Monday, February 7, 2011

ASHA BARAKA AKIRI KUUMIA KUONDOKA KWA NYAMWELA!!!!

Bendi ya Twanga pepeta imepata kama pigo baada ya kuondokewa na wafanyakazi wake WATANO kwa mpigo ambao ni ALEX FERGUSON ambae alikuwa ni rapa, SUPER DANGER (Dancer), Otilia (Dancer), ROGERT HEGA CARTEPILLAR (muimbaji) pamoja na SUPER NYAMWELA ama NYAMWELA ambae ni Dancer wa siku nyingi sana wa TWANGA PEPETA ambae alikuwa kama kitambulisho cha bendi hiyo, kwani ulikuwa ukizungumzia madancer basi jina la nyamwela litakuja la kwanza kwa upande wa wavulana...

Pamoja na wote hao kuondoka, ASHA BARAKA haikuwa kitu kwake ila ameshindwa kuficha machungu yake na kukiri kwamba NYAMWELA ndio mtu pekee ambae kuondoka kwake kumemuumiza sana na wala hajaona pengo lolote kwa hao wengine ila NYAMWELA.

SUPER NYAMWELA amekaa kwa muda wa takribani miaka kumi na moja na bendi ya twanga pepeta lakini mwaka huu amechukua uamuzi mzito wa kuihama TWANGA PEPETA na kuelekea EXTRA BONGO CHINI YA ALLY CHOKI na timu nzima hiyo.

Kwa habari zaidi sikiliza AMPLIFAYA na Millard Ayo kupitia CLOUDS FM RADIO kuanzia saa MOJA kamili usiku mpaka TATU usiku LEO.

No comments: