Thursday, July 21, 2011

NAMISS MUZIKI WA HUYU MTU, NATAMANI KUMUONA TENA KWENYE GAME...


Ukizungumzia mashabiki wa ukweli mpaka sasa naweza nikasema mimi ni mmoja kati ya mashabiki wakubwa sana wa Mr. Nice mpaka sasa.

Inaweza ikawa kama hujanisoma kutokana na mashabiki wake wengi kuwa watoto lakini kiukweli kabisa huyu ni mmoja kati ya wanamuziki ambae aliweza kuteka kundi kubwa sana la watu kupitia muziki wake na kupitia watoto pia ambapo asilima kubwa ya wazazi walijikuta wakimpenda Mr. nice kupitia watoto wao.

Naomba nikiri kwamba mpaka sasa nnaposikiliza mziki wake naendelea kupata hisia ileile ambayo nilikuwa nikiipata enzi hizo ambapo nyimbo zake ndio zilikuwa HIT songs.
Mr. nice alikubalika sana hadi nchi jirani na alikuwa na heshima kubwa mno kwenye nchi hizo ambapo mbali na uimbaji wake vilevile alikuwa akijituma kwenye Stage..

Pamoja na kwamba anaendelea na muziki na kwasasa anafanya live band lakini Naomba nikiri kwamba namiss muziki wa huyu mtu na natamani sana arudi tena kwenye game siku moja kama ilivyokuwa enzi hizo zamani kwani yeye ndio mwanzilishi na mtu wa kwanza kabisa kutambulisha style ya TAKEU na alivuma sana na nyimbo zake kama FAGILIA, KIDALI PO,FRIDAY NIGHT, MAMA, KING'ASTI, FIRST LADY, KIKULACHO ambayo ilikuwa maarufu sana Uganda, BWANA SHAMBA, RAFIKI ambao ni huo wa kwanza hapo juu na moja kati ya nyimbo ninazozipenda kutoka kwake na nyinginezo nyingi sana.

Nyimbo zote hizo zilimpa mafanikio na umaarufu mkubwa sana kwa watoto mpaka watu wazima na kingine kikubwa ilikuwa ni style ya Uchezaji aliyoitambulisha yeye ambapo watoto ulikuwa huwaambii kitu, mtoto akicheza tu basi style ni hiyo bila kujali wimbo ni wa mr. nice ama la.

Fanya kama unawaza tu mtu kama huyu ambae alikuwa ni kipenzi cha watu wengi na hajaonekana kwenye majukwaa makubwa kwa muda mrefu halafu ghafla tu unamuona sehemu kama FIESTA akiperfom HIT zake za enzi hizo, unahisi ataamsha hisia za watu wangapi!!???

11 comments:

Anonymous said...

wengi sana zamaladi mwaya

Anonymous said...

umona zama hebu jamani muekeni

Anonymous said...

duh!UMENIKUMBUSHA MBALI!!!!MUOKENI BHANA FIESTA

Anonymous said...

waooooooooooooooooooh!!jamani kwani fiesta yupo!

Anonymous said...

sana yaani fanyeni awekwe tu!!!!!!!!!!na akiwerkwa cjui atafanyaje!!!!!

Anonymous said...

mimi mtoto wa kiume lakini namkubali samna huyo msellah!awekwe fiesta

Anonymous said...

duh!!!!!itatisha sanaa

Anonymous said...

ebanAn daaaaaaaaaaa!awepo tu huyo ghaina majotrooooooooooo

Anonymous said...

aende zake,,,tutampiga makopooooooooo

Anonymous said...

jamani mi ntafurah akiwepo

Anonymous said...

ooohh! jamani nyimbo hizi zimenikumbusha mbali nazipenda sana. mr nice uko juu kaka fanya utoke tena