Sunday, July 17, 2011

TAMKO LANGU..

JICHO LA TATU - TUTAFIKA KWELI?
Nimeona nirudie tu kitu ambacho niliwahi kukiandika nyuma lakini kwa kuongezea baadhi ya mambo pia
Katika Entertainment Industry hapa Tanzania kuna fani tofautitofauti, lakini zile ambazo zinaonekana ziko juu zaidi na zinachukua attention ya watu wengi ni MUZIKI, MITINDO na FILAMU.

Nikianza kuzungumzia Industry ya Filamu ni kitu ambacho kimekua juu ghafla tu miaka ya hivi karibuni, tofauti na Muziki ambayo ni Tasnia kongwe zaidi, Na Industry ya Filamu imeshatoa watu wengi sana ambao mpaka sasa ni MA-STAR WAKUBWA MNO hapa Tanzania na wanaendelea kufanya vizuri.

Kuna Usemi Usemao HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA ambapo maranyingi huwa tunatumia msemo huu kujifariji na kujipa moyo pale ambapo tunaona mambo yanaenda ‘Slow’ ama tofauti na matarajio yetu. Lakini tukumbuke vilevile kwamba NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI na DALILI YA MVUA NI MAWINGU, kwa upande wa wasanii wa Filamu wanaonesha hakuna kabisa dalili ya mabadiliko kati yao, wanaridhika haraka na kusahau walipotoka. Ili kuweza kufanikiwa katika vitu tunavyovifanya siku zote ni Vizuri kuangalia ‘NEGATIVES’ zetu zaidi kuliko ‘POSITIVES’ sababu kwa kuangalia mabaya na udhaifu wetu itatusaidia kuendelea mbele zaidi kwa kurekebisha tunapokosea kuliko mazuri yanayotufanya tubweteke na kuamini kwamba kilakitu kiko sawa wakati huenda ikawa tofauti.

Ili fani zote hizo ziweze kuendelea mbele kuna kitu kimoja kikubwa kinachohitajika sikuzote ambacho ni MEDIA kwa maana ya Vyombo vya habari kama Television, Radio, Magazeti, Mitandao n.k. Kupitia Vyombo vya habari watu ndio wanatambua uwepo wa watu ama kazi Fulani.
Business without advertising ni kama kumkonyeza mtu gizani. Hata kitu chako kiwe kizuri namna gani lakini kama watu hawakifahamu hakitakuwa na faida yoyote, It’s useless. Hivyo kazi kubwa ya Media ni kuripoti habari na mambo mbalimbali yahusuyo tasnia tofautitofauti ikiwemo na WAHUSIKA WENYEWE.

Ikumbukwe kwamba si kuripotiwa kwa MAZURI TU MNAYOYAFANYA bali hata pale MNAPOKOSEA media haitakuwa nyuma kwa hilo. Na hio ni kwasababu tu unapokuwa mtu maarufu wewe ni kioo cha jamii na kama kioo cha jamii watu watataka kujua mengi sana kuhusu wewe sababu kuna wanaotamani pia siku moja wawe kama wewe. Hivyo kama umeamua kuwa Star SAHAU kuhusu PRIVACY.

Lakini kwa upande wa BAADHI ya wasanii wa filamu ambao wao ndio wangeweza kuwa muongozo kwa wenzao hali inasikitisha kidogo, Inaonekana kabisa kwamba wanasahau WALIPOTOKA, Wanasahau kwamba VYOMBO VYA HABARI ndio vimewafikisha hapo walipo, wanasahau pia kwamba wao ni vioo vya jamii hivyo kila wanalolifanya jamii inataka kujua nini kinaendelea katika maisha yao.

Ombi langu tu kwa YEYOTE anaehusika msiifanye hii fani ikaonekana kama ni ya watu waliokosa muelekeo wa maisha wakaona njia pekee ni kukimbilia huku hapana. Baadhi yenu Reaction zenu zinaonesha udogo wa IQ zenu na hiyo inatukanisha moja kwa moja tasnia yetu hii nzima ya Filamu tukichukua kauli ya Samaki mmoja akioza ni wote wakati kuna wengi ambao wanajua nini wanakifanya. Kwenye hiyo ni kama inawaharibia. Filamu ni Ulimbukeni na Ujuaji mtupu uliojaa huku.

