Thursday, February 17, 2011

UNAMFAHAMU NDEGE MWARABU!!!!?????

Anaitwa ndege mwarabu lakini jina lingine SAFISHA JIJI na jina hilo limetokana na ndege huyu kuwa anakula uchafu mbalimbali na hiyo ndio ikamfanya aitwe safisha jiji.... na hii ni aina ya ndege wanaopatikana kwa wingi zaidi kanda ya ziwa.. na wanapenda sana kukaa maeneo ya mabucha, ufukweni mwa maziwa na ni mlaji mzuri wa mizoga.

Hapa nilikuwa nikijaribu kumlisha huku nikiogopaogopa... I love this pic kwasababu ya huyu ndege..
Hawa ndege wanavutia sana kwa kuwaangalia na wana midomo mirefu mno..Niliwapa chakula nikaona kama wananijia hivi nikawa najaribu kuwakimbia ingawa watu waliniambia huwa hawadhuru kabisa..
Hapa nikielekezwa na mwenyeji jinsi gani ya kuwalisha hawa ndege, maana ukiweka mikono yako vibaya wanaweza wakakudhuru pia....
Wakiwa kwa nyuma yangu...
Baada ya kuwashangaa ndege tulihamia kwenye sekta nyingine ya samaki na huyo unaemuona hapo ni samaki aina ya KAMONGO (nafkiri umeshamsikia MR. EBBO akiimba kamongo umemfanya nini pegere), sasa huyo ndio kamongo mwenyewe ambae ameshikwa hapo, na anasemekana kuwa ni mtamu kuliko samaki yoyote.
Hao ndio ndege SAFISHA JIJI ambao wanapatikana maeneo ya MWANZAna hilo ni jina nililopata kulingana na watu waliuokuwa eneo hilo.

1 comment:

Anonymous said...

bila shaka hao ndege waliokuwa wakikufuata kwa nyuma ni madume lol!