Wednesday, February 9, 2011

KIFUA NA MIKONO YANGU VINANIPA CONFIDENCE YA KUTOSHA....

Anaitwa ALLY HASSAN maarufu kama DAX, ni mmoja kati ya ma-model wa kiume wanaofanya vizuri sana hapa Tanzania akiwa na asili ya kimanyema kutoka mkoa wa Kigoma, amezaliwa mwaka 1983 tarehe 8 january akiwa ni mtoto wa TATU kati ya Wanne wa mzee Hassan Ponda.

Mbali na kuwa Model, utamuona DAXX pia kupitia CLOUDS TV ambapo kuna kipindi kipya kabisa kiko jikoni na ndoto zake kubwa ni kumiliki kampuni ya modelling na kuwa producer mkubwa sana wa vipindi vya TV

Ally hajaoa lakini ana girlfriend anaempenda sana anaeitwa JACKLINE LAWRENCE, anasema aina ya mwanamke anaempenda ni yule anaejielewa, mwenye focus ya maisha na mwenye maamuzi binafsi bila kusikiliza maneno ya watu..

Ukimuuliza kitu anachopenda kwenye mwili wake ALLY humention KIFUA CHAKE pamoja na MIKONO YAKE, hivyo ndio vitu anavyovipenda sana kwenye mwili wake na sababu kubwa inayomfanya apende vitu hivyo kwenye mwili wake anasema kwamba KIFUA NA MIKONO YAKE ni vitu vinavyofanya ajiamini sana hivyo anavipenda sababu vinampa CONFIDENCE ya ajabu.

Huyo ndio ALLY DAXX kama ambavyo unamuona hapo juu akishow wat his poppa gave him

8 comments:

Anonymous said...

Sister Zamaradi, naomba tuwache kuyaandika makabila ya Watanzania tunapotoa wasifu wao. Sisi wote tuna makabila na tunayapenda sana makabila yetu. Tujenge Utanzania kabla ya ukabila. Rwanda wamejifunza kutokana na janga la mauaji ya 1994 : Rwanda huruhusiwi katika vyombo vya habari kutaja kabila la mtu ila unaweza kutaja utaifa wa mtu. Siasa za kikabila zimefeli Rwanda, Burundi na Kenya. Wao baada ya kumwaga damu wanataka kuwa kama sisi, sasa sioni sababu ya sisi kwenda kwenye siasa hizo za kikabila zilzofeli. mshabiki wako Arusha.

Anonymous said...

Zama inavyoonyesha na wewe ni Mmanyema, maana unapenda sana kutaja hili kabila sasa wasiokuwa wamanyema huwaweki kwenye wavuti yako??????????????

Maana hata Mwasiti ulisema kuwa ni Mmanyeka tukueleweje????????????????????????????????????????????????????????????????????

Anonymous said...

karne ya 21 bado watu wanatajana kwa makabila yao, ukienda afrika kusini kila mtu ni Msouth Africa, hakuna Zulu, Xosa,Ndebele nk, nashangaa hapa kwetu tz watu bado wnanajivunia ID ya ukabila na mbaya zaidi ni hao wanaojiita wamanyema, Utanzani ndio kabila teule, utanzania ndio National ID yako, umanyema haukutambulishi kokokte duniani lkn utanzania YES, baadhi ya nchi wanajaribu kuondoa hata suala la imani ingawa ni ngumu kidogo kwani dini pia ni kama vyama vinavyoleta mgawanyiko ktk jamii. ungesema ni Mtanzania halisi naona ingependeza zaidi.

Anonymous said...

afu mimi kama mimi huyu kijana ulie muweka hapo sijui ndo mmanyema sijui vitu gani, nimekuwa nikimuona anajiweka sana kwa hawa dada zetu wanaoishi nnje wakija huwatokea mpaka inakuwa kero. Mimi nilishakuja kushtakiwa na zaidi ya mabinti wawili, mmoja anaishi SA na mwingine yeye ni mfanya biashara anatoa bidhaa nnchi za nnje na kuleta nnchini kwetu. Mwambie hivi, yeye ni kijana mzuri tu ila anaelements za kutaka na kupenda kulelewa , ananguvu zake , ni strong, ni model na pia ni mfanyakazi wa clouds, why do that man! Mmanyema acha hizo mzazi unatutia aibu vijana wenzio. Ni hayo tu, zama naomba usibanie please.

D.

Anonymous said...

"Sister Zamaradi, naomba tuwache kuyaandika makabila ya Watanzania tunapotoa wasifu wao. Sisi wote tuna makabila na tunayapenda sana makabila yetu. Tujenge Utanzania kabla ya ukabila. Rwanda wamejifunza kutokana na janga la mauaji ya 1994 : Rwanda huruhusiwi katika vyombo vya habari kutaja kabila la mtu ila unaweza kutaja utaifa wa mtu. Siasa za kikabila zimefeli Rwanda, Burundi na Kenya. Wao baada ya kumwaga damu wanataka kuwa kama sisi, sasa sioni sababu ya sisi kwenda kwenye siasa hizo za kikabila zilzofeli. mshabiki wako Arusha."
Nimependa comment ya anonymous huyo ndio maana nimecopy na kupaste tu kwani alinicover mbaya kwa comment yake!
Ujumbe ufike dada,unavyofanya,blog yako itakuja boa sasa hivi maana unajitahidi kwa kazi yako so ondoa hii tabia ya kupaisha kabila.

Anonymous said...

kama ni mmanyema ana elements za ki-congo so kujipeleka kwa madada wenye ka-uwezo ndo zao lol!

Anonymous said...

Thanks Anony wa 7:31pm na 3:05 pm, hilo nalo neno ati. Kha mtu anakazi , yake tena sio mbaya, pia ni model but still anataka alelewe pia!!!!!!!! what the f..k? ni kitu gani hasa , anakwepa majukumu au ni nini. Mmh ukiolewa na mtu ka huyo basi jua we ndo baba na ndo mama ktk familia atakuachia majukum yote ya familia.

am disgusted.

Koku

Anonymous said...

tumechoshwa na habari hiziz hizi daily tupe matukio ivi hukujua km blog ni km kazi nyingine na yenyewe ina ugumu wake????? tunajua upo mwanza mbn Dinna nae yupo huko lakini anaupdate blog yake?????? usituzingue