Hebu jiulizeni kuna Mastar wangapi wakubwa hapa Tanzania wame-struggle mpaka kufikia walipofika si kijina tu bali hata Kiuwezo na bado wanaheshima na kuheshimika katika jamii, hawajisahau. Mfano mzuri ni lady Jaydee ambae ni mwanamuziki, This is a real Diva na mfano mzuri wa kuigwa na watu wa tasnia zote kwa sasa, mafanikio yake yanaonekana waziwazi na hiyo ni kutokana na msingi mzuri aliojiwekea , lakini mbona hana majigambo na hizo Showing off za kienyeji!!! I RESPECT THIS WOMAN. Sidhani kama angekuwa na hizo mbwembwe mlizonazo angefika hapo alipo.
Mnachotakiwa kujua ni NO ONE IS PERFECT, kila mtu hukosea si wewe wala mimi, hata wakubwa wa nchi hukosea pia maranyingine na ndiomana kukawekwa washauri, Ubinadamu ulizingatiwa.

Sasa wewe unapokosolewa DON’T TAKE IT PERSONAL sababu hakuna mwenye Chuki na wewe, lengo ni kujenga na si kubomoa, WEWE NI NANI mpaka upambwe kila siku!? Mbona mnapenda SIFA tena zile za kijinga?? Badilikeni jamani ni aibu, nafikiri mngekuwa mnajua mastar wenzenu wa ulaya wanaishi vipi sidhani kama mngelalamika eti kwa KUKOSOLEWA FILAMU.

AMKENI JAMANI, nafikiri wengi wenu HAMJITAMBUI!!, hamjijui nyinyi ni wakubwa kiasi gani, mngelifahamu hilo msingekuwa na hoja za kitoto kama ambazo wengi wenu mnazo, nyinyi ni VIOO VYA JAMII, mtu yoyote ambae ni kioo cha jamii hawezi kufanya madudu hadharani na watu wakakosa kuongelea (media) sababu hauko kwa ajili ya familia yako, ila uko kwa ajili ya jamii nzima, na unapoongelewa HUKO SIO KUINGILIA UHURU WAKO na wala hakuna mwenye chuki na wewe, mtu akuchukie kwa kipi!!??? ama Mnakutana wapi!!?? anakuongelea kwasababu wewe unastahili kuwa mfano kwa wengine wengi ambao wanakuangalia,wewe ni Public figure..

Kumbukeni kwamba hapahapa TANZANIA tu kuna aina fulani ya watu(a certain class of people) ambao bado hatujafanikiwa kuwateka kuangalia hizi filamu zetu, mkatae mkubali hili liko wazi, na kazi kubwa inayotakiwa kufanywa ni kuangalia jinsi gani tutawavuta hawa ili wote tuwe kwenye boti moja, HATULAUMIANI kwenye hili kwani industry yetu bado changa sana, lakini pamoja na uchanga wa industry yetu, tusioneshe basi kwamba hata akili zetu ni changa pia katika kuchanganua mambo jamani, nyinyi ni wakubwa MNO na mnaangaliwa na watu wengi sana hivyo acheni utotoutoto na KUJI-HISIHISI kusikokuwa na sababu.

Mara nyingi huwa tunajipa moyo tunavyoona filamu zetu zinakubaliwa sana nchi jirani kama RWANDA, BURUNDI na CONGO.. labda niwape siri moja kwamba sababu kubwa ya kufurahiwa hivyo ambavyo tunafurahiwa ni kwasababu ya LUGHA YA KISWAHILI ambayo tunaitumia na wao wanaielewa kirahisi na si kwamba filamu zetu ni nzuri saana kupita wengine, na ndiomana nchi kama UGANDA ambao ndio tuko karibu nao zaidi Hatupokelewi kihivyo kama ilivyo nchi hizo nyingine(language barring)...
Pamoja na kwamba hiko ni kitu cha kujivunia (kupokelewa kwetu vizuri) tusibweteke basi badala yake tuongeze juhudi ambazo hata mtu ambae haelewi lugha yetu akae chini na kuangalia na kusema hii ninayoangalia ni filamu, sababu itafika muda watazoea wataona kawaida na watachoka kwani hata kama kitu ni kizuri kiasi gani lakini kama ni kilekile kilasiku KINACHOSHA na ndiomana hata sisi tumezichoka za NIGERIA kwasasa lakini miaka kadhaa nyuma ilikuwa huambiwi kitu kwa filamu hizo za Kinigeria.. Tujaribu kuwa flexible na tukubali mabadiliko.

