkn na cc ni watu wako wa karibu.
Wako
James

Anonymous said...

Namsaidia Zama jamani kama alivyowahi kusema Mwana FA 'siwezi kuwataja wote ila naacha nafasi kwa mkono wako add jina lako' msimlaumu Zama kwa kusahau kuwaandika James na Da Hu naamin alikuwa so Happy and excited na b.day yake ukicheki na surprise zile daaaaaa.No Name