Saturday, July 9, 2011

JACKY WOLPER ATAKA KUZICHAPA NA RAIS WA SHIRIKISHO...

Katika hali isiyotegemewa na mtu yeyote siku ya jana kwenye kikao kilichoandaliwa na shirikisho la wasanii Tanzania TAFF chini ya Rais Simon Mwakifamba na kuhudhuriwa na wadau pamoja na wasanii mbalimbali, msanii wa filamu Jackline Wolper Massawe alitaka kulianzisha na kuchafua utaratibu mzima wakati Rais wa shirikisho akiendedlea kuhutubia ambapo Jacky alijikuta akichomoka alipokuwa amekaa na kuelekea jukwaa kuu kwa lengo la kumvamia rais wa shirikisho la filamu Tanzania Simon Mwakifamba.

Hali hiyo ilijitokeza baada ya Rais huyo kutoa ushahidi wa magazeti tofautitofauti unaoelezea skendo mbalimbali za wasanii na mmonyoko wa maadili ndani ya industry ya filamu kitu ambacho inasemekana kilimkera Wolper kwa kuona rais ni kama anawagandamiza badala ya kuwatetea wasanii wake, hivyo akaona njia pekee ni kumdiscipline rais huyo kwa kutaka kumvamia pale jukwaani alipokuwa.

Zoezi lake hilo la uvamizi halikuweza kufanikiwa kwani alijikuta akitaitiwa na mabaunsa waliokuwa standby kwa ajili ya kazi hiyo na hivyo kuzima harakati zake hizo za uvamizi katika jukwaa hilo ambalo lilisheheni viongozi tofautitofauti wa shirikisho la filamu.

Juhudi za kumtafuta jacky pamoja na Mwakifamba zinaendelea ili waweze kuongelea swala hili kwamba ilikuwaje..
Hiyo ndio hali ilivyo kwasasa kwenye industry ya filamu ambapo kiukweli kumeibuka makundi makubwa mawili ambayo yanapigana vita usiku na mchana, moja likiwa chini ya shirikisho la filamu Tanzania na lingine likiwa ni Bongo movie FC ambao mara nyingi hujihusisha na mambo ya mipira, hivyo shirikisho kupata wasiwasi juu ya uibukaji wa kundi hili jipya kwa kuona kuna kama shirikisho lingine chini ya viongozi wengine ambao sio rasmi hivyo kuhofia kutotambulika kwa shirikisho lenyewe..

NINACHOWAZA hivi jacky angefanikiwa kufika pale ingekuwaje!? Angepigana ama vipi?? na katika kupigana huko angeweza kweli kuzikinga na mwanaume yule!!?? na hata kama angeweza ile ndio Ilikuwa SOLUTION hata kama wanaonewa!?? ama labda alikuwa anafanywa chambo!!?? hayo ni baadhi tu ya maswali ninayojiuliza mimi binafsi ambayo hayahusiani na chochote kile wala upande wowote ule, mwisho wa siku waarabu wa pemba wajuana kwa vilemba bwana kazi yangu ni kukuhabarisha tu ya mjini..
YA NGOSWE MUACHIE NGOSWE!!!

7 comments:

Ciera Rocks Cisuo said...

zamaradi mbona unadharau sana!!!angeweza kumpiga huyo mwakifamba halafu tuone huyo mwakifamba atafanyan nini!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

angeweza tu!!kwani unamchukuliaje mtu mpaka akamfata huko kwenye jukwaa!ina maana kajihakikisha na vinginevyo!!!!!

Bongo Film Data Base said...

jacky alikuwa kama chambo pale uwanjani kwani namna watu wa bongo movie fc walikuwa wamepandwa hasira sana juu ya kuvunjwa club yao na kuwekwa chini ya taff. kwa picha tembelea na utizame zadi kwenye www.bongofilmdatabase.blogspot.com

Anonymous said...

Huyu Jackline Wolper naona amezidi kuwa mgomvi wala hajiheshimu. Wasanii wetu wanatakiwa wawe mfano bora kwa vijana wetu si kama huyo Jacky anayefanya mambo ya kihuni hadharani. Bahati yake mabaunsa walimzuia la sivyo angelitolewa hapo kwa machela kupelekwa hospitali.

Anonymous said...

Jacki wacha ushari, behave yourself please. Ladies don't fight in public.

Anonymous said...

zama usiogope sema ukweli. hili kundi la bongo muvie FC linasadikika kuuza wasanii wa kike kwa mapedeshee kwa kujifanya wanataka michango ya mechi za mpira na mambo mengine amabayo kimsingi hayapo kwenye keundeleza muvi. again inasadikika so nimenukuu kutoka gazeti fulani. anyways kupigana sio ufumbuzi.. hao wanaounga mkono kupigana kwani hawajui kwamba ni kuvunja sheria ya jamhuri? na huyu wolper si ndio kioo cha jamii? mbona kavu sana hawa watu? aarg kwanza ndio maana hata hizo muvi zenyewe zinajieleza kuwa hao ni watu wa aina gani bjjzzzzzyyy!!!!

Anonymous said...

Na juzi wakati wa Ziff walikua na mh flani wa fedha wa huko visiwani, nae kwa totoz usiseme. tembelea kanumba blog utajionea. Mialiko mara 2-2 ya chakula. Mdau hapo juu umenikumbusha ulivyosema wanauzwa kwa mapedeje, sasa naona mpaka kwa waheshimiwa.