Lack of exposure ndio tatizo kubwa linalowakibili wengi wenu, Exposure ni kitu kizuri sana jamani, tusiishie NIGERIA tu, hebu tujaribu kuangalia mbali zaidi, siku zote siri ya mafanikio ni kuangalia wenzenu walioendelea kwenye kitu Fulani wanafanya nini juu ya jambo husika, Hakuna ubaya kuiga kitu kizuri. Tanzania ukishapita mitaa miwili mitatu watu wanakugeuzia shingo na kukuita jina basi unaona umeshamaliza kila kitu na unaridhika kabisa.

Kwa wenzetu mastar wakubwa kila wanachokifanya ni habari na wanaelewa kwamba ile ndio Price of being a superstar, sasa nyinyi kuongelewa filamu tena mara nyingine hata hujaskiliza wewe umefanya tu kuletewa tu habari “INDIRECT SPEECH” ambayo maranyingi kama sio zote haifiki kama ilivyokuwa ndio mnajipanikisha hivyo na mishipa inawasimama. Tutafika kweli? hakuna kitu kibaya kama umasikini wa mawazo/akili, ni bora umasikini wa mali.

Kiukweli mnasikitisha sana na mko kwenye hali mbaya mno bila nyinyi wenyewe kujijua. Acha wanaoendelea kuwasifia ujinga wawasifie na endeleeni kujazana ujinga ila mkikutana na WENZENU wa nchi nyingine ndio mtajiona MKO NYUMA kiasi gani, mara nyingi huwa tunapwaya.
Kibongobongo mtapeta lakini kama lengo ni kufika Hollywood kama mnavyokuwa mnajibu kwenye interview zenu kwa hali hiyo ya kutotaka mabadiliko MNAJIDANGANYA.

Katika maisha yangu mimi ni mtu ambae huwa napenda sana ukweli hata kama utaniuma na sipendi kuukimbia ukweli hata siku moja, acha uniume lakini nijifunze kutokana na huohuo ukweli, tuepuke kuwa wapumbavu, bora tuwe wajinga kwasababu tutajifunza na tutaerevuka, hakuna aliezaliwa anajua, yote tumeyakuta duniani na tunaendelea kujifunza kadri siku zinavyokwenda mbele.

Mwenye masikio na asikie mwenye macho na aone, ni mawazo yangu tu si lazima ukubaliane nayo na hayahusiani na mtu yoyote.

Asante
Zamaradi Mketema.

35 comments:

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe sana sana. Tatizo letu ni kuridhikia na level ya ceiling tuliojiwekea. Watu wanafanya vizuri ila industry haifanyi vizuri hiyo ndo tofauti kubwa, na watu wanachotakiwa kujua ni kuwa huwa kuna kikomo cha watu kufanya vizuri so usipotayarisha industry kuwa tayari kwa mabadiliko ya watu industry inadumaa. Wanaolalamika wanadhani wanasukumwa nje ya tasnia, hakuna atakayewasukuma hiyo ni human nature watatoka tu ila tunachosema sisi wakitoka wao nafasi zao nani wa kuchukua. Utofauti wao uko wapi?? Upya wao uko wapi?? Mi nadhani tuchukulie hizi comments kama changamoto itatusaidia na tusichukulie kama chuki dhidi yetu/ yenu. Mimi sipendi filamu za kibongo sio sababu ya acting mbaya hapana, naamini kuna actors wazuri ila tatizo ni wepesi wa story na script na kutokuwepo kwa directors wanaojua kazi zao. Nahisi ni bahati mbaya sana wote karibu wamekuwa influenced na style moja ya direction ya filam za kinigeria. Nina mengi zaidi ila kwa sasa tujadili tu...

Anonymous said...

hahaaa, Zamaradi mbn umekasirika ivyo? wamekufanyaje hawa watu?? Ila Hapo umenena Zama, nakubaliana na ww 100%...hawa watu the so called stars hawapaendi kukosolewa wanataka kusifiwa tu, kitu ambacho ni upumbavu wa hali ya juu sana, ukitaka maendeleo ya ukwel lazima ukosolewe na anaekukosoa sio lazima awe anakuchukia japo wapo wanaokosoa kwa nia mbaya ila wengi ni kwa ni ya kujenga..Hata Biblia inasema Mwenyezi Mungu anamkekea na kumrudi mtu ampendae iwapo atafanya makosa ili atubu na kujirudi,,Ninyi ni akina nani msikosolewe na media wakati ninyi ni watu maarufu? kama mnataka kuishi maisha binafsi acahaneni na sanaa..

mama rich said...

zamaradi hapo umenena mwanangu

Anonymous said...

true true man!

