Thursday, July 28, 2011

NYUMA YA CAMERA YA TAKE ONE!!!

Kipindi cha TAKE ONE mpaka kikamilike huwa kuna watu wengi ambao wanafanikisha hilo, kazi yangu mimi huwa ni kutafuta materials, kujua nini cha kufanya kwenye kipindi kama producer pamoja na kukipresent nilichokiandaa..

Swala la mwanga sijui umekaaje, upigaji picha pamoja na Set huwa sishughuliki nayo ila kuna watu ambao wao ndio wanafanikisha hilo, watu ambao tunafanya kazi kwa upendo na ushirikiano mzuri kabisa pamoja na masikilizano... watu ambao huwa nyuma ya camera kila wakati ambao tunarekodi na wana mchango mkubwa sana pia kwenye kipindi sababu siwezi kujipiga picha mwenyewe..

Nawazungumzia macameraman wawili ambao wanaijua kazi yao vizuri sana REGINALD MARO (p.diddy) pamoja na RAYMOND CHARLES..

Mbali na kuwa wafanyakazi wenzangu kwangu mimi hawa watu wawili ni kama Brothers kabisa kutokana na jinsi tunavyoishi kwa upendo na bila unafki wowote.

kupitia blog hii leo nimeamua kushow love kwao sababu wanastahili..

SALUTE!!

9 comments:

Hawa said...

Mambo vp Zama! Za swaum,? Nimekupenda sana jana the way ulivyovaa kwenye kipindi cha take one, u looked very smart, I realy like it!! But isiishie Ramadhani tu hata hapo baadae uwe unavaa smtimes!! Just ushauri tu!!
Ramadhan kareem!
By mama wawili!(Mrs. Mjaka)

Anonymous said...

HE JAMANI ZAMA MBNA KIMYA SANA MAMII,UKO OK KWELI JAMANI MY DEAR ME PENDA WEWE SANA SO UCKAE KIMYA MWAYA,POLE NA KAZI.

Anonymous said...

...yawn.

Anonymous said...

UMEISHIWA ZAMA FUNGA BLOG YAKO.

Anonymous said...

Hiki nacho kina kera kweli, umetanga kufungua blog, ulidhani mchezo mbona imekushida, si ufunge

Anonymous said...

umeishiwa lol funga acc ASP.

Anonymous said...

Asalaam aleikum. vipi dada yangu mbona kimya au ndio mfungo wa ramadhani. lkn hata kama ukimya wako ni wamfungo ina maana umeshindwa hata kutuwish wasomaji wako wa blog hii Ramadhani njema? sio vizuri zama,
wako
james

Anonymous said...

we ka binti vipi mbona hu upolodi ma news au swaumu imekua nzito?

James said...

Hi Zama tatizo lako uja weka email wala namba yako ya simu kawma wafanyavyo wana habari wenzio ndio maana tunakundikia humu. Mimi nilikuwa naomba ktk kipindi chako cha movie leo uwafahamishe wacheza sinema kuwa tumechoka kuona twins tower ktk kila sinema wabadilishe maeeneo sio kila sinema wakionyesha town ktk movie wanatuwekea twins tower karibu sinema 10 nishaona hivyo.
Wako
James
James