Monday, November 12, 2012
STAY TUNED... BACK sooon...
Thursday, November 10, 2011
MWINGINE HUYO.. GUESS WHO!!
MMEPATIA.. lol



G5 click wanakuletea.. BODA KWA BODA beach concert!!

BODA KWA BODA BEACH CONCERT ON 12th Nov.....,here comes what you have been waiting for tz BODA KWA BODA BEACH CONCERT..Stage will be covered by Jaguar from Kenya ,Sumalee,Country boy & Stamina,GodZilla,Aslay,Beka,Reycho,Young D and many more.Dj Zero will be on the mix to make the crowd going crazzieeee with the hottest hitz.
ENTRANCE : 10,000tshs
VENUE: MBALAMWEZI BEACH "the finest beach"
TIME: 7pm
Monday, November 7, 2011
GUESS WHO...!


HONGERA SANA VENTURE kwa kutuletea BABY GIRL...
Friday, October 28, 2011
MOJA YA SCENE ZILIZOWAHI KUNIFURAHISHA ZA FILAMU...
Haimaanishi kwamba hiyo filamu ndio the best film hapana, ila ninachozungumzia ni kipande nilichokipenda ambacho kinapatikana kwenye filamu inayofahamika kwa jina la MTAANI KWETU..
Kizuri lazima kisifiwe na hata pale tunapoenda tofauti lazima tuongee pia lengo ni kusonga mbele zaidi na hakuna chuki binafsi..
Hiko ni kipande kinachomuonesha Richie kama mtu aliepoteza mtoto wake sasa anakwenda polisi kuripoti akiwa na jirani yake kufika huko kuna madhila yanayomkuta pamoja na kwamba amepotelewa mtoto wake...
Nikikiangalia hiki kipande mara nyingine kinanichekesha kutokana na Transformaton ya uso wa Richie ambae mwanzo aliingia na mbwembwe zote polisi huku akionekana mjuaji na mjanja mwingi lakini anapopewa kibano na anapobadilika hata uso wake unabadilika na anaonekana mdogoo tofauti na alivyokuwa mwanzo..
Kikubwa ni uhusika aliouvaa Richie na wote wengine, lakini kwa richie zaidi ni ule uhusika wa uso wake ulivyokuwa na ile transformation ya hatari iliyotokea kwenye uso wake..
Zaidi angalia hapo juu...
Wednesday, October 26, 2011
THE LOST ADAM - moja kati ya filamu nilizozipenda kwa mwaka huu...
Nimeangalia filamu nyingi sana kwa mwaka huu na hiyo ni kutokana na kazi yangu pia.. Kiukweli kuna improvements nyingi sana kwenye filamu zetu kwasasa lakini mara nyingi kitu ambacho huwa kinatuangusha ni STORY za filamu zetu.. nyingi ziko too shallow, na haya mambo ya part one na two ndio kabisa yanazidisha u-shallow kwenye filamu
Lakini pamoja na kwamba story nyingi ziko Shallow, bado kuna watu ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye filamu, ambapo hata kama story ni ya kawaida utakutaSCRIPT yake imesimama na hata DIRECTOR anakuwa ameitendea haki kiasi kwamba unaangalia filamu na unaona kabisa kwamba hii filamu imedirectiwa..
Moja kati ya filamu nilizoziona na zikanifurahisha kwa mwaka huu.. ni filamu ambayo imedirectiwa na Mtitu Game ambayo inaitwa THE LOST ADAM..
Kikubwa ni Uchezaji wa baadhi ya watu humo ndani.. ni kwamba wamefanya vizuri sana nikianzia na ROSE NDAUKA ambae amevaa uhusika vilivyo kabisa, JACOB STEVEN(JB) pia amefanya vizuri sana na naweza kusema huyu ni mtu ambae kwa movies zake nilizowahi kuangalia naweza kusema Hajawahi kuniangusha.. pia kuna Patcho Mwamba, Hemed Suleiman na wengine wengi ambao kila mtu amekamua kwa nafasi yake..
Kikubwa nampongeza sana Director wa hii filamu kwa kazi aliyoifanya kwani ukiangalia filamu yenyewe unaona kabisa kwamba imekuwa directed na mtu ambae yuko serious na anaijali kazi yake, ila zaidi angalia hiko kipande hapo juu ambacho ni MOJA kati ya SCENES nilizozipenda sana kwenye hii Filamu..
Tuesday, October 25, 2011
Thursday, October 20, 2011
KWA KUMSIKILIZA LULU AKIONGELEA MWENYEWE KUHUSIANA NA JUSTIN BIEBER.. BONYEZA HAPO CHINI!!!
LULU na JUSTIN BIEBER by nelly@g5click.com
Hiyo ni Interview niliyofanya nae kwenye redio ambapo amejielezea mwenyewe kiurefu zaidi kwamba, NI kweli?? na kama kweli ni kimapenzi ama kishabiki?? na pia Bieber akitaka mapenzi klwake itakuwaje??
Kwa majibu yote msikilize LULU hapo juu!!!
Wednesday, October 19, 2011
HEMED na MLELA kuja kivingine..
HII NI KWELI..!!?? lol