Anonymous said...

wameambizana wasifanye interview na wewe nini luv? achana nao,jamaa ni malimbukeni sijapata kuona,yani kwanza kitendo cha kujifanya kila mtu lazima awajuwe wao kinabore kichizi, eti mimi ndiyo sijui nani, huwa wanafikili kila mtu anaangalia hizo movie zao za kutowa kila wiki, wenye akili watasikia ulichowaambia si kibaya ni cha maana sana kwao, hawajui kazi ya media ni nini, laiti kama wangelijuwa wangekuwa wanakunyenyekea kulikoni.

Anonymous said...

Asante dada yangu zamaradi,mimi ni mtanzania ninayeishi Calfonia marekani,naomba nikushauri dada yangu nina uhakika hukurazimishwa kuwa mtangazaji wa kipindi cha movie uliamua mwenyewe sasa unapokutana na matatizo kama hayo usikarikike na kujifanya unaandika upumbavu wako hapa eti ukweli ukicompare na hollywood sisi tuko huku hayo unayozungumza kwa mastaa wa huku mbona hatuyaoni wacha kuiwadanganya watu kwa fikra zako duni,hata hollywood hakuna star anayependwa kuandikwa kwa upuuzi hasa kama wenu kwaiyo bongo wakilalamika kuhusu privace zao ni kawaida kote duniani bila shaka hujatembea dunia,kama vipi acha utangazaji wa movie katangaze mengineyo.....ni ushauri tu...

Anonymous said...

Hivi ni lini utaacha kumsakama RAY na KANUMBA? hasahasa KANUMBA?kwani kakufanya nini?mbona yeye katika blog yake hajawai kukusema kwa lolote hata kwa mafumbo?wala kukuandikia makala?unaposema mnapokelewa CONGO,RWANDA,BURUNDI, na unaposema msiishie NIGERIA TU ni dhahiri unamsema KANUMBA,maana yeye ndiye kashatembelea huko na kufanya show na ndiye anayefanya kazi sana na WANIGERIA sasa hilo linakuudhi?mbona wewe hujafika hata Kenya kwa Utangazaji wako?wacha chuki za kijinga na kitoto,jiulize si unasema media inamkuza msanii wewe kwa utangazaji wako na tv na radio yenu mmechangia nini katika ukuaji wa sanaa ya KANUMBA?na mbona kafika hapo alipo na anasonga mbele?tatizo lenu mnapenda kusujudiwa sasa unapoona msanii hataki kuwasujudu mnaanza madongo,wacha fikra za kipumbavu.

Anonymous said...

INAELEKEA MAENDELEO YA KANUMBA HUWA YANAKUUMIZA SANA...ETI HOLLYWOOD MBONA KASHAFIKA HOLLYWOOD,WEWE UMEFIKA WAPI,NDIO MAANA HUNENEPI KWA ROHO MBAYA

Anonymous said...

lakini mi nawashangaa kweli hawa wasanii wawili ray na kanumba, kwanza inaonekana huyo aliecomment hapo juu ni RAY anajifanya mtu kutoka California maana yeye ndio ana matatizo ya spelling na kuchanganya R na L, kwanza nakupongeza sana zamaradi kwa ulichokiandika, nakufatilia sana siku nyingi na kazi zako tangu hujjui we nani unagomabania nyota wa c2c mpaka leo unajitambua, wewe ni bright sana hata ulichokiandika kinaelezea hilo, huyo ray na kanumba mbona wanapenda kujihisihisi, kwani we ni mpinzani wao? uwachukie kwa lipi? ama ni mashoga hao labda maana niliwahi kusikia ray ana hako kamchezo isije ikawa anajiona wewe ni mshindani wake maana mwanaume kukuchukia hivyo mtoto wa kike bila sababu ya msingi inaogopesha kidogo, hawa watu ni malimbukeni sana, nimefurahi sana na hii makala yako, mtu mpumbavu pekee hapa ndie ambae ataona umeandika ujinga lakini mtu na akili yake hawezi kuona ubaya wa alichokiandika zamaradi, hayo majamaa hasa huyo ray ni mambumbumbu kweli tena mambumbumbu ya mwish0 kabisa. fanya kaZi yako zama achana nao hao.

Anonymous said...