Hebu angalia hizo picha hapo kwa umakini sana halafu uniambie kuna ukweli wowote katika maana zilizotolewa kwenye hizo aina za ulalaji wa mtu na mpenzi wake!??
Niambie WEWE na YEYE mnahusika kwenye ipi zaidi kati ya hizo hapo juu!!?? na ukiangalia aina yenu ya ulalaji inaendana na jinsi mahusiano yenu yalivyo!!???
LET'S SHARE
Tuesday, October 18, 2011
MLOPELO AILALAMIKIA CLOUDS KWA KUTOPIGA WIMBO WAKE
Msanii wa siku nyingi wa maigizo MLOPELO ambae alikuwa akiigiza kama jini mara nyingi kwa enzi hizo kupitia kaole ameibuka na kuilalamikia CLOUDS kwa kutopiga wimbo wake ambao kwa mujibu wa yeye anasema uko kwenye mahadhi ya R n B..
Kwa kuusikiliza wimbo huo na malalamiko yake bonyeza hapo juu ili uweze kuuusikiliza vizuri wimbo huo na kusema yaliyomo yamo!!!
Monday, October 17, 2011
LULU ANATARAJIA KWENDA EUROPE KUMTAFUTA JUSTIN BIEBER.. ANASEMA ATACHANGISHA HATA KADI KWASABABU HIYO...

Nilipomuuliza sababu ya kumtafuta kama ni ya kishabiki ama ya kimapenzi alijibu kwamba ni kishabiki lakini lolote pia linaweza kutokea,Lakini hapohapo nikataka kujua kama amesahafanya juhudi zozote za kuwasiliana nae akasema kwasasa bado hapana ila anachotaka kufanya ni hiko kumuendea hukohuko kumsaka..
Kuhusiana na NAULI nilipotaka kujua amejipangaje LULU akasema atachangisha kadi kwasababu anaamini kitendo anachotaka kukifanya ni cha kimaendeleo na ni UJASIRI mkubwa kwasababu amejitosa kwenda kumtafuta mtu ambae hapatikani kirahisi hivyo ni USHUJAA..
kabla sijamaliza interview nae nilimuuliza lulu ikitokea bahati akakutana nae na mara itokee JUSTIN BIEBER nae amevutiwa na yeye KIMAPENZI, je atakuwa Tayari!!??? alichonijibu ni kwamba YANI BILA KUULIZA YUKO TAYARI KABISA na hilo sio swali la kuuliza kwani bila wasiwasi atafanya hivyo..
Soon nitakuletea CLIP ya sauti ya interview ambayo nilifanya nae!!
Monday, October 10, 2011
HALI YA KIAFYA YA MZEE KIPARA SI YA KURIDHISHA SANA...