JUZI JUZI NILIMUULIZA MAENEO YA LEADERS CLUB KANUMBA UNA TATIZO GANI NA ZAMARADI AKAJIBU SINA NIKAMUULIZA WHY SIJAWAHI KUKUONA KATIKA INTERVIEW ZAKE AKAJIBU SIJAITWA BADO NIKIITWA UTANIONA NIKAJARIBU KUMDADISI KUONA KAMA ATAJIBU LOLOTE BAYA KUHUSU WEWE KIUKWELI JAMAA ALIKUWA VERRY POLITE NA MARA ZOTE HUWA YUKO MKIMYA NA MWENYE AIBU TENA KULIKO RAY,ZAMARADI MANENO YAKO MARA ZOTE UKICHUNGUZA HUWA YANAMSEMA KANUMBA AU RAY PLZ LEAVE THEM ALONE.

Anonymous said...

nazi haivunji jiwe wewe...toka umeanza kusema wamepungukiwa nini...pumbavuuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

jiwe limerushwa gizani, ukisikia yalaaaaaaaaaaaaaaaa ujue limekupata.

Anonymous said...

mbona zamaradi hajataja mtu jina, iweje mjimalize wenyewe?

Anonymous said...

hahahaaaaa eti jiwe gizani, ukijihisi ujue wewe, lol!!

Anonymous said...

ukitaka kujua kuwa si wasanii tu wanaohitaji vyombo vya habari bali hata vyombo vya habari vinahitaji wasanii tena sana kuliko wao wanavyowahitaji tizama kipindi chako cha take one kinavyoboa sana na kutia kichefu chefu hakuna jipya kila siku habari zile zile tu tena za kijinga kuhusu wema na uchafu wake,ni kwasababu haushirikiani na mastaa level ili kukipamba kipindi chako kionekane Class,watumie RAY,KANUMBA,JB nk na si kupoteza mda kuandika upumbavu ili kufurahisha nafsi yako tizama vipindi vya movie vya nje uone kama kuna programu za uozo kama zako,tizama chanel E,tizama JARA,MTIZAME MWENZAKO JOYCE KIRIA alivyokuacha mbali kwasababu kaacha malumbano na kusonga mbele,hakuna kazi isiyokuwa na ugomvi hata Joyce kiria anakutana nayo lakini huombana radhi kisha kusonga mbele kushirikiana nao na si kutafuta maneno ya kejeli kuwaandikia,bila hao wasanii wa filamu wewe ungetangaza nini?heshimu mchango wao ndio ulipopata ajira unataka wakusujudu wewe nani kwa lipi na mchango upi ulionao kwao mpaka wakunyenyekee?usipende kutoa mifano ya uongo kuhusu hollywood wakati hujui na wala hujawai kufika,iga mifano ya akina OPRAH WINFREY.

Anonymous said...

mimi ni msanii wa filamu pia na japo si kwa ukaribu sana lakini namjua zamaradi na namjua ray na kanumba, wakati tiko mwanza ray na kanumba walipata nafasi ya kuongea na boss wa zambaradi na kuna mengi sana walimwambia kuhusu zamaradi ambayo mimi binafsi sikuona kama yana msingi,wananchi jkuna kitu hawajui ray na kanumba wanamchukia zamaradi kuliko kawaida na huwa wanaongereaga kabisa mbele za watukuhusu chuki zao kwa huyo mtoto lakini sababu ya kumchukia mimi siioni pamoja na kwamba mi ni msanii na huyo mtoto pia alishawahi kuongelea vibaya filamu moja niliyowahi kucheza na kusema za ukweli simchukii alichoongea ni cha kweli, rakini hao wakikosolewa tu wanamind vby sana, sasa wao kina nani? mi nimefurahi na hii makala, maana lengo la hawa walivyomsemelea kwa bosi wake ilikuwa wanataka afukuzwe kazi nnachocheka mpaka leo yuko hapo clouds na anafanya kazi yake kama kawaida, hiyo ni chuki ambayo haina sababu, mtu kama ray akiwa anashoot filamu haipitagi siku hajamuongelea huyo msichana tupo tunaona na sidhani kama huyo msichana huwa anafanya hivyo, mi nafkiri tuelewe kwamba zamaradi hana chuki anchofanya ni kazi yake, kanumba na ray kwa jinsi wanavyotetemekewa nba watu hawakutegemea kwamba kuna mtu siku moja atajitokeza na kuponda kama wameharibu maana wanajiona kama mungu watu, wapunguze kujikweza maana hata sisi tu wasanii huwa inatukwaza.

Anonymous said...

Sister Zama,nakusihi siku moja fanya interview na the great kanumba zamani nilikuwa namuona kama bishoo na malaya fulani ila the day nilipokutana nae wakati nafanya reseach kuhusu filamu industry in east africa katika ofisi yake sinza niligundua jamaa IQ yake iko juu,anajua mengi na he is polite sema atakuboa kucheka cheka

Anonymous said...

we nae, joyce kiria na zama sawa???? zama kamuacha mbali kabisa joyce kiria acheni unafki, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, huyo joyce hampati zama hata kwa robo, bongo movie dorooo kabisa. take one juu

Anonymous said...

kama umekwazika pole sana zamaradi,kama aliyoyasema mchangiaji mmoja hapo juu wamekuchongea kwa bosi wako jamaa hawafai, watu wote mko wakubwa kama kuna tofauti mnakaa na kuzimaliza maisha yanaendelea, haya mambo ya kuchikiana sijui kuchongeana hayana nafasi katika jamii, hakuna hata mmoja anayemlipia mwenzie maisha,kila mtu anaishi kutokana na utashi wake.zama naweza leta posa kwenu?nakusudia kweli kama utanikubalia!

Anonymous said...

huyu mtoto zama namfagilia sidhani kama mnakumbuka juzi kati katundika mnisi na kiswaili englishi chake !akimtimua aunty ezeckiel. sasa hawa vijana tatizo lao elimu ndogo na hua hawakubali kukosolewa i,mean ray na kandumba.wamejipachika majina mmoja eti ze greti mwingine ze gritisi.ray akiwa anaongea utafkiri anatamka maneno bila hata kufkiria anaongea saaana tu. kandumba yeye bisho na hua anahisi kwamba iq ipo ilaa sivo kama hukubaliani na hili wee kaa ucheki movies zao ndo utagundua iq zao zimefkia wqapi. ni wababe saana hawa vijana.ni hayo tu senkyuuu

Anonymous said...

zama dah! hapo umejua kusema ukweli kweli mwenye macho atayaona uloyasema. kwani umejaribu kuwapa muongozo

Anonymous said...

Zmaradi katika siku ulizoongea leo meongea point sana kikubwa hapa ni exposure hawa wasanii pamoja na barrie of language kwa wasanii wetu.
wataishia hapa hapa tu bongo.

Anonymous said...

wewe-anonymous-unaesema-ndiyo-maana-zama-hanenepi-yeye-amekwambia-anataka-kunenepa?mbona-kuna-watu-wanawish-kuwa-na-mwili-wake-na-wanashindwa,take-ur-dumb-ass-somewhere-else,pipo-just-hating-for-no-reason,we-umesikia-unene-ni-afya?if-u-dont-have-nothing-to-say-shut-f%#ck-up,leave-girl-alone-and-she-look-gergeous-anyway.

Eunice said...

hahahhahahah, ukiona mtu anajibu pasipokuulizwa ujue limemchoma hahahah, mimi sioni tatizo lolote kutokana na hii mada aliyoandika hapa, tena ameandika mada nzuri sana ambayo kupitia hapo ndo tunajifunza, lakini watanzania sio waelewa kabisa, wamekalia majungu na fitina, mi binafsi huwa siangalii bongo movie kbs kwasabu wanaoact wenyewe ni wapuuzi aah............
Wewe ni mtangazaji mzuri sana tena hawawezi kukufananisha hata siku moja na Joyce Kiria, anawabembeleza ili apate habari badala ya kuwaambia ukweli, kutwa anahangaika akisafiri nao badala ya kufanya yanayomhusu, upuuzi mtupu.
Ninayo kibao ya kuandika ila tuishie hapa kwaleo.
KEEP IT UP MDADA, LOVE THE WORK OF YOUR HANDS.

Anonymous said...

me naona sawa km kuna ukweli zama sema ila tafuta cku wahoji ray na kanumba km kuna tofauti kati yenu muimalize kuandika au kubishana kwenye blog hakusaidii kitu ila ray na kanumba wanafanya vizuri mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Anonymous said...

you have written the truth zama 100% ,binfsi i dont watch those the so called bongo movies ,yan ni bora nikalala kuliko kuwaste my time,hawana elimu, washamba,umaskin umewagubika thats why wakipata vijisent wanakengeuka,hawana lolote,bongo bado sana, kwanza waende skul then wajifunze life and finaly wanaweza kugain at least 0.000000001% ya ucelebrity na professnal life,watobolee zama(hakuna cha ray wala kanumba ,wanacopy nigeria2 waambie waende skul,upeo wao mdogo

Anonymous said...