KAJALA - MTOTO WANGU NDIO KILA KITU KWANGU
Hii ilikuwa kupitia kipindi cha TAKE ONE ya Clouds TV ambapo Kajala aliweza kufunguka vitu vingi sana kuhusiana na maisha yake ikiwemo mahusiano yake yaliyopita na P.funk jinsi walivyokuwa wakiishi, siku ambayo hataisahau ambapo aliwahi kupelekwa segerea,kitu kilichosababisha na vitu vingi kuhusiana na maisha yake..
Kwa hayo na mengine mengi bonyeza hapo juu (kwenye video yake) ili uweze kumsikia na kumuona mwenyewe akiongelea kuhusiana na maisha yake!!!!
Friday, October 7, 2011
JINSI WEMA SEPETU ALIVYOVALISHWA PETE NA DIAMOND..
SIJUI NIELEZEE VIPI NIELEWEKE LAKINI JUA TU NAUPENDA HUU WIMBO KULIKO MAELEZO YENYEWE...
Ukiniuliza sababu naweza nisiwe na ya maana sana ya kukupa lakini kwakweli NAUPENDA huu wimbo kuliko kawaida, na nikiwa nausikiliza huwa sipendi kabisa bugdha na ni moja kati ya nyimbo ambazo nikizisikia zinaniingia ile kabisa moyoni ( i feel this song for real yani),Kwa kifupi naweza nikasema ujio mpya wa Sumalee UMETISHA!!!!
Nikianzia na mistari jinsi ilivyopangwa kuna kama kaubunifu fulani hivi kametumika kwenye vina, mdundo wake kama wa ki-kwaitokwaito hivi, na hata idea ya wimbo kwa ujumla..Kiufupi huu wimbo Unanimaliza.. Big Up kwa hilo Suma!!
Tukirudi kwenye Video ndio kabisa yani.. nimependa jinsi wanavyocheza humo ndani, its really nice na kingine hata sumalee mwenyewe mwanzo kama haonekani hivi, anakuja kuonekana mwishoni mwishoni mwa wimbo!!! Sidhani kama masikioni mwangu utachuja leo ama kesho.. na mara nyingi huu wimbo ukipigwa nashindwa kuvumulia, ntainuka tu kama nna nafasi hiyo, na hata kama sina nafasi basi hata ntashtuka tu bila kutegemea!!!
NAMSHUKURU SANA SUMALEE kwa kuniongezea furaha kwenye siku yangu ya kuzaliwa kwa kunipa ka-suprise kadogo ambako kana maana kubwa sana kwangu, nafikiri alijua ama alinisikia nikisema kwamba huu wimbo naupenda sana, nilipigwa na butwaa siku ya birthday yangu baada ya Babu tale kunipigia simu na kuniambia kuna mtu ana zawadi yangu nimsikilize ghafla akampatia simu mtu na nikashikwa na butwaa nilivyosikia sauti ikiniimbia HAKUNAGA ambapo sauti hiyo ilikuwa ya sumalee mwenyewe.. I felt soooooo GOOD aisee and i really really appreciate kwa hilo suma...
KIUKWELI HATA KAMA KUNA MTU ANAUPENDA HUU WIMBO SIDHANI KAMA ATAKUWA KANIZIDI MIMI...
I LOVE the SONG!!!
UNAMKUMBUKA MBONI MASIMBA KWENYE HII VIDEO!!???
Wimbo unaitwa ZUWENA..
Moja kati ya nyimbo ambazo ziliwahi kufanya vizuri na kutamba sana hapa Tanzania kwa kipindi hiko kutoka kwa Mr. Paul ambayo ilikuwa ni katika zile zilizowahi kufanyiwa Copy kutoka kwa wanamuziki wa zamani...
Hivi unafahamu msichana alietumika kupamba video hiyo na kuifanya ivutie zaidi ambapo ndio aliigiza kama Zuwena kwenye hii Video ni MBONI MASIMBA a.k.a Kim K!!???
kama ulikuwa hufahamu hebu icheki hiyo video vizuri.....
Tuesday, October 4, 2011
ASANTE SANA SHAMSA for the CAKE!!!