Mi nadhani wengi wetu tunachagua kuhisi tu kuwa kuna fulani na fulani wanazungumziwa wao. Kuna siku niliona kwenye blog ya Kanumba amepiga picha akiwa B&H NY ananunua vifaa vya camera. Kama tunakubali kuwa kule ndo kuna vifaa bora na kiwango chao kiko bora nani anakataa wakati huo huo tukikosoana ili tuweze kufika huko. Nani anazungumzia quality ya picha hapa??? Wenzetu wanashoot on film toka miaka na miaka, sisi tunajitahidi kutoka na vifaa tulivyonavyo na nataka nipongeze ubora wa quality ya picha siku hizi. Ubora wa quality ya sauti ila bado tuna matatizo ya soundtrack, either tunatumia vinanda vya kanisan of very poor quality au loop mbaya za instrumental ambazo sio hata za film. Sasa jamani vitu kama hivyo tusiambiane....??? Mbona tunapenda kutafuta mchawi tu. Zamaradi yuko sawa kabisa na anapokosoa tusiichukulie kama ni personal conflict ila ni changamoto za industry. Huko huko tulikoenda kununua vifaa kuna watu maarufu sana mmoja akiwa ni marehemu sasa Siskel & Ebert...hebu wagoogle muwafahamu ni watu maarufu wa kucritic filam zote zinazotoka. Na jiulize wamekuwa wanafanya hiyo kazi miaka mingi....Ray , Kanunba, Richie, Hemed, Juma, Roza, na yeyote yule aliyechagua kuingia kwenye tasnia hii....changamoto ni yetu sote, tusikalie kuhisi tunanyooshewa vidole.

Anonymous said...

Hawa jamaa mimi nimesikia hadi wamelalamika kuhusu kipindi cha B12 cha diss eti B12 anawasema sana. Jamani zile ni comment za diss zinazotumwa na watu tu, so kama ni kutokuwepo labda kipindi kisiwepo. Mbona wasanii wa bongoflava wanatumiwa diss kila siku na wanacheka na kuchukua kama ushauri tu. tusijishtukie sana, zamaradi mi siamini kama una ugomvi binafsi na hao wanaolalamika. Mi naamini kama ingekuwa hivyo basi b12 nae angekuwa kagombana na wasanii wote maana anasoma diss zinazotumwa kwake.

Anonymous said...

We naye sikupendi unajishaua mno

Anonymous said...

duuu naona mpambano mkali sana hku, aaaah acha niendelee kusoma then ntakuwa wa mwisho kucoments.

Anonymous said...

mi yangu macho tuu

Anonymous said...

KIMTAZAMO WANGU SIONI SABABU YA WACHEZA FILAMU WA TANZANIA WAKIKOSOLEWA KIDOGO KWENYE UKWELI WANAONA KAMA WANAONEWA...HEBU NIWAPENI MFANO MDOGO TU WA MOVIE MOJA YA KANUMBA AMBAYO MONALISA AKIWA NA YUSUPH MLELA THEN KANUMBA AKAWATEKA..ETI KANUMBA ANAWAPELEKA MPAKA HOTELINI NA KUKAA NAO NA KUAGIZA CHAKULA KISHA ANAONEKANA AKIWA NA ILE BASTOLA MCHANA KWEUPE HOTELINI NA ANAIBUSU BUSU....HEEEEEEEEEEE!! HIVI JAMANI KWA MAISHA YA KAWAIDA NI WAPI AMBAPO SOKO LA FILAMU LINALENGA AMBAKO MTU ANAWEZA KUWATEKA WATU AKAZURURA NAO TENA AKIWATISHIA BASTOLA NJE YA GARI HADHARANI?? AU NI WAPI AMBAPO UNAWEZA KUKAA HOTELINI UNAKULA MCHANA HUKU UMEISHIKILIA BASTOLA UNAIBUSU HADHARANI NA WATU WANAKUANGALIA TU??? SASA WASANII WA FILAMU MKIKOSOLEWA HATA KWENYE HILO MNASEMA MNAONEWA??? SIWAFICHI WADAU YANI TANZANIA YETU UKILEMAA KWA KUSIFIWA NA KUAMBIWA KILA UNACHOFANYA NI KIZURI BILA KUKOSOLEWA KILE AMBACHO UMEKIKOSEA HUTOFIKA MAHALI ZAIDI UTAVIMBA BICHWA TU SANA SANA KWENYE FILAMU. UTAZAME MUZIKI WA TANZANIA HASA KIZAZI KIPYA YANI HAO BAADHI YA WASANII WANAOLALAMIKA KUWA WANABANIWA NA BAADHI YA RADIO, UKIWASIKILIZA MASHAIRI YAO NI MABOVU/MEPESI, MIDUNDO HAIELEWEKI SASA UKIMKOSOA NA KUMWAMBIA KAREKEBISHE HAPA HAPA ULETE TENA UTASIKIA ANALALAMIKA ANABANIWA..JAMANI LENGO SIO KUPIGA TU MUZIKI AU KUTOA TU FILAMU ILA LENGO NI KUPATA MUZIKI/FILAMU ZENYE VIWANGO BORA ILI TUZIDI KUTANUA SOKO LA BIDHAA ZETU. HUU NI MTAZAMO WANGU TU AMBAO NIMEUTOA KWENYE KICHWA CHANGU SO SISHANGAI USIPOKUBALIANA NAO MANA NDO MANA HATA SIZE ZA VICHA ZINATOFAUTIANA. ASANTENI.

Anonymous said...

duh Zama una kaz ngumu sana.Maana kam wasanii wanachukulia haya mambo kuwa personal inakuwa ngumu sana aisee.Nakutia moyo uskate tamaa maana unafanya kwa nia njema na kama vipi wtafutekina Kanumba muongee usikie wao tatzo lao ni nini then muanze ukurasa mpya kwa kushirikiana na wasanii ili kuiboresha hyo Tasnia ya Filam.

Anonymous said...

Mmmmmhhhh!!!! amakweli leo msumali umegonga kwenye mfupa, yote waliyoongea wachangiaji wenzangu ni muhimu sana na yana maana moja ya kuboresha, tukubali tusikubali wasanii wa filamu wanapenda sana sifa hata pale pasipo stahili huwezi kusonga mbele anaekukosoa anakupenda jamani si wivu hebu tuliangalie hili kwa makini

Anonymous said...

hahahahahaahhaha dah nilikuwaga wapi sikuipataga hii si mbaya mi nadhani kama concluder yameongelewa mengi juu ila yote yana ukweli ndani yake.
1.Kiukweli movies nyingi za bongo ni hovyo now natazama movie ya bongo ambayo ndugu zangu wataisifia sifia na pia nikikuta kitu kimekwenda wrong hapo hapo naokatisha ujinga wa kubebwa sitaki.
2.Yeah its true hawa wenye vimajina kukosolewa kwao hawataki si wa movie tu wengi mbona wasaniii wa filamu,watangazaji,wanamuziki etc wenye vimajina wana tabu sana na yote haya hata washauri wao ni washkaji tu ambao mawazo na akili zao zinafanana so la maana hapo huwezi kulipata as ushauri toka kwa washauri wao.
3.Pia kuna ukweli usiopingika kweli Clouds wanapenda kuabudiwa mbaya,,,dah to be honest hili clouds hawawezi kulikimbia Clouds wanajiona Miungu vbaya mno kwa lolote wao wanajiona wako right wakati si kweli kuna mambo kibao wanayafanya kiukweli naamin kama kwa mtu ambaye kweli ana nia ya kweli kuwasaidia wasanii wasingekuwa wanayafanya wanayoyafanya.
4.Of coz alichokiandika Zamaradi kina ukwei kimtindo kama tutaondoa hilo tatizo sijui la beef na kina ray n kanumba,kaongea ukweli kama kila siku utataka kuambiwa mazuri tu bila mabaya hatuwezi kuendelea,ila tukikubali na kukosolewa yeah tutapiga hatua kiukweli.
5.kumpambanisha Zama na Joyce its like uchizi hivi unaua kila mtu anajua nini anafanya na wote lengo lao ni moja kusaidia kukuza tansia ya filamu as they say,,ila ukisema sijui nani zaid ya mwenzake sijaona huko kumzid mwenzake kwa lipi,,wote wanazungumzia movies za bongo na ukiangalia kwa makini nia yale yale tu matatizo ya lugha katika filamu,,hayo ya mwendelezo wa party 1 & 2,,labda muwashindanishe katika graphics design za vipind vyao ama siku hiyo wamevaaje nje ya hivyo wako sawa tu labda lingine kubwa wanaweza kutofautiana kwa mmojawapo kuwahi kuizungumzia hot news labda...sidhani kama wao wanafanya mashindano yoyote haahahahah
6.Movie nying za kibongo hazina uhalisia achilia mbali utofauti kati ya movie na movie..nimetazama movie ya irene uwoya uongo mtupu wapi hapa kibongo bongo mtu anamiliki machine gun ya maana then anaitumia waziwazi haahahah nachekaga miye jamani hakunaga bana,,
7.All in All ndo Bongo Hii HAKUNAGA kama BONGO