Mimi ni shamsa hatujajuana jana wala juzi, na wala hatukukutania ukubwani ila ni mtu ambae ukiuliza rafiki wa zama ni yupi basi utatajiwa Shamsa, ni rafiki yangu wa muda mrefu SANA ambae tumepitia mengi pamoja, shida, mitihani, raha na mambo yote tunakuwa wote
Leo mapema asubuhi hata kabla sijaamka ametoka nyumbani kwake mpaka kwangu lengo likiwa ni moja tu kunisuprise pamoja na KEKI hiyo unayoiona hapo.. Am really happy kiukweli na nathamini sana alichonifanyia, it means alot to ME!!!
Kwa leo sina mengi sana ya kuongea ila zaidi ni kukushukuru kwa kuweza kutambua siku yangu hii muhimu na kufanya kitu cha kuweza kunipa na kuongeza furaha katika siku yangu... Thats what friends are for!!!..
Nakupenda sana... Together Forever!!!
Monday, October 3, 2011
I CANT WAIT FOR MY BIRTHDAY KESHO.. SHUKRANI KWA MAMA YANGU PAMOJA NA WOTE WALIO KWENYE MAISHA YANGU.

Nakumbuka kwa mwaka niliozaliwa ilikuwa ni Ijumaa lakini kwa mwaka huu tarehe yangu ya kuzaliwa imeangukia Jumanne ambayo ni KESHO....
Always naipenda sana hii siku na naithamini sana na hata kama mtu atanikera kwenye hii siku huwa sipendi kumpa nafasi ya kuharibu siku yangu
Nikizungumzia wazazi nazungumzia BABA na MAMA... Napenda sana kuchukua nafasi hii kutoa heshima kubwa sana kwa my lovely DAD ambae tayari ameshatangulia mbele ya haki, naamini asilimia kubwa ya Zamaradi anaeonekana leo ni matokeo ya malezi yako wewe, umenilea kwa mapenzi makubwa sana ambayo yalinijenga kwenye mambo mengi sana na kubwa kuliko yote ikiwa ni kujiamini sababu always ulikuwa ukiniambia AM THE BEST na nimekuwa nikiamini hivyo mpaka leo hii. Hivyo kujiamini ulikonijengea kunanisaidia kwenye mambo mengi sana katika maisha yangu mpaka leo hii. Upumzike kwa amani!!!

Nikirudi kwa upande wa MAMA nafikiri inajulikana kwamba hakuna kama MAMA duniani, mama ndio kila kitu na napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru kwa mapenzi ya DHATI na UKWELI alionionesha tangu utotoni na ambayo anaendelea kunionesha mpaka leo.. mapenzi yako hayalingani na mtu yoyote katika dunia hii, wewe ni mtu ambae hata wote wanitenge wewe utakuwa upande wangu, ni aina ya mtu ambae maumivu yangu ni maumivu yako, ni mtu ambae unafurahia kwa dhati kabisa mafanikio yangu na pia ni mtu ambae Unaumia kiukweli na kuanguka kwangu...

Hakuna zaidi yako mama

UNAMKUMBUKA HUYU!!!????


Kwa kumuangalia kutokana na umbo lake unaweza ukahisi labda ni mdogo kiumri lakini huo ni udogo wa umbo tu ila kiumri amejaaliwa kula chumvi kidogo kwani kwasasa ana UMRI wa miaka Thelathini na tisa (39).
NAOMBA RADHI KWA KUWA KIMYA KWA MUDA WOTE HUO

Monday, September 5, 2011
HONGERA DJ VENTURE..... VENCHAAAAAAAAAAAA!!!!
